MZUNGUKO
WA NNE WA KOMBE LA SHIRIKISHO LA AZAM KUANZA KESHO
Hatua ya mzunguko wa Nne(4) wa mashindano ya Kombe la
Shirikisho la Azam inatarajia kuanza kesho Jumatano Februari 21, 2018.
Kwenye Uwanja wa Sabasaba Njombe kutakuwa na mchezo mmoja
utakaowakutanisha mwenyeji Njombe Mji atakayecheza dhidi ya Mbao FC kutoka Mwanza saa 10 jioni.
Mechi nyingine za Kombe la Shirikisho la Azam zitaendelea
Jumamosi Februari 24,wakati Singida United watakapowakaribisha Polisi Tanzania
kwenye Uwanja wa Namfua saa 10 jioni na KMC watawaalika Azam FC saa 1 usiku
Azam Complex.
Jumapili Februari 25, 2018 Buseresere watakuwa uwanja wa
Nyamagana Mwanza saa 8 mchana kucheza dhidi ya Mtibwa Sugar ya Morogoro,Majimaji
FC ya Ruvuma watakuwa nyumbani kwenye uwanja wa Majimaji kuwakaribisha Young
Africans ya Dar es Salaam saa 10 jioni wakati Ndanda FC watakuwa ugenini
kucheza na JKT Tanzania saa 1 usiku Azam Complex Chamazi.
Jumatatu Februari 26, 2018 kutachezwa mechi mbili Kiluvya
United dhidi ya Tanzania Prisons saa 8 mchana Uwanja wa Mabatini na Stand
United watawaalika Dodoma FC saa 10 jioni uwanja wa Kambarage.
NDANDA
VS YANGA SASA KUCHEZWA MWISHO WA MWEZI
Mchezo namba 152 wa mzunguko wa 19 wa Ligi Kuu ya Vodacom
Tanzania Bara kati ya Ndanda FC ya Mtwara na Young Africans umepangiwa tarehe
ya kuchezwa.
Bodi ya Ligi imetaja tarehe hiyo baada ya awali mchezo
tajwa kutokuwa umepangiwa tarehe kwa mujibu wa ratiba ya Ligi Kuu.
Mchezo huo sasa utachezwa Jumatano Februari 28, 2018
katika Uwanja wa Nangwanda Sijaona uliopo mkoani Mtwara.
Timu zote tayari zimejulishwa kuhusu tarehe ya kuchezwa
mchezo huo.
FIFA
WAONGEZA TIKETI ZA KOMBE LA DUNIA KWA TANZANIA
Shirikisho la Mpira wa Miguu Duniani FIFA limeongeza
tiketi kwa Tanzania kwaajili ya fainali za kombe la Dunia zitakazochezwa Russia
mwaka huu.
Kwa shabiki yeyote anayetaka kwenda kushuhudia fainali
hizo za Kombe la Dunia awasiliane na idara ya mashindano ya TFF kwa utaratibu
wa namna ya kupata tiketi hizo.
Ngwe hii ya pili ya tiketi za Kombe la Dunia imefunguliwa
Februari 15, 2018 na itafungwa Machi 12, 2018.
Ikumbukwe awali FIFA walitoa tiketi 290 kwa Tanzania ili
kushuhudia fainali hizo za Kombe la Dunia kabla ya zoezi hilo kufungwa mwezi
Januari na sasa imefunguliwa ngwe nyingine ya tiketi hizo.
IMETOLEWA
NA SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA TFF