BASI LA KAMPUNI YA TAHMED LAUNGUA MOTO LIKIWA SAFARINI

January 29, 2018

 NA MWANDISHI WETU,HANDENI.
BASI la kampuni ya Tahmed lililokuwa linafanya safari zake kati ya Dar es Salaam na Arusha limewaka moto na kuungua katika eneo la Kitumbi Kata ya Kabuku wilayani Handeni mkoani Tanga likiwa njiani huku akibiria wakinusufika baada ya kuwahi kutoka nje.
Kamanda wa Polisi mkoani Tanga,Edward Bukombe aliuambia Mtandao wa Tanga Raha kuwa  tukio hilo lilitokea leo saa nne na dakika arobaini na tano likiwa linaelekea mkoani Arusha.
Alilitaja gari hilo lenye namba za usajili T.483 DFL lilikuwa likiendeshwa na Bakari Saidi (30) likiwa na abiria sita lilipofika eneo hilo ndipo lilipowaka moto kutokana na hilifau za kiufundi .
Alisema wakati basi hilo likianza kuwaka moto abiria waliokuwepo ndani waliwahi kutoka na kujinusuru na kifo huku wakiliacha likiendelea kuungua moto .
Hata hivyo Kamanda huyo alisema chanzo cha ajali hiyo bado wanafuatilia ili kuweza kubaini moto huo ulisababishwa na nini.
“Labda nisema taarifa ya kuungua moto na kuwaka basi hilo ni kweli kwa sasa tunafanya uchunguzi kwa lengo la kubaini nini chanzo chake “Alisema.
Mwisho.

Share this

Related Posts

Previous
Next Post »