UKOSEFU WA MALEZI BORA UMECHANGIA MATUKIO YA UFISADI NCHINI

April 05, 2018


Mjumbe wa Halmashauri kuu ya Baraza la Waislamu BAKWATA Mkoa wa Tanga Shk Hassan Kabeke wakati wa uzinduzi wakampeni ya baba bora iliyofadhiliwa na ubalozi wa Swedeni kwa kushirikiana na madhehebu ya dini nchini kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Tanga Martine Shigella
Askofu wa kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania KKKT dayosisi ya Kaskazini Mashariki Stephen Munga akizungumza kwenye halfa hiyo kushoto ni Balozi wa Swedeni nchini Katarina Rangnitt na Mkuu wa Mkoa wa Tanga Martine Shigella.


Mkuu wa Mkoa wa Tanga Martine Shigella akizungumza katika uzinduzi huo kulia ni Mjumbe wa Halmashauri kuu ya Baraza la Waislamu BAKWATA Mkoa wa Tanga Shk Hassan Kabeke
Balozi wa Swedeni nchini Katarina Rangnitt katikati akimsikiliza kwa umakini Askofu wa kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania KKKT dayosisi ya Kaskazini Mashariki Stephen Munga wakati wa uzinduzi huo kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Tanga,Martine Shigella

Askofu wa kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania KKKT dayosisi ya Kaskazini Mashariki Stephen Munga kulia akifurahia jambo na Mkuu wa Mkoa wa Tanga Martine Shigella wakati wa uzinduzi huo

Sehemu ya wadau walioshiriki uzinduzi huo uliofanyika kwenye ukumbi wa YDCP Jijini Tanga
Sehemu ya wanahabari walioshiriki kwenye uzinduzi huo




IMEELEZWA kuwa kuongezeka kwa vitendo vya ukatili pamoja na matukio yauhalifu na ufisadi nchini inatokana na jamii kusahau swala la malezibora hususani katika ngazi ya familia.

Hayo yameelezwa hapo jana na Mjumbe wa Halmashauri kuu ya Baraza la Waislamu BAKWATA Mkoa wa Tanga Shk Hassan Kabeke wakati wa uzinduzi wakampeni ya baba bora iliyofadhiliwa na ubalozi wa Swedeni kwa kushirikiana na madhehebu ya dini nchini.

Alisema kuwa shida zote za kimaadili zinazoendelea kulikumba taifa kwa sasa zinatokana na jamii kusahau jukumu lake la malezi na kuachiwa mtu mmoja pekee ambaye ni mwanamke.

“Jamii bado inaendelea kuteseka katika ufisadi na maovu mengine sasa imefika wakati wa baba nae kuhakikisha nachukuwa nafasi yake katika malezi ili kujenga watoto wenye tabia njema”alisema Shk Kabeke.

Kwa upande wake Balozi wa Swedeni nchini Katarina Rangnitt alisema kuwa kampeni hiyo imelenga katika kuhakikisha wanaleta mabadiliko katika jamii kuhusu malezi kupitia viongozi wa dini.

“Kupitia maonyesho ya picha naamini watu wataweza kujadili zaidi maanaya kuwa baba bora kwa kushiriki kikamilifu katika malezi ya watoto wao kwani inafaida kubwa “alisema Balozi huyo.

Alisema kuwa viongozi wa dini wanaushawishi mkubwa katika maswala hayo na wanaweza kuchukuwa jukumu la pekee katika kufikia na kuendeleza haki za kijinsia kwa wababa katika malezi .
Hata hivyo Askofu wa kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania KKKT dayosisi ya Kaskazini Mashariki Stephen Munga alisema kuwa wababa wa Tanzania wanafikiri kuwa ubaba ni kutoa mahitaji muhimu pekee wakati kwa uhalisia ni zaidi ya hivyo.

Alisema kuwa kuwa baba bora ni kuhakikisha unakuwa tayari kujitolea nakuwekeza muda wako katika malezi ya watoto na sio kuhusu unachofanya pekee.

Kampeni ya baba imezinduliwa rasmi katika mkoa wa Tanga ambapo itajumuisha maonyesho ya picha ya wababa wa kitanzania na kiswidiinatoa fursa nyingine kwa baba kuonyesha nafasi yao katika malezi ya watoto.

Share this

Related Posts

Previous
Next Post »