Ubalozi
wa Tanzania wa Riyadh nchini Saudi Arabia hivi karibuni ulishiriki
katika maonyesho ya Travel and Tourism Pioneers Forum 2018 mjini Riyadh.
Maonyesho haya ya kimataifa yaaliandaliwa na Al Awasat Expo chini ya
udhamini wa MwanaMfalme HRH Prince Dr. Saif Al Islam. Maonyesho haya
yalizishirikisha taasisi mbalimbali zinazohusika na utalii ndani na nje
ya Saudi Arabia.
Ubalozi
wa Tanzania ulishiriki na kufanikiwa kutangaza vivutio mbalimbali vya
utalii vilivyopo nchini ikiwa ni pamoja na kukutana na mawakala wa
utalii, tour operators, travel agencies na makampuni ya kutangaza
utalii.
Baadhi
ya wananchi waliotembelea banda la Tanzania katika maonyesho ya Travel
and Tourism Pioneers Forum 2018 mjini Riyadh nchini Saudi Arabia.
Balozi wa Tanzania nchini Saudi Arabia Mhe. Hemedi Iddi Mgaza(kushoto) akizungumza na Mwanamfalme HRH Prince Dr. Saif Al Islam bin Saud bin Abdel Aziz Al Saud alipotembelea banda la Tanzania.
Balozi
wa Tanzania nchini Saudi Arabia Mhe. Hemedi Iddi Mgaza(katikati) akiwa
kwenye picha ya pamoja na wahudumu wa banda la Tanzania wakati wa
maonyesho ya Travel and Tourism Pioneers Forum 2018.
Wananchi
wakiwa kwenye banda la Tanzania walivutiwa na taarifa walizopata na pia
kuchukua vipeperushi vyenye taarifa kuhusu Tanzania.
Wakinamama
walikuwa ni miongoni mwa watu waliotembelea banda la Tanzania kwenye
maonyesho ya Travel and Tourism Pioneers Forum 2018 mjini Riyadh nchini
Saudi Arabia.
Balozi
wa Tanzania nchini Saudi Arabia Mhe. Hemedi Iddi Mgaza(wa pili kushoto)
akifanya mazungumzo na wananchi waliotembelea banda la Tanzania ili
kupata taarifa za kina kuhusu masuala mbalimbali Tanzania kwenye maonyesho ya Travel and Tourism Pioneers Forum 2018 mjini Riyadh nchini Saudi Arabia.