Mwalimu Mkuu wa Shule ya Sekondari ya Muheza Muslimu
KAMISHNA wa Tume ya Utumishi wa Umma nchini Balozi Adadi Rajab akigawa vyeti kwa wahitimu wa kidato cha nne wakati wa maafali ya shule ya Sekondari Muheza Muslim
KAMISHNA wa Tume ya Utumishi wa Umma nchini Balozi Adadi Rajab akigawa vyeti kwa wahitimu wa kidato cha nne wakati wa maafali ya shule ya Sekondari Muheza Muslim
KAMISHNA wa Tume ya Utumishi wa Umma nchini Balozi Adadi Rajab katikati akiwa na wadau wa maendeleo na wajumbe wa bodi ya shule ya Sekondari Muheza Muslim wakati wa maafali hayo
Na Oscar Assenga,MUHEZA
KAMISHNA wa Tume ya Utumishi wa Umma nchini Balozi Adadi Rajabu amewataka wanafunzi katika shule ya Sekondari Muheza Muslim kuhakikisha wanasoma kwa bidii ili wataalamu mbalimbali waweze kupatikana kupitia huko.
Balozi Adadi aliysema hayo wakati wa mahafali ya shule hiyo yaliyofanyika mjini Muheza ambapo alisema lazima wanapokuwa shuleni waweze kujiandaa na kuzingatia nidhamu ,malengo na kusoma vizuri ili baadae waje kufanikiwa kupitia elimu.
Alisema kwamba mitihani inahitaji maandalizi mazuri ili waweze kufanya vema hivyo hawana budi kuhakikisha wanajiandaa ili kuweza kufanya vizuri katika mitihani yao.
Katika Mahafali hayo Balozi Adadi aliendesha Harambee kwa ajili ya ujenzi wa vyumba vya maabara katika shule hiyo ambapo huku akihaidi kuendelea kushirikiana nao katika kuhakikisha wanapata mafanikio.
Kamishna huyo aliuomba uingozi wa shule kwamba hiyo maabara utakapo kamilika ipewe jina la Bahoza Laboratory ili kuwaenzi kwa juhudi kubwa ambazo wamezifanya kufanikisha maabara hiyo.
Hata hiyo Balozi Adadi alisema Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais Samia Suluhu imefanya mambo makubwa na kuleta maendeleo huku akieleza fedha ambazo zinakuja zinatokana na kurudisha mahusiano ya na mataifa mengine ambayo yalikatika na ameyarudisha kwa kasi kubwa.
Alisema kutokana na kurejesha mahusiano hayo yamewasaidia kupata fedha nyingi za kujenga shule, maabara,barabara na kila Jimbo kuhakikisha maendeleo yanapatikana ule ufufuaji wa mahusiano na mataifa mengine.
Katika hatua nyengine Balozi Adadi aliitaka Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa nchini kuhakikisha wana buni mbinu zinazoweza kudhibiti vitendo vya rushwa ya ngono nchini.
Balozi Adadi alisema kwamba vitendo vya rushwa ya ngono vimekuwepo na Takukuru wamepewa jukumu la kudhibiti vitendo hivyo ni wakati sahihi kuhakikisha wanakuja na mwarobaini wake.
Alisema kwamba wao wanapaswa kuona namna nzuri ya kubuni mbinu ambazo zinaweza kupelekea
kudhibiti badala ya kusubiri matukio yanatokea ndio waweze kuanza kupambana nayo.
" Haya mambo yapo kwa sababu kwenye vyuo hivyo ni jinsi ya vyombo vilivyo kabidhiwa kufanya kazi hiyo wanafanya nini ili kuweza kuondokana na tatizo hilo"Alisema Balozi Adadi.
Aidha alisema kwamba wanataka wanaofanya vitendo hivyo wakamatwe ili iweze kuwa fundisho kwa wengine wenye tabia za namna hiyo kuweza kubadilika hivyo suala hili lina umuhimu wake hasa chombo ambacho kimepewa mamlaka ya kusimamia.
EmoticonEmoticon