JIJI LA TANGA LAMWAGA MIKOPO YENYE THAMANI YA ZAIDI YA BILIONI 2

October 29, 2022

 




Mstahiki Meya wa Jiji la Tanga Mhe. Abdulrahman Shiloo akizungumza wakati wa kukabidhi hundi kwa niaba ya Mbunge wa Jimbo la Tanga Mjini na Waziri wa Afya, Mhe. Ummy Mwalimu kwa ajili ya vikundi vya kiuchumi vya wanawake, vijana na wenye ulemavu kutoka katika asilimia kumi (10%) ya mapato yake ya ndani kushoto ni Mkurugenzi wa Jiji la Tanga Dkt Sipora Liana

Mkurugenzi wa Jiji la Tanga Dkt Sipora Liana akizungumza wakati wa halfa hiyo 
Mkurugenzi wa Jiji la Tanga Dkt Sipora Liana akizungumza wakati wa halfa hiyo kulia ni Mstahiki Meya wa Jiji la Tanga Abdurhaman Shilloo
Mkuu wa Idara ya Maendeleo ya Jamii Jiji la Tanga Bw. Simon Mdende akizungumza wakati wa halfa hiyo
Meza kuu wakifuatilia matukio mbalimbali
Meza kuu wakifuatilia matukio mbalimbali
Mstahiki Meya wa Jiji la Tanga Mhe. Abdulrahman Shiloo wa tatu kutoka kushoto akieleza jambo kabla ya kukabiudhi hundi hizo
Mstahiki Meya wa Jiji la Tanga Mhe. Abdulrahman Shiloo akikabidhi hundi kwa moja ya vikundi vya wakina mama wajasiriamali Jijini Tanga 
Mstahiki Meya wa Jiji la Tanga Mhe. Abdulrahman Shiloo katika akiwa kwenye picha ya pamoja na maafisa kutoka taasisi za kifedha Jijini Tanga mara baada ya kukabidhi mikopo hiyo kushoto ni Mkurugenzi wa Jiji la Tanga dkt Sipora Liana na kulia ni Mkuu wa Idara ya  Maendeleo ya Jamii Jiji la Tanga Bw. Simon Mdende
Sehemu ya wanufaika wa mikopo hiyo wakiwa kwenye halfa hiyo
Sehemu ya wanufaika wa mikopo hiyo wakiwa kwenye halfa hiyo
Sehemu ya wanufaika wa mikopo hiyo wakiwa kwenye halfa hiyo

Na Oscar Assenga,TANGA.


HALMASHAURI ya Jiji la Tanga imefanikiwa kuongeza kiwango cha utoaji wa fedha za mikopo kwa vikundi vya kiuchumi vya wanawake, vijana na wenye ulemavu kutoka katika asilimia kumi (10%) ya mapato yake ya ndani, ambapo kwa mwaka wa fedha 2021/2022 jumla ya shillingi Billion 2,088,530,000.00 zimetolewa kama mikopo isiyo na riba kwa makundi hayo ili kuwawezesha kiuchumi, kulinganisha na Million 943 kwa mwaka 2020/2021. 

Kiwango hicho cha fedha, kinajumuisha fedha zilizopangwa kutoka Bajeti ya mapato kwa mwaka huo, kiasi cha Billion 1,115,607,800.00 pamoja na fedha za marejesho ambazo nazo zimeingia katika mzunguko wa ukopeshaji. 

Akikabidhi mfano wa hundi zenye thamani ya shillingi million 377 kwa vikundi 43 (Wanawake vikundi 31 wakipokea jumla ya shillingi million 266, Vijana vikundi 6 Tsh. 83 M na wenye ulemavu vikundi 6 Tsh. 28 M), ambapo vinahitimisha awamu ya nne ya utoaji kwa mwaka 2021/2022. 

Mstahiki Meya wa Jiji la Tanga  Abdulrahman Shiloow amewataka wanavikundi hao kuzingatia mipango yao na kufanya biashara zenye tija ili warudishe mkopo na kupata faida ya kazi na kubadili hali zao za maisha. 

Amesema fedha hizo sio za bure, ni mkopo, hivyo wanapaswa kufanya utafiti wa biashara sio kuiga kwa mwingine. 

Mheshimiwa Shiloow ambaye alikabidhi hundi hizo kwa niaba ya Mbunge wa Jimbo la Tanga Mjini na Waziri wa Afya, Mhe. Ummy Mwalimu, aliwataka wakazi wa Jiji la Tanga kuwa na imani na Mbunge wao kwa jinsi anavyofanya kazi kubwa ya kuwaletea maendeleo,  na kwamba kila shughuli ya maendeleo, mkono wake upo, na kwamba alipenda awepo katika tukio hilo. 

Awali, Mkurugenzi wa Jiji la Tanga Dkt. Sipora Liana alisema vikundi vinavyopata mkopo safari hii vimetumia njia ya mtandao katika kujaza taarifa zao na kwamba elimu na mafunzo yametolewa kwao na maafisa kutoka Idara ya Maendeleo ya Jamii. 

Kwa upande wake Mkuu wa Idara ya Maendeleo ya Jamii Jiji la Tanga Bw. Simon Mdende amesema hali ya marejesho inakwenda vizuri na kwamba vipo vikundi vilivyomaliza mkopo na sasa wanapata kwa awamu ya pili.

TSAP YAIBUKA NA TAFITI ZITAKAZOBORESHA SEKTA ZA MIFUGO NA UVUVI.

