MASOKO
yasiyokuwa rasmi yanayolizunguka soko la Mgandani Jijini Tanga yanadaiwa
kusababisha upatikanaji wa mapato kuwa madogo.
Hatua hiyo
imepelekea uongozi wa soko hilo kuiomba Halmashauri ya Jiji hilo kuingilia kati
kutumia nguvu za ziada ili kuweza kuwaondoa wafanyabiashara hao ambao wanauza
bidhaa zao kwenye mazingira hatarishi.
Akizungumza na Tovuti hii mwishoni mwa wiki Katibu wa Soko hilo, Ridhiwani Mwinyiheri
alisema licha ya hivyo lakini pia wafanyabiashara hao wamepelekea biashara kwa
walipoo kwenye vizimba ndani ya soko hilo kukosa wateja.
“Jambo hilo
tukilifumbia macho linaweza kukwamisha mipango yetu hivyo tunaiomba Halmashauri
ya Jiji la Tanga kuangalia namna mzuri ya kuhakikisha wafanyabiashara hao
wanaondoka kwenye maeneo hatarishi ya barabarani “Alisema
“Lakini pia
kuwepo kwao nje ya soko kumepelekea hata biashara kuwa ngumu kwani baadhi ya wateja
wanaofika hapa huishia nje hivyo kwa wale wanaouzia ndani wanakuwa wakikosa
wateja”Alisema.
Hata hivyo
aliopngeza hivi sasa soko hilo limekuwa na msongamano mkubwa wa wafanyabiashara
ambao wengine wanalazimika kupanga bidhaa zao chini kutokana na ongezeko ambalo
limesababisha kwa asilimia kubwa na vijana waliomaliza darasa la saba na kidato
cha nne.
“Licha ya hivyo
lakini pia hali hiyo imesababishwa na wafanyabiashara wenyewe kwa sababu
anamuingiza msaidizi wake sokoni hapo baadae anamtafutia sehemu ya kupanga
bidhaa zake”Alisema.