Picha Ikionesha baadhi ya wajumbe katika kikao cha Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Afya na Masuala ya UKIMWI kilichofanyika Bungeni Dodoma Tarehe 26 Oktoba 2023.
NA;
MWANDISHI WETU – DODOMA
Ofisi ya Waziri Mkuu kwa
kushirikiana na Tume ya Kudhibiti UKIMWI Tanzania, inaendelea kushauriana na
Serikali kuhusu kuwa na chanzo endelevu na cha uhakika cha Mfuko wa udhamini wa
kudhibiti UKIMWI nchini.
Hayo yamesemwa mapema leo
Tarehe 26 Oktoba 2023 Bungeni Dodoma na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu
(Sera Buange na Uratibu) Mhe. Ummy Nderiananga alipowasilisha Taarifa kuhusu Utekelezaji
wa Mkakati Endelevu kwa ajili ya kuimarisha mfuko wa udhamini wa Kudhibiti UKIMWI
Tanzania (AIDS TRUST FUND – ATF), kwa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Afya na Masuala
ya UKIMWI.
Naibu Waziri Nderiananga
alisema, Ofisi ya Waziri Mkuu kwa kushirikiana na Tume ya Kudhibiti UKIMWI (TACAIDS)
inafanya mapitio ya Mkakati wa Ukusanyaji wa Rasilimali kwa kuzingatia wakati,
mwelekeo na mahitaji ya sasa na kupitia upya vigezo na malengo ili kufanya
maboresho kwa kuzingatia Mkakati ulioboreshwa wa kukusanya rasilimali.
Akiongelea suala la kukuza
mchango wa sekta binafsi katika mapambano dhidi ya UKIMWI, Naibu Waziri
Nderiananga alisema, Tume imeanzisha mfumo wa majadiliano na wadau kupitia
vikao ili kujadili uendelevu wa rasilimali za afua za UKIMWI nchini.
“Malengo makuu ya kuanzishwa kwa Mfuko wa ATF
ni pamoja na kupunguza utegemenzi wa rasilimali za kufadhili afua za VVU/UKIMWI
kutoka nje ya nchi, kuongeza uendelevu wa huduma muhimu za UKIMWI.” Alisisitiza
Nderiananga.
Aliendelea kusema kuwa,
Serikali
imeendelea kutekeleza sheria kwa kutenga bajeti ya Serikali kila mwaka kwa
ajili ya mfuko huo, pamoja na kuimarisha ushirikiano na wadau mbalimbali kwa
mujibu wa mwongozo wa mfuko.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Kamati
ya Kudumu ya Bunge ya Afya na Masuala ya UKIMWI Mhe. Stansalus Nyongo alisema
ni vizuri Serikali ikatenga na kuongeza fedha za kutosha kwa ajili ya Mfuko huo wa
UKIMWI na kuendelea kusema kuwa kamati yake ipo tayari kuhamasiha upimaji wa VVU
kupitia mabonanza mbalimbali ya michezo yanayofanyika..
Captions
P1.
P2.