October 29, 2022

 



Afisa Mauzo kutoka kampuni ya Pembejeo za Mifugo ya "Afrifarm" Bw. Emanuel Senge (kushoto) akimuonesha Kaimu Katibu Tawala wa Mkoa wa Arusha Bw. David Lyamongi (kulia) chakula cha Mifugo kinachouzwa na kampuni hiyo mara baada ya Bw. Lyamongi kufika kwenye banda hilo jana (28.10.2022) ikiwa ni muda mfupi kabla hajafunga Kongamano la chama cha wanataaluma wa sayansi ya uzalishaji wa Mifugo na Uvuvi (TSAP) lililokuwa likifanyika mkoani humo. Kushoto kwake ni Kaimu Mkurugenzi wa Uzalishaji na Maendeleo ya Masoko kutoka Wizara ya Mifugo na Uvuvi Bw. Jeremiah Temu.


Mwenyekiti wa Chama cha Wanataaluma wa sayansi ya uzalishaji wa Mifugo na Uvuvi (TSAP) Dkt.Jonas Kizima akiainisha maazimio ya kongamano la chama hicho kwa mwaka huu wakati wa kilele cha kongamano hilo lililokuwa likifanyika jijini Arusha, jana (28.10.2022).



-Dkt. Kizima aziweka wazi..

Kongamano la  Chama cha wanataaluma wa sayansi ya uzalishaji wa Mifugo na Uvuvi (TSAP) lililokuwa likifanyika jijini Arusha kuanzia Oktoba 26 mwaka huu limefikia tamati jana (28.10.2022) ambapo baada ya majadiliano ya kina yaliyokuwa yakihusu tafiti mbalimbali zilizolenga kuboresha sekta za Mifugo na Uvuvi, wataalam hao wamefikia maazimio kuhusu tafiti hizo.

Akizungumza mara baada ya kumalizika kwa kongamano hilo, Mwenyekiti wa Chama hicho Dkt. Jonas Kizima amesema kuwa wanataaluma hao kwa pamoja wamebaini kuwa ni lazima zifanyike tafiti za kutafuta vyakula mbadala na vyenye ubora  vya Mifugo na samaki ili viwasaidie wadau wanaojishughulisha na shughuli za ufugaji kuzalisha zaidi.

“Lakini tumeona athari za mabadiliko ya tabia nchi yanavyoathiri sana uzalishaji wa Mifugo kwa hiyo tumekubaliana ni lazima zifanyike tafiti ambazo zitaibua aina ya malisho na mifugo inayoweza kukabiliana na mabadiliko hayo” Ameongeza Dkt. Kizima.

Dkt. Kizima amebainisha jambo jingine walilobaini kupitia kongamano la wataalam hao kwa mwaka huu  ni umuhimu wa bima ya Mifugo ambapo wamejadili kwa kina umuhimu wa bima hiyo na kuainisha manufaa mbalimbali ambayo mfugaji anaweza kupata kupitia bima hiyo.

“Kingine ambacho kimefanyika kupitia kongamano la mwaka huu ni wasilisho la namna ambavyo taratibu za kitafiti zinapaswa kupata kibali cha maadili yanayohusu utafiti huo hivyo kuanzia sasa kabla hujachapisha tafiti zako kwenye majarida ya mitandaoni ni lazima uwe na kibali hicho kitakachoonesha ni kwa kiasi gani umezingatia maadili ya taaluma hiyo” Amesema Dkt. Kizima.

Awali akizungumza katika hotuba yake ya kufunga kongamano hilo aliyoisoma kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Kaimu Katibu Tawala wa mkoa huo Bw. David Lyamongi amesema kuwa mkoa huo kwa sasa unatekeleza maazimio ya wanataaluma hao kwa vitendo kupitia elimu ya namna ya kuboresha shughuli za ufugaji inayotolewa na Vyuo vya Nelson Mandela, Wakala ya Mafunzo ya Mifugo nchini (LITA) kituo cha Tengeru na Kituo cha Taifa cha Uhimilishaji (NAIC).

“Mkoa wetu ni moja ya mikoa inayofanya shughuli za ufugaji kwa kiasi kikubwa na tayari tumeshaanza kufuga kisasa kwa kupunguza idadi ya mifugo na kuiboresha michache inayobaki ili kumuongezea tija mfugaji mwenyewe na Taifa kwa ujumla” Amesema Bw. Lyamongi.

Akizungumzia kuhusu  kuongeza idadi ya washiriki kwenye Kongamano lijalo, Naibu Katibu Mkuu wa chama hicho Dkt. Zabron Nziku ametoa wito kwa wataalam wa sekta za Mifugo na Uvuvi waliopo kwenye Mamlaka za Serikali za Mitaa kushiriki kwenye kongamano hilo ili waweze kuongeza ujuzi utakaowawezesha kwenda kuwahudumia vizuri wananchi kwenye maeneo yao.

“Lakini pia nitoe rai kwa wadau wa sekta binafsi wanaojishughulisha na sekta za Mifugo na Uvuvi, kushiriki kwa wingi na kuja kutoa elimu juu ya bidhaa mbalimbali wanazozalisha ili wawatumie wataalam  wanaoshiriki kongamano hili kama mabalozi wa bidhaa zao pindi watakapoenda kule chini kwa watumiaji wa bidhaa hizo” Amehitimisha Dkt. Nziku.

