Na Cathbert Kajuna - Kajunason Blog/MMG, Manyara
Mkuu wa Mkoa wa Manyara Mhe. Queen Cuthbert Sendiga mapema leo Januari 23, 2024 amefanya ziara ya kukagua baadhi ya miradi inayoendelea katika mkoa wake wilayani Babati.
Ziara hiyo ilianzia katika Ujenzi wa Jengo la Wagonjwa wa Dharula (EMD) katika Hospitali ya Mji wa Babati, ambapo amewataka wasimamizi wa mradi huo akiwemo mkuu wa Wilaya ya Babati Mhe. Lazaro Twange kujitahidi ujenzi wa jengo hilo unakamilika kwa haraka.
Akitoa taarifa Mganga Mkuu wa Mji Daktari Kyabaroti Kyabaroti amesema kuwa jengo hilo lilitengewa Mil. 300 ambapo mpaka sasa lipo katika hatua za umaliziaji na ifikapo mwanzoni mwa mwezi wa Februari litaanza kutumika.
Mkuu wa Mkoa wa Manyara Mhe. Queen Cuthbert Sendiga akiteta jambo na Wilaya ya Babati Mhe. Lazaro Twange mara baada ya kutembelea ujenzi wa jengo la Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Mkoa wa Manyara ililopo eneo la Maisaka Katani kata ya Maisaka, Babati Mjini.
Pia, Mhe. Queen Sendiga alipata wasaa wa kutembelea ujenzi wa jengo la Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Mkoa wa Manyara ililopo eneo la Maisaka Katani kata ya Maisaka, Babati Mjini ulioanza Oktoba 25, 2023.
Mhe. Sendiga amejionea ujenzi huo huku akiwataka wataalamu hao kumaliza kwa wakati bila kutoa visingizio vyovyote vitavyosababisha ukwamishaji wa ujenzi huo.
Ujenzi huo unaogharimu shilingi Mil. 600 ambapo awamu ya kwanza wamepewa zaidi ya mil. 285 kwa ajili ya ukamilishaji wa Boma, msingi mpaka gorofa ya kwanza na sasa ujenzi umefikia asilimia 21.4.
Aidha Jeshi la Zimamoto Walimemshukuru Amiri Jeshi Mkuu Rais Dkt. Samia Suluhu kwa kuendelea kuwezesha majeshi ya Tanzania katika kukabiliana na majanga mbali mbali huku wakimshukuru Mhe. Sendiga na ofisi yake kwa ujumla kuweza kuwawezesha katika miongozo mbali mbali.
Mradi wa ujenzi wa ofisi ya Kamanda wa Polisi Mkoa wa Manyara linalojengwa eneo la mkoani wilayani Babati.
Baadae Mhe. Queen Sendiga alifika katika mradi wa ujenzi wa ofisi ya Kamanda wa Polisi Mkoa wa Manyara linalojengwa eneo la mkoani wilayani Babati. Mradi ulibuliwa baada ya Serikali kuanzisha mkoa wa Manyara mwaka 2002 na ndipo uhitaji wa Ofisi ya Kamanda wa Polisi Mkoa ulipotokea.
Jengo hilo la ghorafa nne ambapo likikamilika litakuwa na jumla ya vyumba vya ofisi 33 kati ya hivyo 06 ni vyumba vya ofisi za maafisa wakuu ngazi ya mkoa.

EmoticonEmoticon