Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Ndugu Dr.
Harrison Mwakyembe, Leo Jumamosi Januari 20, 2018 ameitembelea timu ya
Taifa ya Vijana chini ya miaka 16 Serengeti Boys iliyopo kambini kwenye
hostel za Makao Makuu ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania TFF na
kuwaachia ujumbe wa Serikali.
Dr.
Mwakyembe akitoa salamu za Serikali amewaambia Vijana wanaounda timu
hiyo kuwa serikali inawaamini na wanalo jukumu la kuiperusha vyema
bendera ya Tanzania.
Amewataka
kupambana kwaajili ya Tanzania na kuhakikisha wanafanya vyema kwenye
kila mashindano huku akiwataka makocha wa kikosi hicho kuwapa mafunzo
mazuri kwa ustawi wa Vijana hao.
Aidha
Dr. Mwakyembe amesema anaamini Vijana hao watakuwa bora chini ya TFF
iliyopo madarakani inayoongozwa na Rais Ndugu Wallace Karia.
"Naamini mtaimarika na kuwa bora maana hata TFF hii sasa ina ari na morali kubwa".Alisema Dr. Mwakyembe.
Katika
ziara yake hiyo Dr. Mwakyembe alipata nafasi ya kutazama mchezo wa
kirafiki kati ya Serengeti Boys na Makongo Sekondari iliyomalizika kwa
Serengeti Boys kupata ushindi wa mabao 4-1.
Kabla
ya mchezo huo Serengeti Boys walicheza mchezo mwingine wa kirafiki
dhidi ya Kituo cha Bombom iliyomalizika kwa sare ya kufungana bao 1-1.
IMETOLEWA NA SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA TFF