Mbali na majadiliano ya kina kuhusu tafiti za Mifugo na Uvuvi, Kongamano hilo la Chama cha wanataaluma wa sayansi ya uzalishaji wa Mifugo na Uvuvi (TSAP) kwa mwaka huu liliambatana na shughuli mbalimbali ikiwa ni pamoja na wanataaluma wa chama hicho kwenda kutembelea hifadhi ya Taifa ya Ngorongoro ikiwa ni sehemu ya kuunga mkono juhudi za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan katika kuhamasisha utalii wa ndani nan je kupitia filamu yake ya “Royal Tour”.

ZAIDI YA TRILIONI 2 KUFANYA MAGEUZI SEKTA YA MIFUGO

October 26, 2022

Kaimu Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi (Mifugo) Dkt. Charles Mhina (kulia) akiangalia mashine ya kukamulia maziwa mara baada ya kufika kwenye banda la Kampuni ya pembejeo za Mifugo ya "Afrifarm" leo (26.10.2022) ikiwa ni muda mfupi kabla ya kufungua kongamano la Chama cha Wanataaluma wa sayansi ya Uzalishaji wa Mifugo na Uvuvi (TSAP) linalofanyika jijini Arusha

3

Kaimu Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi (Mifugo) Dkt. Charles Mhina (kushoto) akielezea umuhimu wa hereni za kielektroniki alipofika kwenye banda la Kampuni ya pembejeo za Mifugo ya "Afrifarm" muda mfupi kabla ya kufungua kongamano la Chama cha Wanataaluma wa sayansi ya Uzalishaji wa Mifugo na Uvuvi (TSAP) leo (26.10.2022) jijini Arusha. Kulia ni Afisa Mauzo wa kampuni hiyo Bw. Emanuel Senge.
Meneja Masoko wa kampuni ya Maziwa ya Asas kwa upande wa kanda ya Kaskazini Bw.Tumainieli Joakim (kulia) akimkabidhi zawadi ya Maziwa Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi ( Mifugo) Dkt. Charles Mhina leo (26.10.2022) ikiwa ni muda mfupi kabla hajazindua kongamano la Chama cha wanataaluma wa sayansi ya uzalishaji wa Mifugo na Uvuvi (TSAP) linalofanyika jijini Arusha. Katikati anayeshuhudia ni Mwenyekiti wa Chama hicho Dkt. Jonas Kizima

Kaimu Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi (Mifugo) Dkt. Charles Mhina (wa kwanza kushoto) na baadhi ya viongozi wa Chama cha Wanataaluma wa sayansi ya Uzalishaji wa Mifugo na Uvuvi (TSAP) wakifuatilia uwasilishwaji wa maandiko ya wanataaluma mbalimbali ikiwa ni sehemu ya kongamano la chama hicho linalofanyika jijini Arusha kuanzia Oktoba 26-28, 2022




Dkt. Kizima abainisha namna TSAP inavyo wainua wataalam mbalimbali wa sekta za Mifugo na Uvuvi

Serikali kupitia Wizara ya Mifugo na Uvuvi imeanza zoezi la utekelezaji wa mpango wa mabadiliko wa miaka 5 wa Sekta ya Mifugo ambao unatarajia kutumia zaidi ya shilingi Trilioni 2 mpaka kukamilika kwake.

Hayo yamesemwa leo (26.10.2022) na Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo kwa upande wa Sekta ya Mifugo Dkt. Charles Mhina katika hotuba yake ya Ufunguzi wa kongamano la Chama cha wanataaluma wa sayansi ya uzalishaji wa Mifugo na Uvuvi (TSAP) uliofanyika kwenye Ukumbi wa “Olasit Garden” jijini Arusha.

Dkt. Mhina ametumia jukwaa hilo kuwasisitiza wataalam waliopo kwenye chama hicho kuendelea kufanya tafiti zenye tija na zinazolenga kuboresha ufugaji na maisha ya wafugaji kwa ujumla ili kuirahisishia Serikali katika utekelezaji wa Mpango huo.

“Mpango huu unalenga kuboresha sekta ya Mifugo kwa ujumla kuanzia katika eneo la uzalishaji wa mifugo hasa katika eneo la uhimilishaji na matumizi ya madume bora ya mbegu, uzalishaji wa malisho kupitia mashamba darasa ambayo tunaenda kuyaanzisha kwenye Halmashauri takribani 100 ili wafugaji wetu waweze kujifunza namna ya kulima mbegu na malisho yenyewe kuanzia kupanda hadi kuyavuna na lengo letu ni kuhakikisha mbegu hizo zinapatikana kwenye maduka mbalimbali ya pembejeo hivyo ninaamini kupitia maandiko yenu kama wanataaluma tutaendelea kupata suluhu ya namna ya kufanikisha hayo ” Amesisitiza Dkt. Mhina.

Dkt. Mhina ameongeza kuwa eneo jingine ambalo Mpango huo utaliangazia ni lile la afya ya Mifugo ambapo Wizara yake imeendelea kuongeza dawa za kuogeshea mifugo na chanjo za magonjwa mbalimbali yanayoikabili mifugo hapa nchini.

“Lakini pia kupitia mpango huo tunaendelea kuboresha huduma za ugani, tafiti na uanagenzi ambapo tumeanzisha Vituo atamizi 8 vinavyolenga kuwasaidia vijana waliopo mtaani wenye taaluma ya ufugaji kujifunza kwa vitendo namna ya kufanya unenepeshaji wa Mifugo ambapo tunawapatia mifugo ya kunenepesha, tunawafundisha namna ya kunenepesha na wakimaliza mafunzo tunawagawia ng’ombe hao kama mtaji wa kuanzia huko waendako na kwa mwaka huu tumeanza na vijana 240” Amebainisha Dkt. Mhina.

