Waziri wa Fedha na Mipango
ya Uchumi wa Rwanda Mhe. Gatete Claver akisaini kitabu cha wageni alipowasili
katika Ofisi ya Waziri wa Fedha na Mipango Jijini Dar es Salaam kwa ajili ya
Mkutano kuhusu upatikanaji wa Fedha za mradi wa Reli ya Kisasa (SGR) kuanzia
Isaka Shinyanga hadi Kigali nchini
Rwanda.
Waziri wa Fedha na
Mipango wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) (wa pili kulia), Waziri
wa Fedha na Mipango ya Uchumi wa Rwanda Mhe.
Gatete Claver (kushoto) na Balozi wa Rwanda nchini Tanzania Eugene
Kayihura (kulia) wakiwa katika majadiliano ya pamoja kabla ya kuanza kwa
mkutano kuhusu namna ya kupata fedha kwa ajili ya mradi wa ujenzi wa Reli ya
Isaka Shinyanga hadi Kigali nchini Rwanda.
Mkutano kati ya Waziri wa Fedha na Mipango wa Tanzania
Mhe. Dkt Philip Isdor Mpango (wa pili kushoto) na Waziri wa Fedha na Mipango ya
Uchumi wa Rwanda Mhe. Gatete Claver (wa
pili kulia) ukiendelea kuhusu upatikanaji wa fedha za mradi wa Reli ya Isaka
Shinyanga hadi Kigali nchini Rwanda katika ukumbi wa Wizara ya Fedha na Mipango
Jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Fedha na
Mipango ya Uchumi wa Rwanda Mhe. Gatete
Claver (wa pili kulia) akizungumza jambo wakati wa mkutano kati yake na Waziri
wa Fedha na Mipango wa Tanzania Mhe. Dkt Philip Isdor Mpango (Mb) (hayupo
pichani) kuhusu upatikanaji wa fedha za mradi wa Reli ya Isaka Shinyanga hadi
Kigali nchini Rwanda katika ukumbi wa Wizara ya Fedha na Mipango Jijini Dar es
Salaam.
Waziri wa Fedha na
Mipango ya Uchumi wa Rwanda Mhe. Gatete
Claver (kushoto) na mwenyeji wake Waziri wa Fedha na Mipango wa Tanzania Mhe.
Dkt Philip Isdor Mpango (kulia) wakiondoka baada ya kumalizika kwa mkutano
kuhusu upatikanaji wa fedha za mradi wa Reli ya Isaka Shinyanga hadi Kigali
nchini Rwanda Jijini Dar es Salaam.
Ujumbe kutoka
Wizara ya Fedha na Mipango ukiongozwa na Waziri Mhe. Dkt Philip Isdor Mpango (Mb) (kushoto) na kutoka Rwanda ukiongozwa
na Waziri wa Fedha na Mipango ya Uchumi wa Rwanda Mhe. Gatete Claver (wa pili kulia) wakifurahia
jambo baada ya kumalizika kwa Mkutano kati yao Jijini Dar es Salaam.
Katibu Mkuu wa
Wizara ya Fedha na Mipango wa Tanzania Bw. Doto James (kulia) na mwenzake wa
Rwanda Bw. Caleb Rwaunganza wakisaini maagizo kutoka kwa Mawaziri wa Wizara
hizo mbili kuhusu hatua za upatikanaji
wa fedha za mradi wa Reli ya Isaka Shinyanga hadi Kigali nchini Rwanda Jijini
Dar es Salaam.
Benny Mwaipaja, WFM
Mawaziri wa Fedha
na Mipango wa Tanzania na Rwanda
wamekutana Jijini Dar es Salaam kujadili
namna ya kupata fedha za Ujenzi wa Reli yenye Kiwango cha Kimataifa (SGR) kutoka
Isaka Shinyanga hadi Kigali Rwanda ikiwa ni mwendelezo wa mikutano kuhusu suala
hilo iliyoanza kuanzia Januari 20, 2018.
Katika Mkutano huo
wamejadili kuhusu njia ambayo inaweza kuwa rahisi kupata fedha ikiwemo ya kutumia
Sekta binafsi, Serikali kukopa au kumweka mwekezaji ambapo wamekubaliana kupitia
upya taarifa zilizo wasilishwa mezani za pande hizo mbili na kufanya maboresho na pia kuzungumza na
Benki ya Dunia (WB), Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) na Benki ya Maendeleo
ya Afrika kwa pamoja ili wakati wa kikao kijacho waweze kujadili suala hilo kwa
kuangalia vigezo na masharti ya kupata fedha.
Kikao hicho ambacho
ni cha watalamu kimewakutanisha Waziri wa Fedha na Mipango wa Tanzania Mhe.
Dkt. Philip Isdor Mpango na Waziri kutoka Rwanda Mhe. Gatete Claver pamoja na Balozi
wa Rwanda nchini Tanzania, Eugene Kayihura na Makatibu wakuu wa wizara hizo na
wajumbe wengine.
Katibu Mkuu wa
Wizara ya Fedha na Mipango wa Tanzania Bw. Doto James na mwenzake wa Rwanda Bw.
Caleb Rwaungaza, wamesaini maagizo hayo ya Mawaziri kwa ajili ya utekelezaji.
Ikumbukwe kuwa mapema
mwezi huu Mhe. Rais Dkt. John Pombe Joseph Magufuli na Rais wa Rwanda Paul
Kagame walikubaliana kutekeleza mradi huo wa ujenzi wa Reli kutoka Isaka
Shinyanga hadi Kigali Rwanda na wakatoa maagizo ya kuanza utekelezaji kwa
kuangalia namna ya kupata fedha za mradi huo.