TAARIFA KUTOKA NDANI YA SHIRIKISHO LA SOKA TFF

February 23, 2018
MZUNGUKO WA NNE KOMBE LA SHIRIKISHO LA AZAM KUENDELEA WIKIENDI HII
Hatua ya mzunguko wa Nne(4) wa mashindano ya Kombe la Shirikisho la Azam inaendelea Jumamosi Februari 24, 2018 kwa michezo miwili.
Singida United watakuwa Uwanja wa Namfua Mjini Singida kucheza na Polisi Tanzania saa 10 jioni na mchezo mwingine utakaohitimisha siku hiyo utakuwa kati ya KMC watakaokuwa nyumbani Azam Complex,Chamazi kuwakaribisha Azam FC saa 1 usiku.
Mzunguko huo wa Nne(4) utaendelea tena Jumapili Februari 25, 2018 kwa Buseresere kuwaalika Mtibwa Sugar kwenye Uwanja wa Nyamagana Mwanza mchezo utakaochezwa saa 8 mchana wakati Majimaji FC ya Ruvuma watakuwa nyumbani kwenye uwanja wa Majimaji kuwakaribisha Young Africans ya Dar es Salaam mchezo ukichezwa saa 10 jioni nao Ndanda FC watakuwa ugenini kucheza na JKT Tanzania Azam Complex Chamazi saa 1 usiku.
Mzunguko huwa wa 4 utakamilika Jumatatu Februari 26, 2018 Kiluvya United dhidi ya Tanzania Prisons saa 8 mchana Uwanja wa Mabatini na Stand United watawaalika Dodoma FC saa 10 jioni uwanja wa Kambarage.
LIGI KUU YA WANAWAKE YA SERENGETI PREMIUM LITE KUZINDULIWA RASMI NA WAZIRI MWAKYEMBE JUMAPILI
Ligi Kuu ya Wanawake ya Serengeti Premium Lite hatua ya Nane bora inataraji kuzinduliwa rasmi mkoani Kigoma Jumapili Februari 25,2018 kwenye Uwanja wa Lake Tanganyika.
Mchezo utakaotumiwa kuzindua ligi hiyo utazikutanisha timu za Kigoma Sisterz ya Kigoma dhidi ya Simba ya Dar es Salaam.
Aidha uzinduzi utaenda sanjari na mpango maalumu wa FIFA wa kuhamasisha soka la Wanawake uliopewa jina la Live Your Goal ambapo mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Dr.Harrison Mwakyembe.
Mbali na mechi ya uzinduzi mechi nyingine za ligi hiyo ya Wanawake ya Serengeti Premium Lite zinatarajia kuchezwa kesho kwenye viwanja tofauti.
Uwanja wa Samora Panama FC watacheza dhidi ya Evergreen Queens ya Dar es Salaam saa 10 jioni,huko Mbweni JKT Queens watacheza dhidi ya Alliance saa 10 jioni,mabingwa watetezi Mlandizi Queens wanasafiri mpaka Jamhuri Dodoma kucheza na Baobab Queens.
Wakati huohuo Kozi ya makocha wa kozi ya grassroots kwa watoto wenye umri wa miaka 6-12 Wasichana na Wavulana imeanza Jumatano kwenye Uwanja wa Lake Tanganyika,Ujiji,Kigoma.
MCHEZO WA LIPULI NA NDANDA WASOGEZWA
Bodi ya Ligi (TPLB) imefanya mabadiliko ya mchezo namba 153 kati ya Lipuli na Ndanda uliokuwa uchezwe Ijumaa Machi 2,2018 kwenye Uwanja wa Samora,Iringa.
Mchezo huo sasa umesogezwa mpaka Jumapili Machi 4,2018 na utachezwa kwenye Uwanja ule ule wa Samora.
Sababu za kusogezwa mbele kwa mchezo huo ni kuipa nafasi Ndanda FC kusafiri kutoka Mtwara baada ya mchezo wao na Yanga ambao sasa umepangwa kuchezwa Jumatano Februari 28 ,2018 kwenye Uwanja wa Nangwana Sijaona ,Mtwara.
IMETOLEWA NA SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA TFF

Share this

Related Posts

Previous
Next Post »