Katika hatua nyingine Dkt. Mhina amewapongeza wataalam wanaounda Chama cha wanataaluma wa sayansi ya uzalishaji wa Mifugo na Uvuvi (TSAP) kwa kuandaa maandiko ya tafiti zao na kuziwasilisha ili zijadiliwe kabla ya kuchapishwa kwa matumizi ya sekta ya Ufugaji ambapo amebainisha kuwa utekelezaji wake utakuwa na tija kwa mfugaji mmoja mmoja na Taifa kwa ujumla.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Chama hicho Dkt. Jonas Kizima amesema kuwa lengo la kufanyika kwa kongamano hilo kila mwaka ni kujadili na kuchambua mada za kisayansi zinazoonesha matokeo ya utafiti ili matokeo hayo yapelekwe kwa wadau mbalimbali wa sekta za mifugo na Uvuvi.

“Uchambuzi wa mada hizo ukishakamilika utatupa picha ya aina ya teknolojia zinazopaswa kutumika ili kuongeza tija katika sekta za Mifugo na Uvuvi na matokeo hayo tutayaweka kwenye chapisho kwa ajili ya kutumiwa na wadau wa sekta hizo” Ameongeza Dkt. Kizima.

Dkt. Kizima amesema kuwa machapisho yote ya kisayansi yanayopitishwa kupitia kongamano hilo la wataalam huwekwa kwenye majarida ya kisayansi yanayopatikana mitandaoni ambayo pia huweza kumsaidia mtaaluma husika kupanda cheo kwenye ajira yake na kumruhusu kuyawasilisha katika majukwaa mbalimbali ya wanataaluma.

Kongamano hilo la 49 la wanataaluma litafanyika kwa muda wa siku 3 kuanzia Oktoba 26-28 ambapo mwaka huu linaambatana na dhima isemayo “kuenzi matokeo ya teknolojia na ubunifu ili kuongeza chachu katika maendeleo ya Sekta ya Mifugo na Uvuvi.


BALOZI ADADI AWATAKA WANAFUNZI WA SHULE YA MUHEZA MUSLIM KUSOMA KWA BIDII

October 26, 2022
KAMISHNA wa Tume ya Utumishi wa Umma nchini Balozi Adadi Rajab akizungumza wakati wa maafali ya shule ya Sekondari Muheza Muslim 
Mwalimu Mkuu wa Shule ya Sekondari ya Muheza Muslimu
KAMISHNA wa Tume ya Utumishi wa Umma nchini Balozi Adadi Rajab akigawa vyeti kwa wahitimu wa kidato cha nne  wakati wa maafali ya shule ya Sekondari Muheza Muslim 
KAMISHNA wa Tume ya Utumishi wa Umma nchini Balozi Adadi Rajab akigawa vyeti kwa wahitimu wa kidato cha nne  wakati wa maafali ya shule ya Sekondari Muheza Muslim 
KAMISHNA wa Tume ya Utumishi wa Umma nchini Balozi Adadi Rajab  katikati akiwa na wadau wa maendeleo na wajumbe wa bodi ya shule ya Sekondari Muheza Muslim wakati wa maafali hayo


Na Oscar Assenga,MUHEZA

KAMISHNA wa Tume ya Utumishi wa Umma nchini Balozi Adadi Rajabu amewataka wanafunzi katika shule ya Sekondari Muheza Muslim kuhakikisha wanasoma kwa bidii ili wataalamu mbalimbali waweze kupatikana kupitia huko.


Balozi Adadi aliysema hayo wakati wa mahafali ya shule hiyo yaliyofanyika mjini Muheza ambapo alisema lazima wanapokuwa shuleni waweze kujiandaa na  kuzingatia nidhamu ,malengo na kusoma vizuri ili baadae waje kufanikiwa kupitia elimu.

Alisema kwamba  mitihani inahitaji maandalizi mazuri ili waweze kufanya vema hivyo hawana budi kuhakikisha wanajiandaa ili kuweza kufanya vizuri katika mitihani yao.

Katika Mahafali hayo Balozi Adadi aliendesha Harambee kwa ajili ya ujenzi wa vyumba vya maabara katika shule hiyo ambapo huku akihaidi kuendelea kushirikiana nao katika kuhakikisha wanapata mafanikio.

Kamishna huyo aliuomba uingozi wa shule kwamba hiyo maabara utakapo kamilika ipewe jina la Bahoza Laboratory ili kuwaenzi kwa juhudi kubwa ambazo wamezifanya kufanikisha maabara hiyo.

Hata hiyo Balozi Adadi alisema Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais Samia Suluhu imefanya mambo makubwa na kuleta maendeleo huku akieleza fedha ambazo zinakuja zinatokana na kurudisha mahusiano ya na mataifa mengine ambayo yalikatika na ameyarudisha kwa kasi kubwa.

Alisema kutokana na kurejesha mahusiano hayo yamewasaidia kupata fedha nyingi za kujenga shule, maabara,barabara na kila Jimbo kuhakikisha maendeleo yanapatikana  ule ufufuaji wa mahusiano na  mataifa mengine.

