NAIBU
Waziri wa Kilimo, Dk Mary Mwanjelwa akiongea machache na Mkuu wa Mkoa
wa Iringa, Mhe. Amina Masenza alipofika kwa utambulisho na kuanza ziara
katika Mkoa huo Februari 23 2018. Pamoja naye (kushoto) Afisa Mtendaji
Mkuu wa SAGCOT, Geoffrey Kirenga viongozi wa wasaidizi wake mkoani humo.
(Imeandaliwa na Robert Okanda blogs)
|
NAIBU
Waziri wa Kilimo, Dk Mary Mwanjelwa akiagana na Mkuu wa Mkoa, Mhe.
Amina Masenza baada ya kufanya naye mazungumzo ofisini wakati wa kuanza
kwa ziara yake mkoani humo. Kushoto ni Afisa Mtendaji Mkuu wa SAGCOT,
Geoffrey.
|
NAIBU
Waziri wa Kilimo, Dk Mary Mwanjelwa akiwabadilishana mawazo na wakina
mama wanajitegemea 'Single mothers' baada ya kukagua sehemu ya shamba
lenye hekari 651 lililonunuliwa na Taasisi ya Ilula Programu 2013 mkoani
Iringa kwa ajili ya kilimo cha biashara maalum kwa ajili yao, watoto
yatima na wanafunzi wenye nia ya kukuza uelewa wa kilimo kutoka katika
Wilaya ya Iringa hasa wa shule za primary na awali.
|