BALOZI NJALIKAI AKUTANA NA BALOZI WA KWANZA WA ALGERIA NCHINI TANZANIA

October 30, 2023

 Balozi wa Tanzania Nchini Algeria Iman Njalikai leo Oktoba 30, 2023 amekutana na kufanya mazungumzo na Mhe. Balozi Noureddine DJoudi, Rais wa Taasisi ya Kimataifa ya Marafiki wa Algeria tangu kipindi cha Ukombozi ambaye ndiye Balozi wa Kwanza wa Nchi hiyo nchini Tanzania mara tu baada ya kujipatia uhuru wake mwaka 1962.


Mazungumzo na Balozi huyo mwenye historia na kumbukumbu kubwa ya uhusiano wa Algeria na Tanzania yalifanyika kwenye Ofisi za Ubalozi wa Tanzania jijini Algiers na yalilenga kuimarisha uhusiano wa kidiplomasia baina ya Algeria na Tanzania.

Mheshimiwa Balozi Joudi alifika Ubalozini kufuatia mwaliko wa Balozi Njalikai kwa lengo la kufahamiana na kumpongeza kwa majukumu mapya aliyokabidhiwa na Serikali ya Algeria.

Aidha, sambamba na kumhakikishia ushirikiano zaidi Balozi Njalikai alimshukuru Balozi Joudi kwa kuendelea kuwa kiungo muhimu katika kuimarisha mahusiano kati ya Ubalozi na Mamlaka mbalimbali za Algeria ikiwemo sekta binafsi.

Kwa upande mwingine, Ubalozi umepokea na unafanyia kazi ombi la Balozi Joudi kuhusu kuimarisha kituo cha Kiswahili kilichopo Ubalozini ikiwa ni pamoja na kuitangaza zaidi Lugha hiyo adhimu kwa kuifundisha kwa WaAlgeria.




Share this

Related Posts

Previous
Next Post »