Katika hatua nyengine Balozi Adadi aliitaka Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa nchini kuhakikisha wana buni  mbinu zinazoweza kudhibiti vitendo vya rushwa ya ngono nchini.

Balozi Adadi alisema kwamba vitendo vya rushwa ya ngono vimekuwepo na  Takukuru wamepewa jukumu la kudhibiti  vitendo hivyo ni wakati sahihi kuhakikisha wanakuja na mwarobaini wake.

Alisema kwamba wao wanapaswa kuona namna nzuri ya kubuni mbinu ambazo zinaweza kupelekea 
 kudhibiti badala ya kusubiri matukio yanatokea ndio waweze kuanza kupambana nayo.

" Haya mambo yapo kwa sababu kwenye vyuo hivyo ni jinsi ya vyombo vilivyo kabidhiwa kufanya kazi hiyo wanafanya nini ili kuweza kuondokana na tatizo hilo"Alisema Balozi Adadi.

Aidha alisema kwamba wanataka wanaofanya vitendo hivyo wakamatwe ili iweze kuwa fundisho kwa wengine wenye tabia za namna hiyo kuweza kubadilika hivyo suala hili lina umuhimu wake  hasa chombo ambacho kimepewa mamlaka ya kusimamia.



JIJI LA TANGA LAWAITA WAWEKEZAJI

October 26, 2022
 Mkurugenzi wa Jiji la Tanga Dkt Sipora Liana  wakati akizungumza na Waandishi wa Habari ambao hawapo pichani kuhusu fursa za uwekezaji katika Jiji hilo na namna walivyojipanga kupokea wawekezaji ambao watafika.

 


Na Oscar Assenga,TANGA.


HALMASHAURI ya Jiji la Tanga imewaita wawekezaji  kutoka ndani na nje ya nchi kuchangamkia fursa za uwekezaji zilizopo kutokana na uwepo wa  maeneo yanayotosha kwa ajili ya viwanda hasa sekta mbalimbali ikiwemo  ya Madini.

Hayo yalibainishwa leo na Mkurugenzi wa Jiji la Tanga Dkt Sipora Liana  wakati akizungumza na Waandishi wa Habari kuhusu fursa za uwekezaji katika Jiji hilo na namna walivyojipanga kupokea wawekezaji ambao watafika.

Aliyataja maeneo ambayo yanafaa kwa ajili ya uwekezaji katika sekta ya Madini katika Jiji hilo yapo katika eneo Maere,Chumvini,Kisosora,Ndaoya,Machui,Tongoni, Chongoleani,Mwarongo.

Dkt Sipora alisema katika maeneo hayo yana hekta 212 na yanafaa kwa ajili ya maeneo ya viwanda vya saruji,chokaa,chumvi pamoja na rangi kwamba sababu chumvi inayozalishwa inatumika uzalishaji bidhaa mbalimbali hivyo wanatangaza na kualika wawezekezaji wafika kwa ajili ya viwanda.

"Katika maeneo ya madini tunawaalika  wawekezaji wakubwa na wadogo  wa Madini na chumvi hivi sasa uzalishaji ni mdogo sana unakuta wazalishaji wadogo wadogo wanazalisha kama tani 6000 hazitoshi hivyo tunawaalika kuja kuwekeza na tumehaidi hakutakuwa na urasimu wa kupata maeneo hayo ambayo tayari yameshapimwa"Alisema Dkt Sipora.


Alisema pia katika maeneo hayo yanayofaa kwa ajili ya sekta ya uvuvi yaani uchumi wa bluu kutokana na uwepo wa bahari hivyo kuna fursa ya kufanya uvuvi na kuwaalika wawekezaji wanaoweza kuja kuingia meli kubwa na boti kwa ajili ya kufanya uvuvi.


"Lakini pia unenepeshaji wa magongoo bahari,kilimo cha mwani hao wote tunawaita lakini pia ufungaji wa samaki kwenye vizimba na uvuvi wa kutumia vyombo vya kisasa" Alisema


Alisema wameamua kuwaita wawekezaji hao kwa ajili ya shughuli za uwekezaji na viwanda ambavyo ni muhimu sana huku akieleza Rais Samia Suluhu ametangza ameifungua nchini na kuiunganisha nchi na masoko nje ya nchi hivyo kilichobakia ni wana Tanga waongeza uzalishaji ku
uza nje ya nchi na zile zilizopo kwenye bara la Afrika


"Tunapokuwa na viwanda inasaidia kuchukua nguvu kazi ya vijana ,twaliopo baada ya kilimo wanakuwa hawana cha kufanya kwa hiyo wote watapata ajira kwenye viwanda ambavyo vitaongeza thamani na muda wa kuishi kwa bidhaa husika kwa mfano unaposafirisha machungwa yanaweza kuozea njiani lakini wanapounguza gharama za kusafirisha na kukuta nafasi kubwa inchukuliwa kwenye gari na bidhaa nyengine zinaharibikia njiani hivyo kupunguza upotevu wa mazao na kuongeza thamani ya mazao" Alisema Mkurugenzi huyo.


Aidha aliwataka wawekezaji ambao wanakwenda kuwekeza Visiwani Zanzibar kupitia uchumi wa bluu waona namna ya kugawana na wengi wake Jijini Tanga ambako mako kuna fursa ya uwekezaji huo ambao ni muhimu kwa maendeleo.


