Katibu wa chama cha mapinduzi Mkoa wa Iringa Christopher Magala akizungumzia utekelezaji wa ila ya chama cha mapinduzi Mkoa wa Iringa
Na hii ni baadhi ya mifuko ya saruji na bati walizopewa Halmashauri ya Manispaa ya Iringa
Mwenyekiti wa chama cha mapinduzi manispaa ya Iringa Said Rubeya akifanya kazi kwa vitendo wakati wa hafla ya kukabidhi msaada huo
Mwenyekiti wa umoja wa vijana Mkoa wa Iringa Kenani kihongosi akifanya kazi kwa vitendo
Mbunge wa viti maalum Mkoa wa Iringa Ritta Kabati akifanya kazi kwa vitendo
Na Fredy Mgunda, Iringa.
Chama cha mapinduzi mkoa wa Iringa kimeanzimisha miaka arobain na moja (41) kwa kutoa msaada wa bati mia tatu (300) na mifuko ya saruji mia tano (500) kwa halmashauri ya Manispaa ya Iringa kwa ajili ya kusaidia ukarabati na ujenzi kwenye shule zenye mahitaji hayo kwa kufanya kazi za kimaendeleo
Akizungumza wakati wa kukabidhi
msaada huo Katibu wa chama cha mapinduzi Mkoa wa Iringa Christopher Magala alisema kuwa wameamua kutoa msaada kwa kutimiza
malengo ya ilani ya chama cha mapinduzi ya mwaka 2015 hadi 2020 kwa kuwatumikia
wananchi waliowaweka madarakani hivyo kufanya ni sehemu ya kazi za chama.
“Tunachokifanya hii leo ni
kuendelea kuonyesha wananchi waliotuweka madarakani jinsi gani tunavyofanya
kazi kwa mjibu wa ilani yetu kama mwenyekiti wa chama Dr John Pombe Magufuli
anavyotekeleza vizuri ilani yetu” alisema Magala
Magala alisema kuwa halmashauri
ya manispaa ya Iringa imekuwa kama yatima kimaendeleo kutokana na utendaji kazi
wa viongozi wanayoingoza halmashauri hivyo chama cha mapinduzi mkoa wa Iringa
kimeamua kuanza kufanya kazi za kimaendeleo kwa wananchi.
“Leo hii hakuna kitu kipya
ambacho kimefanya na halmashauri ya Iringa ndio maana tumeingia kazini kufanya
kazi kwa nguvu zetu zote hivyo tutawatumikia wananchi ipasavyo na kuhakikisha
manispaa inasonga mbele kimaendeleo” alisema Magala
Magala alisema kuwa wameamua kukabidhi
misaada hiyo sambamba na kufanya kazi katika shule ya sekondari ya Mawelewele
iliyopo kata ya Mwangata kama mfano wa kuikwa kwa wananchi wa kata hiyo
sambamba na wanafunzi na viongozi wengine kufanya kazi kwa vitendo na sio kukaa
tu maofisini.
“Leo tunakabidhi kama mfano tu
wa msaada wetu hapa shuleni tunatoa bati mia hamsini na mifuko ya saruji sitini
kwa lengo la kusaidia kumalizika kwa ujenzi huu ambao unaendelea hii leo hivyo
naomba uupokee msaada huu ambao najua kwa kiasi furani utachangia maendeleo ya
shule hii” alisema Magala
Aidha Magala aliwataka walimu
wa shule hiyo kufundisha kwa kuhudi na maarifa ili kuongeza ufaulu wa wanafunzi
wa shule hiyo kwa kuwa serikali inatoa elimu bure bila malipo na kufanikisha
kila mtoa apate elimu inayostali.
“Naombeni na sitaki kusikia
kuna mtoto amefukuzwa shule kwa kukosa ada wala michango yoyote ile hapo
mtanijua mimi nani na jinsi gani navyosimamia ilani ya chama changu hivyo naomba
mfanye majukumu yenu kama mnavyotakiwa kufanya” alisema Magala
Magala aliwataka viongozi wote
wa mkoa,wilaya, kata hadi tawi kuhakikisha wanafanya kazi vuizuri kwa kusimamia
ilani ya chama cha mapinduzi ili kuendelea kutoa huduma bora kwa wananchi ambao
wamewaka madarakani.
Baada ya kupokea msaada huo
mkuu wa wilaya ya Iringa Richard Kasesela alikishukuru chama cham mapinduzi
mkoa wa Iringa kwa kutoa msaada huo ambazo utasaidia kutatua matatizo ya
miundimbinu ya shule za manispaa ya Iringa ambazo zipo taabani kabisa.
“Kazi mnayoifanya kweli
ilitakiwa kufanywa na serikali ya halmashauri ya manispaa ya Iringa lakini
imeshindwa hivyo naomba nitoe shukrani zangu za dhati kwa viongozi wangu wote
CCM mkoa wa Iringa kwa kazi kubwa mnayoifanya kuhakikisha wananchi wanapata
maendeleo” alisema Kasesela
Kasesela aliongeza kuwa kuwepo
kwa upinzani ndani ya halmashuri ya manispaa ya Iringa kunarudisha nyuma
maendeleo ya wananchi kwa kuwa wapinzani hawafanyika kazi kama inavyostahili
hivyo tunaomba viongozi wa chama mtusaidie msaada wa kutuletea maendeleo.
“Halmashauri ya manispaa ya
Iringa ni yatima hivyo tunaomba chama cha mapinduzi kupitia viongozi wangu
mtusaidie kufanya shughuli za kimaendeleo msiishie leo tu maanakuna vitu vingi
bado havijakaa sawa” alisema Kasesela
Kasesela akatoa agizo kwa
kiongozi yeyoto Yule atakayetumia vibaya msaada huo ulitolewa na chama cha
mapinduzi atakula naye sahani moja hadi atajuta kwa kwanini ametumia vibaya
msaada huo.