MTANDAO
wa jinsia Tanzania (TGNP) wakishirikiana na Internews kupitia Mradi wa
Boresha Habari watoa mafunzo kwa Wanachuo wanaosoma Masomo ya Uandishi
wa habari katika Chuo Kikuu Cha Huria Tanzania ili waweze kuwa na jicho
la kijinsia kwenye habari.
Akizungumza
jijini Dar es Salaam leo Machi 23, 2023 na waandishi wa habari,
Mwezeshaji kutoka Mtandao wa jinsia Tanzania (TGNP), Deogratius Temba
amesema kuwa lengo la ni kuwaweka waandishi wa habari sehemu nzuri
mapema kabla hawajawa na msongamano wa majukumu pale watapomaliza chuo.
“Tunataka waandishi waweze kuzingatia usawa wa kijinsia katika Uandishi wa habari mbalimbali katika jamii.”
Amesema
zipo habari nyingi kwenye jamii ambazo hazijaandikwa kuhusiana na
wanawake pamoja na makundi ya watu wenye ulemavu ambazo zinaonekana
hazina maana katika uuzaji kwenye vyombo vyao vya habari.
“Habari
hizo ndizo tunazojaribu kuwaeleza waandishi wa habari vijana ili wajue
ni namna gani wanazipa kipaumbele wanapokuwa wanafanya kazi zao.”
Ameeleza Temba
Amesema
kuwa ili kuleta maendeleo lazima habari ziwe zuri na ziweze kuandikwa
kwa kukwepa uzalilishaji wowote wa jinsi ya ME au KE ili kuleta
maendeleo katika shughuli zozote za maendeleo.
Amesema kuwa habari inayozingatia sauti za jinsi zote mbili ya wanawake na wanaume .
Kwa
upande wa Mratibu wa mafunzo wa Mradi wa Boresha Habari kutoka
'Internews', Mariam Oushoudada amesema mafunzo hayo yataenda kusaidia
wanafunzi katika kuhakikisha kunakuwa na uwiano wa uongozi katika tasnia
ya habari.
"Mafunzo
haya tumeona tuyatoe kwa wanachuo wakiwa chuoni yaani mwanzoni kabisa
ili wawe na uelewa wa masuala ya jinsia pale wanapo andika habari katika
vyombo vyao vya habari pale watapomaliza masomo." Amesema Mariam.
Amevitaj
vyuo ambavyo vitanufaika na mafunzo hayo kuwa ni Chuo Kikuu cha
Tumaini, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) ,Chuo Kikuu Huria cha
Tanzania, Chuo Kikuu cha Mtakatifu Augustino(SAUT) na Practical School
of Journalism.
Amesema
Mradi huo utatanua uelewa wa jamii kuhusiana na usawa wa kijinsia
pamoja na kutoa uelewa kwa waandishi wa habari chipukizi ili waweze
kuandika na kuzipa kipaumbele habari za jinsia.
Amesema
mafunzo hayo yatakuwa endelevu pia kutakuwa na atamizi kwaajili ya
kuendelea kuwa nao pamoja ili waweze kuandika habari ambazo zitakuwa na
usawa wa kijinsia bila kukandamiza jinsi yeyote katika jamii.
Kwa
upande wa Mwezeshaji kutoka TGNP Ester Wilium amesema mafunzo hayo
yanawajengea uelewa waandishi wa habari chipukizi kuweza kuandika habari
ambazo hazipendelei na zinaangalia jinsi zote ‘Mwanamke na mwanaume’
ili uandishi wa habari wa sasahivi uwe tofauti na uandishi wa zamani.
Kwa
upande wa mnufaika wa mafunzo hayo, kutoka Chuo Kikuu Huria Tanzania,
Aniva Mwongola amesema kuwa mafunzo hayo atayafanyia kazi kwa vitendo
kwani kumekuwa na changamoto ya waandishi kuandika habari ambazo hazina
sauti za jinsia zote.
“Mafunzo
haya yamenijengea uelewa wa masuala mapana na namna ambavyo nitaweza
kuisaidia jamii kuelewa uhalisia wa jinsia hasa ukiangalia masuala ya
kutambua haki ya kila mwanadamu na kupata fursa mbalimbali.” Amesema
Aniva
Mwezeshaji
kutoka Mtandao wa jinsia Tanzania (TGNP), Deogratius Temba akizungumza
na wanachuo Kikuu Huria cha Tanzania wakati wa kutoa mafunzo ya usawa wa
kijinsia wakati wa kuripoti habari. Mafunzo hayo yamefanyika jijini Dar
es Salaam leo Machi 23, 2023.
Mratibu
wa mafunzo wa Mradi wa Boresha Habari kutoka 'Internews', Mariam
Oushoudada akizungumza na wanachuo Kikuu Huria cha Tanzania wakati wa
kutoa mafunzo ya usawa wa kijinsia wakati wa kuripoti habari. Mafunzo
hayo yamefanyika jijini Dar es Salaam leo Machi 23, 2023.
upande
wa Mwezeshaji kutoka TGNP Ester Wilium akizungumza na wanachuo Kikuu
Huria cha Tanzania wakati wa kutoa mafunzo ya usawa wa kijinsia wakati
wa kuripoti habari. Mafunzo hayo yamefanyika jijini Dar es Salaam leo
Machi 23, 2023.
Baadhi
ya wanachuo Kikuu Huria cha Tanzania wakiuliza maswali wakati wa
mafunzo ya uandishi wa habari za jinsia kutoka Mtandao wa Kijinsia
Tanzania (TGNP) wakishirikiana na Internews kupitia Mradi wa Boresha
habari. Mafunzo hayo yamefanyika jijini Dar es Salaam leo Machi 23,
2023.
Baadhi
ya wanachuo Kikuu Huria cha Tanzania wakipata mafunzo ya uandishi wa
habari za jinsia kutoka Mtandao wa Kijinsia Tanzania (TGNP)
wakishirikiana na Internews kupitia Mradi wa Boresha habari. Mafunzo
hayo yamefanyika jijini Dar es Salaam leo Machi 23, 2023.
EmoticonEmoticon