Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Dk Steven Kebwe
akimuongoza Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Jenerali Venance Mabeyo kushoto
na Mkuu wa Wilaya ya Kilosa Mh. Adam Mgoyi katikati wakati walipokagua
athari za uharibifu wa madaraja, Mashamba na nyumba za wananchi
kufuatia mafuriko yaliyosababishwa na mvua kubwa zinazonyesha wilayani
Kilosa mkoani Morogoro
Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Dk Steven Kebwe
akitoa maelezo kwa Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Jenerali Venance Mabeyo
katikati na Mkuu wa Wilaya ya Kilosa Mh. Adam Mgoyi kushoto wakati
walipokagua athari za uharibifu wa madaraja, Mashamba na nyumba za
wananchi kufuatia mafuriko yaliyosababishwa na mvua kubwa
zinazonyesha wilayani Kilosa mkoani Morogoro
Maji yakiwa yametapakaa
kandokando ya Reli ya kati na kusababisha uharibifu mkubwa wa reli,
Mashamba pamoja na nyumba za wananchi.
Madaraja yakiwa katika hatari ya kusombwa kutokana na mvua hizo
…………………………………………………………………………………………………….
Na. Andrew Chimesela – Morogoro
Hali mbaya ya mafuriko
yanayoendela kuathiri wananchi wa Wilaya ya Kilosa Mkoani Morogoro
yamemfanya Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Tanzania Generali Venance Mabeyo
kufika Kilosa na kutembelea baadhi ya maeneo yaliyoathirika ili kutafuta
ufumbuzi wa pamoja wa kuokoa maisha ya wananchi wa maeneo hayo na mali
zao.
Generali Mabeyo aliwasili Kilosa
Jan.19, 2018 majira ya jioni na kuungana na mwenyeji wake Dkt. Kebwe
Stephen Kebwe Mkuu wa Mkoa wa Morogoro aliyepiga kambi Wilayani humo kwa
ajili ya mafuriko hayo kisha bila kujali mvua iliyokuwa inaendelea
kunyesha muda wote wakatembelea baadhi ya maeneo yaliyoakuwa
yamethiriwa ili kuona hali halisi ya mafuriko hayo.
Kwenye kikao cha majumuisho Mkuu
huyo wa Majeshi nchini alishauri kuwa ili kutatua changamoto hiyo
inatakiwa nguvu ya ziada na ya pamoja kwa taasisi zote kuungana, Ikiwa
ni pamoja na taasisi mbali ili kuweza kuokoa maisha ya watu, mali zao
pamoja na miundombinu iliyoathiriwa.
Hata hivyo alisema changamoto
hiyo inatakiwa kuwe na mpango wa muda mfupi, muda wa kati na muda mrefu.
Amesema suluhisho la mpango wa mda mfupi ni kuwa na kazi ya dharura, na
kazi hiyo ya dharura inahitajika kuwepo na mpango wa dharura ambao ni
kuokoa maisha ya watu waliozingirwa na maji ili wasiendelee kukosa
huduma za kijamii na pia kuathiri afya zao kwa kunywa maji ambayo si
salama.
Pamoja na kuwepo kwa wazo la
kurekebisha tuta la mto Mkondoa ikiwa ni mpango wa muda wa kati ili maji
hayo yafuate mkondo wake lakini pia Generali Mabeyo ameshauri kuangalia
namna ya kupunguza kasi ya maji hayo kuanzia yanakotoka kwa kujenga
mabwawa ikiwa ni mpango wa muda mrefu.
“Maji haya yanakuja huku ni kama
sisi ni waathirika zaidi lakini yanakoanzia hatujui hali iko namna gani,
pengine katika mpango wa muda mrefu ingetazamwa namna ya kuyapunguza
haya maji kasi yake.Sasa katika kuyapunguza, taasisi mablimbali zina
wataalamu ambao wanaweza kusaidia kuweza kujenga mabwawa makubwa huko
yanakoanzia ili haya maji kupunguza kasi yake kabla hayajafika huku”
alisema Generali Mabeyo.
Akitoa maelezo ya awali Mkuu wa
Mkoa wa Morogoro Dkt. Stephen Kebwe amesema tuta hilo la mto Mkondoa
lilijengwa enzi za Mkoloni kama kinga kwa mji wa Kilosa na kwa mara ya
kwanza lilipasuka mwaka 2010. Ujenzi wake kuanzia hapo haukukamilika
vizuri kutokan na hali ya kifedha na sasa limepasuka baada ya Mvua
nyingi kunyesha kuamkia Jan,11 mwaka huu.
Hata hivyo Dkt. Kebwe ametoa Ombi
kwa Mkuu huyo wa Majeshi, kupata nguvu kazi ya wanajeshi, vifaa na
utaalamu wao ili baada ya mvua hizi kupungua waendelee na kutafuta mbinu
ya kuuongozo mto Mkondoa uweze kupita katika sehemu yake ya awali na
hivyo kutoathiri wananchi, mali zao na miundombinu iliyopo eneo hilo .