Mwisho

Mkurugenzi TSB alipongeza Jiji la Tanga kuzindua kitalu cha Mkonge

October 21, 2022


 

Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Mkonge Tanzania (TSB), Saddy Kambona amewapongeza Mkuu wa Wilaya ya Tanga, Mhe Hashim Mgandilwa na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji, Sipora Liana kwa kuzindua zoezi la ugawaji wa mbegu za Mkonge bure kwa wananchi.

 

Mapema wiki hii, Jiji la Tanga lilitoa bure miche takribani 358,000 kwa wakulima wa Mkonge walioko Kwenye kata sita za halmashauri hiyo.

 

“Natoa pongezi nyingi sana kwa Mhe Mgandilwa na Mama Liana kwa kuzindua zoezi la ugawaji wa mbegu za Mkonge bure kwa wananchi ikiwa ni utekelezaji wa maagizo ya Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe Kassim Majaliwa Majaliwa ambaye aliagiza kuwa kila Halmashauri ya Wilaya, Manispaa na Jiji katika Mikoa inayofaa kwa Kilimo cha Mkonge kuanzisha kitalu cha mbegu za Mkonge kisichopungua ekari 10 na kugawa mbegu bure kwa wananchi.

 

“Hii ni fursa nzuri kwa wakulima wa Mkonge katika Jiji la Tanga, Bodi ya Mkonge inawaahidi ushirikiano wa kila hali wasisite kuwasiliana nasi pindi wanapohitaji ushauri wa kitaalamu na mambo mengine yanayohusu sekta ya Mkonge milango iko wazi,” amesema Mkurugenzi Kambona.

 

Akizindua zoezi hilo la kugawa miche ya Mkonge kwa wakulima hao, DC Mgandilwa alisema lengo ni kuwasaidia wakulima kuongeza uzalishaji na kufikia lengo la serikali la kuzalisha tani 120,000 ifikapo mwaka 2025.

 

“Nawaomba miche hiyo mkaipande kwenye mashamba yenu na si kuiacha ikaharibikia mashambani hapo mtakuwa hamjaitendea haki serikali ambayo imetumia rasilimali kuendeleza miche hiyo,” alisema DC Mgandilwa

 

Pamoja na mambo mengine, baadhi ya wakulima waliopatiwa miche hiyo, wameishukuru serikali kwa kuwapatia zao mbadala la biashara ambalo litawakwamua kiuchumi tofauti na sasa ambapo walikuwa wanategemea mihogo kama zao kuu la biashara ambalo kwa sasa halifanyi vizuri hivyo kuja kwa mkonge fursa mpya ya kujikomboa kiuchumi kutokana na faida zake.

AGIZO LA RAIS SAMIA LAANZA KUTEKELEZA NA TASAC

October 19, 2022

 


Mkurugenzi Mkuu wa TASAC, Kaimu Abdul Mkeyenge akizungumza na waandishi wa habari mjini Kigoma ambao hawapo pichani kuhusu kutekeleza maagizo ya Rais Samia Suluhu kuufanya mkoa Kigoma kuwa Kitovu cha uchumi kwa mikoa ya magharibi nchi za ukanda wa maziwa makuu
Mkurugenzi Mkuu wa TASAC, Kaimu Abdul Mkeyenge akizungumza na waandishi wa habari mjini Kigoma kuhusu kutekeleza maagizo ya Rais Samia Suluhu  kuufanya mkoa Kigoma kuwa Kitovu cha uchumi kwa mikoa ya magharibi nchi za ukanda wa maziwa makuu

Boti za abiria na mizigo zinazofanya safari kutumia ziwa  Tanganyika

                               

Na Mwandishi Wetu ,Kigoma


 SHIRIKA la uwakala wa meli Tanzania (TASAC) limesema kuwa limejipanga kutekeleza kwa vitendo agizo la Rais Samia Suluhu Hassan la kuufanya mkoa Kigoma kuwa kitovu cha biashara kwa mikoa ya magharibi na nchi za maziwa makuu kwa kuhakikisha wanasimamia kwa tija kubwa vyombo vya usafirishaji majini kwenye ziwa Tanganyika.


Hayo yalisemwa  leo na Mkurugenzi Mkuu wa TASAC, Kaimu Abdul Mkeyenge wakati akizungumza na waandishi wa habari mjini Kigoma ambapo alisema kuwa mkoa Kigoma unayo tija kubwa ya kufanya biashara na shughuli za kiuchumi na nchi za maziwa makuu ambapo ziwa Tanganyika kwa sasa ndiyo njia kuu inayohudumia usafirishaji wa bidhaa na abiria kutoka na kuingia kwenye nchi hizo.


Kutokana na hali hiyo alisema kuwa TASAC imejipanga kuongeza maradufu watendaji wake mkoani Kigoma kuhakikisha shughuli zinazohusiana na taasisi hiyo na wasafirishaji majini zinashughulikuwa kwa urahisi kwa kipindi kifupi ili kusiwe na mkwamo kwenye utekelezaji wa shughuli za biashara na uchumi.


Mkeyenge alisema kuwa wamejipanga pia kuhakikisha taratibu za kisheria za kimataifa na zile za Tanzania za  usalama wa usafirishaji majini ziwa Tanganyika kwa vyombo vinavyokwenda nchi za Burundi,Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo na Zambia zinatekelezwa kikamilifu.


“Zipo changamoto za usimamizi wa taratibu na sheria kwa wenzenu wa nchi zinazozunguka ziwa Tanganyika ikiwemo meli na boti za abiria kuchanganya bidhaa hizo wakati sheria za Tanzania zinakataza bidhaa hizo mbili kuchanganywa hivyo vipo vikao na majadilinao yanaendelea ili kuliweka jambo hilo sawa,”Alisema Mkeyenge.


