TANZANIA YADHAMIRIA KUONDOA TATIZO LA SARATANI YA MLANGO WA KIZAZI KWA WANAWAKE NCHINI

February 27, 2018

????????????????????????????????????
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu (MB) akisisitiza jambo mbele ya Wadau wa Afya na waandishi wa habari wakati akifungua mkutano wa wadau wa chanjo ya kukinga saratani ya mlango wa kizazi jijini Dar es salaam.
????????????????????????????????????
Mganga Mkuu wa Serikali Prof. Muhammad Bakari Kambi akimkaribisha mgeni rasmi Mh. Ummy Mwalimu (hayupo kwenye picha) wakati akifungua mkutano wa wadau wa chanjo ya kukinga saratani ya mlango wa kizazi
????????????????????????????????????
Meneja mpango wa Taifa wa Chanjo Wizara ya Afya Dkt. Dafrossa Lyimo akiwasilisha taarifa mbele ya Mgeni rasmi (hayupo kwenye picha) wakati wa mkutano wa wadau wa chanjo ya kukinga saratani ya mlango wa kizazi
????????????????????????????????????
Mwakilishi wa WHO Dkt. Ritha Njau akiwasilisha salamu za WHO wakati wa mkutano wa wadau wa chanjo ya kukinga saratani ya mlango wa kizazi
????????????????????????????????????
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu (MB) akiteta jambo na Mganga Mkuu wa Serikali Prof Bakari Kambi
????????????????????????????????????
Wadau wa Afya na Waandishi wa Habari wakifuatilia taarifa kutoka kwa Mgeni rasmi (hayupo kwenye picha) wakati wa mkutano wa wadau wa chanjo ya kukinga saratani ya mlango wa kizazi
????????????????????????????????????
Picha ya pamoja ikiongozwa na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu (MB)  wakati akifungua mkutano wa wadau wa chanjo ya kukinga saratani ya mlango wa kizazi jijini Dar es salaam.
…………………..

SERIKALI kupitia Wizara ya Afya, Maendeleo ya jamii, Jinsia, Wazee na Watoto imedhamiria kupambana na Saratani ya mlango wa kizazi nchini kwa kuwapa kinga wasichana kuanzia umri wa miaka 9 mpaka 14 huku lengo likiwa ni kuondoa tatizo hilo nchini.
Hayo yamebainishwa na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu (MB) mapema leo wakati akifungua mkutano wa wadau wa chanjo ya kukinga saratani ya mlango wa kizazi jijini Dar es salaam.
“Katika kukabiliana na ugonjwa wa Saratani na kuimarisha afya ya wanawake Tanzania na kupunguza vifo vitokanavyo na Saratani , Wizara ya Afya itaanza kutoa chanjo ya kuwakinga wasichana dhidi ya Saratani ya mlango wa kizazi”. Alisema Mhe. Ummy Mwalimu.
Waziri Ummy aliendelea kusema kuwa kwa mujibu wa takwimu za taasisi ya Ocean Road Saratani ya Mlango wa kizazi zinazoongoza nchini kwa Asilimia 36 huku ikifuatia na saratani ya matiti, huku jumla ya wagonjwa wa Saratani nchini katika kila wagonjwa 100, wagonjwa 46 ni wa Saratani ya mlango wa kizazi na Saratani ya Matiti.
Aidhe, Serikali imepanga kuanza na wasichana wenye umri wa miaka 14 kama umri wa chini, huku ikitegemea kuchanja zaidi ya wasichana 610,000 katika jitihada za kutokomeza kabisa tatizo hili la Saratani ya mlango wa kizazi nchini,
Mhe Ummy alisisitiza kuwa Chanjo hii itatolewa katika vituo vyote vya Afya nchini  vya Serikali, vya watu binafsi na vikundi mkoba bure, na kuwahimiza wazazi na walezi kuhakikisha mabinti zao wanapata chanjo hii ili kujikinga na ugonjwa huo.
Nae Meneja wa Mpango wa Taifa wa Chanjo Wizara ya Afya, Maendeleo ya jamii, Jinsia, Wazee na Watoto  Dkt. Dafrossa Lyimo aliendelea kuwatoa hofu wananchi na kusisitiza juu ya umuhimu wa kinga kuliko tiba na kusema kuwa chanjo hiyo ni salama na imethibitishwa na shirika la Afya duniani na mamlaka ya chakula na viodozi nchini (TFDA).

Share this

Related Posts

Previous
Next Post »