"NAJIVUNIA KUFANYA KAZI CHINI YA RAIS MAGUFULI ANAYEFANYA MAAMUZI KWA WAKATI" MHE BITEKO

February 20, 2018

Naibu Waziri wa Madini Mhe Doto Mashaka Biteko akisisitiza jambo wakati akizungumza na viongozi na watumishi mbalimbali wa ngazi ya Wilaya ya Ileje Mkoa wa Songwe na Kyela Mkoani Mbeya katika ukumbi wa ofisi za Mgodi wa Kiwira zilizopo katika Kijiji cha Kapeta, Kata ya Ikinga Wilayani Ileje, Leo Februari 2018. Picha Zote Na Mathias Canal, WazoHuru Blog
 Naibu Waziri wa Madini Mhe Doto Mashaka Biteko akiwasili mgodini
Naibu Waziri wa Madini Mhe Doto Mashaka Biteko akikagua hali ya mitambo tangu kusimamishwa kwa uzalishaji wa mgodi wa makaa ya mawe wa Kiwira mwaka 2009 katika Kijiji cha Kapeta, Kata ya Ikinga Wilayani Ileje, Leo Februari 2018.
Naibu Waziri wa Madini Mhe Doto Mashaka Biteko akikagua hali ya magari tangu kusimamishwa kwa uzalishaji wa mgodi wa makaa ya mawe wa Kiwira mwaka 2009 Kijiji cha Kapeta, Kata ya Ikinga Wilayani Ileje, Leo Februari 2018.

Na Mathias Canal, Songwe

Naibu Waziri wa Madini Mhe Doto Mashaka Biteko amebainisha kuwa anajivunia kufanya kazi chini ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt John Pombe Magufuli Kwani amekuwa ni kiongozi anayefanya maamuzi kwa wakati pasina kuchelewa.

Mhe Biteko ameyasema hayo Leo 12 Februari 2018 wakati akizungumza na viongozi na watumishi mbalimbali wa ngazi ya Wilaya ya Ileje Mkoa wa Songwe na Kyela Mkoani Mbeya katika ukumbi wa ofisi za Mgodi wa Kiwira zilizopo katika Kijiji cha Kapeta, Kata ya Ikinga Wilayani Ileje.

Alisema kuwa Rais Magufuli ameonyesha dhamira ya dhati ya kuepuka michakato ya kuchelewesha maendelo kwa maamuzi ya busara na haraka anayoyafanya huku akieleza kufurahishwa na maamuzi ya kujengwa ukuta katika machimbo ya Tanzanite yaliyopo katika eneo la Merelani Wilaya ya Simajiro Mkoani Arusha.

Mhe Biteko akiwa ziarani Mkoani Songwe amemtaja Rais Magufuli kama kiongozi mpenda haki, na msimizi madhubuti wa rasilimali za umma hivyo maamuzi yake yamepelekea Taifa kwa sasa kufikia hatua ya kuheshimika ndani na nje ya mipaka ya Tanzania.

Hata hivyo alisema kuwa ili kuitafsiri vyema ndoto ya Rais Magufuli ya kuwanufaisha wananchi kupitia sekta ya Madini amekusudia kuhakikisha sekta hiyo inakuwa na tija kwa kukuza uchangiaji wa pato la Taifa.

Akizungumza kwa msisitizo juu ya kusudio la serikali kuhakikisha Mgodi wa Kiwira unaanza uzalishaji ili kuchochea ajira kwa wananchi aliutaka uongozi wa Wilaya ya Ileje na Kyela kuketi mezani kwa ajili ya mazungumzo ya makubaliano ya namna bora ya kumaliza sintofahamu ya namna ya ukusanyaji mapato kutokana na mgodi huo kuwa Wilaya ya Ileje lakini baadhi ya huduma zingine zikipatikana Wilaya ya Kyela zikiwemo makazi ya wafanyakazi wa mgodi.

Aidha, alisema kuwa viongozi hao pindi watakapokuwa na makubaliano mazuri wanapaswa kutumia fedha watakazokuwa wanakusanya kwa kuzielekeza katika miradi inayoonekana.

Sambamba na hayo pia Mhe Biteko alielekeza Wakurugenzi kutotoza ushuru usiokuwa na tija ambao utawafanya wawekezaji na wachimbaji kushindwa kumudu jambo litakalopelekea kudumaa kwa faida wanayopata na hatimaye kushindwa kuwekeza.

Share this

Related Posts

Previous
Next Post »