Akizungumzia mpango wa serikali wa kuufanya mkoa Kigoma kuwa kitovu cha biashara Mwenyekiti wa chama cha wasafirishaji wa maboti mkoa Kigoma, Ibrahim Sendwe alisema kuwa jambo hilo ni muhimu na litachochea biashara na uchumi wa mkoa Kigoma.


Sendwe alisema kuwa wao kama wasafirishaji wa mizigo na abiria wapo tayari kushiriki kwenye mipango hiyo lakini wanapaswa kupewa uelewa wa fursa ambazo kwao wanaweza kuzitumia kuleta tija kwenye mpango huo.


Mwenyekiti huyo alisema kuwa wamejipanga kuhakikisha wanasimamia taratibu za usalama wa usafirishaji abiria ikiwemo taratibu na sheria za usafirishaji wa abiria na mizigo ili shughuli zao zisipingane na maelekezo ya serikali.


Kwa upande wake Mmiliki wa boti zinazofanya shughuli zake ziwa Tanganyika, Almas Juma amemshukuru Raisi Samia kwa maboresho makubwa yanayofanywa kwenye bandari ya Kibirizi na miradi mikubwa kwa mkoa Kigoma kwenye sekta ya biashara na uchumi kwani imechochea shughuli za biashara na uchumi mkoani humo.


Hata hivyo Juma ameomba serikali ya Rais Samia kuondoa tozo ya Viza inayotozwa kwa wasafiri wanaoingia mkoani Kigoma kutoka Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo na ada ya dola 20 kwa wafanyabiashara wadogo ambao hawana nyaraka za kufanya biashara.

KAMPUNI YA AGRICOM YATUMIA MASHINDANO YA SHIMIWI KUTOA ELIMU

October 16, 2022
i




Na Oscar Asssenga, Tanga, 

AFISA Masoko kutoka Kampuni ya Agricom inayojihusisha na uuzaji na usambazaji wa zana za kilimo Baraka Konkara amesema wametumia mashindano ya Shirikisho la michezo ya idara,   wizara na taasisi za serikali (SHIMIWI)  kutoa elimu na kuwahamasisha watumishi wa umma namna ya kuweza kujiajiri katika kilimo ili hata wanapostaafu wawe na shughuli ya kuwakwamua kiuchumi. 

Baraka aliyasema hayo wakati wa ufungaji wa mashindano  ya 36 ya Shimiwi yaliyofanyika Kitaifa Mkoani Tanga. 

Alisema kuwa serikali imekuwa ikiweka jitihada kubwa katika suala zima la kilimo hivyo basi na wao wamekuwa sehemu ya kuweza kuunga mkono ile agenda ya wizara ya kilimo. 

Alisema kilichowavutia zaidi kuweza kudhamini mashindano haya kwanza kabisa ilikuwa inakosa ufadhili hivyo basi tumekuwa kwa kipindi cha miaka miwili ikiwemo mwaka jana na mwaka huu wamedhamini mashindano hayo lakini wanaona katika udhamini wa mashindano hayo wanaweza kuwasaidia wenzao wa serikali ambao ni wadau muhimu sana ili waweze kufanikisha michezo katika kuboresha afya zao na kujenga mahusiano mazuri kazini.

Alisema kwamba  licha ya kuwajua watumishi hao wa Umma lakini pia wamekuwa wakijihusisha na shughuli nyingine za kujiingizia kipato ikiwemo za kilimo jambo ambalo limewasukuma kudhamini mashindo hayo kwa lengo la kuwaweka karibu na kuwapa mbinu za kilimo chenye tija kinatachowakwamua na umasikini. 

Konkara amesema kuwa watahakikisha wanaendelea kuangalia ni namna gani wanavyokuwa na ukaribu na watumishi hao wa umma katika suala zima la mikopo ambayo inakuwa na riba nafuu kwa kushirikiana na mabenki mbalimbali. 

"Lengo letu ni kuweza kuwafikia popote pale walipo ili pia wanapostaafu wawe na shughuli nyingine za kufanya baada ya kustaafu wasije wakawa wanaingia mtaani wakawa wageni zaidi kwahiyo tunawahudumia zana hizi za kisasa za kilimo na kuwapatia unafuu mkubwa ambao maeneo mengine wanashindwa kupata, "alisisitiza Konkara. 

Awali akizungumza wakati akifungua Mashindano hayo ya Shimiwi,  Mkuu wa Mkoa Tanga Omari Mgumba aliipongeza kampuni hiyo ya Agricom kwa kuwa wadhamini wakuu wa mashindano hayo jambo ambalo linapaswa kuigwa na makampuni mengime huku akiwataka watumishi hao wa  umma kuendelea kutenga muda wa kufanya mazoezi katika sehemu zao za kazi. 

Mkuu huyo wa Mkoa aliwataka watakaporudi kwenye sehemu zao za kazi kuhakikdha wanaendelee kufanya mazoezi kama sehemu ya maisha .

Hata hivyo Mkuu huyo wa Mkoa aliwataka pia waende kujiandaa kwa ajili ya mashindano ya mwaka ujao huku akiwataka wakawe mabalozi wazuri kuwahimiza wenzao ili  mwaka ujao wanatekeleza maelekezo ya Makamu wa Rais ya kuhakikisha wanachama wote wanaoshiriki kwenye michezo hii wanatimiza azma ya serikali ya kuwashirikisha watumishi wote kufanya mazoezi na kushiriki kwenye mashindano.

