Serikali ya Norway imeihakikishia Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania ushirikiano katika sekta za kilimo, usalama wa chakula,
nishati, biashara na uwekezaji pamoja na mabadiliko ya tabianchi.
Ahadi
hiyo imetolewa na Naibu Waziri wa Norway anayeshughulikia Maendeleo ya
Kimataifa Mhe. Bjørg Sandkjær alipokutana kwa mazungumzo na Naibu Waziri
wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Mbarouk
Nassor Mbarouk katika Ofisi Ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam.
Balozi
Mbarouk alisema kuwa Norway imekuwa mdau mkubwa wa Tanzania katika
sekta ya afya na imekuwa ikisaidia katika masuala mbalimbali katika
sekta hiyo.
“Katika hii ziara Mhe. Naibu Waziri anatagemea
kufanya ziara ya kutembelea hospitali ya Kiluteri ya Hydom ambayo
imekuwa ikifadhiliwa na Serikali ya Norway……… madhumuni ya zaira hiyo ni
kuangalia ni kwa namna gani Norway inaweza kuongeza ushirikiano na
kuisaidia hospitali hiyo,” alisema Balozi Mbarouk.
Kwa upande
wake Naibu Waziri wa Norway anayeshughulikia Maendeleo ya Kimataifa Mhe.
Bjørg Sandkjær amesema kuwa ameitembela Tanzania kutokana na
ushirikiano imara uliopo baina yake na Serikali ya Norway uliodumu kwa
muda mrefu na ulianza kama ushirikiano wa maendeleo.
“Lengo la
ziara yangu hapa Tanzania ni kuangalia ushirikiano katika sekta ya afya
kwa sababu Norway imekuwa ikifadhili sekta, Mashirika ya Umoja wa
Mataifa, mifuko ya kimataifa, wadau wengine wanaohusika katika sekta ya
afya pamoja na asasi za kiraia zinazofanya kazi na Serikali ya Tanzania
katika kuboresha huduma za afya,” alisema Mhe. Sandkjær.
Hivyo
nitaitembelea Hospitali ya Kilutheri ya Haydom ili kujionea shughuli
zinavyofanyika na kuangalia zaidi maeneo ya ushirikiano katika sekta
hiyo.
Tanzania na Norway zimekuwa zikishirikiana katika sekta za
afya, elimu, uvuvi, nishati jadidifu, kilimo, ushafirishaji na utalii
pamoja na masuala ya bahari.
Next
« Prev Post
« Prev Post
Previous
Next Post »
Next Post »
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
EmoticonEmoticon