Chama cha wauza nazi katika soko la Mgandini Jijini
Tanga wameeleza sababu za nazi zinazotoka Mombasa nchini Kenya kukukabilia
kuliko za Tanga kutokana na ubora zilizokuwa nazo na kubwa.
Hayo yalibainishwa na Katibu wa chama cha Wauza Nazi
katika soko hilo (Coconut Group) Kassim Mohamed katika mahojiano na Blog hii
ambapo alisema sababu nyengine ni wakulima nchini humo kuiweka nazi hiyo muda
mrefu shambani kwa kufuata utaratibu kuliko ilivyo kwa wengine.
Alisema hali hiyo imezifanya nazi zinazotoka huku
kuonekana kupendwa na wafanyabiashara wengi ambao wamekuwa wakifika kwa ajili
ya ununuaji wa zao hilo kwenye soko hilo kuliko ilivyo za mkoani Tanga hali inayotajwa
kuchangiwa na wakulima.
“Kwa mfano utakuwa mkulima wa nazi mkoani Tanga anavuna
nazi mapema shambani kutokana na shida alizokuwa nazo lakini wa Mombasa nchinio
Kenya wamekuwa wakiziweka muda mrefu na hivyo zinavunwa zinakuwa kubwa na wenye
ubora”Alisema
“Lakini pia wanasema uharakishaji wa uvunaji wakulima
hao zao hilo wamepeleka kupata nazi ndogo ambazo sokoni zimekuwa na changamoto
kubwa kuliko ambazo zinatoka nchi jirani ya Kenya kwani hizi za Tanga unaweza
kuwa nazo unauza reja reja “Alisema.
Alisema sababu inayopelekea wakulima hao kupata nazi
ndogo inatokana na kushindwa kuendeleza zao hilo kwa kuipanda mingine kwani
iliyopo hivi sasa ni ya zamani ambayo wamerithi katika maeneo yao.
“Lazima watambue kuwa hata kama utakuwa umerithi mnazi
unapaswa kutambua umuhimu wa kupanda mingine kwani inapokaa muda mrefu
inapelekea kuzalisha nazi ndogo.
Naye mchuuzi kwenye soko hilo,Akida Juma aliwataka
wakulima wa zao hilo mkoani hapa kubadilika kwa kulima kisasa ili kuondokana na
kutegemea minazi ya zamani ili waweze kuvuna jambo ambalo linaweza kuwapeleka
kukosa soko kabisa kutokana na ushindani uliopo.
“Ndugu zangu tunajua minazi mingi watu wamerithi kutoka
na kupandwa miaka ya nyuma hivyo hakikisheni mnaipanda mingine kwa kufuata
taratibu mzuri na baadae mnaweza kupata mafanikio kuliko sasa “Alisema.