Mwisho.

ELIMU YANG'ARA MCHEZO WA RIADHA KATIKA MICHUANO YA SHIMIWI

October 11, 2022

 


Na Oscar Assenga,TANGA


TIMU ya Mchezo wa Riadhaa ya Wizara ya Elimu,Sayansi na Teknolojia imeng’ara katika Mashindano ya Shimiwi yanayoendelea Jijini Tanga.

Wachezaji wa timu ya Elimu ilianza kwa kasi katika mchezo huo wa Riadhaa ambapo wakimbiaji wake walikuwa hari kubwa ya kukimbiza upepo ili kuweza kupata ushindi katika mashindano hayo.

Katika mchezo huo timu ya wanaume imefanya vizuri kwa upande wa mita 100 kupokezana vijiti huku kwenye zile za mita 200 wakiibuka washindi wa pili.

Kwa upande wa michezo mengine timu za Wizara hiyo walipambana mpaka kufikia hatua ya nane bora kwa mchezo wa kuvuta kamba ,mpira wa miguu,mpira wa pete .

Akizungumza kuhusu mashindano hayo Makamu Mwenyekiti ywa timu ya Elimu Sports Deogratius Wenga alisema kwamba mashindano hayo yamekuwa na ushindani mkubwa.

 

MFUKO WA NSSF TANGA WAHITIMISHA WIKI YA HUDUMA KWA WATEJA KWA KUTOA VIKOMBE NA VYETI

October 09, 2022

 

Meneja wa NSSF Mkoa wa Tanga Audrey Claudius  kushoto akimkabidhi  cheti na kikombe  Mkuu wa Idara ya Fedha ya Tanga Cement Isaack Mponela kwa kuibuka washindi wa jumla katika mwajiri mkubwa anayechangia mchango  ndani ya mfuko huo 




Na Oscar Assenga,TANGA.

MFUKO wa Taifa wa Hifadhi za Jamii (NSSF)mkoa wa Tanga mwishoni mwa wiki wamehitimisha wiki ya huduma kwa wateja huku wakitambua umuhimu wa waajiri hususani wakubwa kwa kuwapatia vyeti na tu vikombe ikiwa ni kuthamini mchango wao kwa kuchangia wazuri katikia mfuko huo

Akizungumza mara baada ya zoezi hilo Meneja wa NSSF Mkoa wa Tanga Audrey Claudius alisema kwamba katika wiki hiyo ambapo alisema waliwapa vyeti ambavyo zinao nyesha mchango wao kama waajiri wakubwa na waliwaweka kwenye makundi mbalimbali kwenye waajiri wakubwa na
wanaolipa michango kwa wakati na wenye taarifa nzuri nzuri.

Aidha alisema kwamba waajiri hao wamekuwa na mchango mkubwa ndani ya mfuko huo huku akihaidi kushirikiana nao kuhakikisha wanaendelea kupata mafanikio.

"Niwapongeze waajiri tuendelee kufanya vizuri kwa vipindi vyenginevyo vyote kwani kwa kufanya vizuri kunachangia nasi kuweza kutoa huduma nzuri na kwa wakati hivyo ni muhimu kushirikiana" Alisema Meneja huyo

Aidha alisema katika kipindi cha wiki ya huduma kwa mteja kwa mkoa huo wanachama walio wafungulia madai zaidi ya 15 na yote yamefanikiwa kulipwa na hiyo inatokana na waajiri kuwajibika ipasavyo kwa kupeleka michango yao kwa wakati na taarifa za wanachama kiwa sahihi.

"Niwasihi wafanyakazi wenzangu tuendelee niwashii wafanyakazi wenzangu tuendelee kushirikiana kuweza kufanya vizuri zaidi lakini Tanga Cement ni mwajiri mkubwa anayechangia mchango mkubwa kwa Mkoa wa Tanga na ndio mshindi kwa ujumla”Alisema

Naye kwa upande wake Mkuu wa Idara ya Fedha ya Tanga Cement Isaack Mponela kwa niaba ya waajiri wote aliwashukuru ofisi ya Mfuko huo mkoani Tanga kwa kushirikiana pamoja nao katika wiki ya huduma kwa mteja..

Mponela alisema katika wiki ya huduma kwa mteja na ile huduma nzuri kwa wateja wao kama waajiri na nmwanachama wa mfuko Mfuko huo wanaipata siku zote.

Alisema kwamba mfuko huo unafanya vizuri kuhakikisha mahusiano kati yao na wanachama wakiwemo waajiri yanakuwa mzuri sana.

Alisema wao kama Kampuni wanatoa kipaumbele pamoja na kufuatilia na kushika sheria za nchi ikiwemo ya Mfuko huo hivyo ni jukumu lao kuhakikisha michango inafika NSSF na waajiri wote wanajiunga na mfuko huo kwani wao wanatoa kipaumbele kuhakikisha taratibu za nchi
zinafuatwa.

Naye kwa upande wake Mwanachama wa Mfuko huo Mkoani Tanga,Ally Juma alisema kwamba wanashukuru walifungua madai na amelipwa kwa wakati huku akiwataka watanzania kuendelea kujiunga na Mfuko huo iki kuweza kuendelea kunufaika na huduma mbalimbali.