Baadhi ya
Wawekezaji na wageni kutoka Taasisi za Kimataifa walioshiriki Mkutano wa
tatu wa majadiliano kati ya wadau wa Sekta Binafsi na Sekta ya Umma
uliofanyika mjini Dodoma.
Makamu Mwenyekiti
wa Taasisi ya Sekta Binafsi nchini (TPSF), Bw. Salum Shamte,
akizungumza wakati wa mkutano wa tatu kati ya Sekta Binafsi na Sekta ya
Umma uliojadili namna ya kuboresha masuala ya biashara na uwekezaji
nchini, mjini Dodoma.
Baadhi ya Wafanyabiashara na
Wawekezaji walioshiriki Mkutano wa tatu wa majadiliano kati ya wadau wa
Sekta Binafsi na Sekta ya Umma uliofanyika mjini Dodoma.
Baadhi ya
Manaibu Mawaziri, Makatibu Wakuu na Manaibu Makatibu Wakuu na Maafisa
wengine kutoka Wizara mbalimbali wakifuatilia mkutano kati ya Sekta
Binafsi na Sekta ya Umma, Mjini Dodoma.
Baadhi ya Wafanyabiashara na
Wawekezaji walioshiriki Mkutano wa tatu wa majadiliano kati ya wadau wa
Sekta Binafsi na Sekta ya Umma uliofanyika mjini Dodoma.
Sehemu ya wadau mbalimbali
wakiwemo wabunge, wawekezaji na viongozi wa Serikali walioshiriki
mkutano kati ya Sekta Binafsi na Sekta ya Umma, Mjini Dodoma.
Baadhi ya wabunge wakifuatilia kwa makini mkutano wa tatu wa wadau wa Sekta Binafsi na Sekta ya Umma uliofanyika mjini Dodoma
Waziri wa
Fedha na Mipango, Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) akifungua mkutano wa
tatu kati ya Sekta Binafsi na Serikali uliofanyika mjini Dodoma.
Katibu Mkuu wa
Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji Prof. Elisante Ole-Gabriel,
akionesha kabrasha lenye maelezo ya utekelezaji wa makubaliano
mbalimbali yaliyotekelezwa na yanayoendelea kutekelezwa baada ya
mikutano miwili ya awali kufanyika Mjini Dodoma na Jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya
Maafisa wa Serikali wakishiriki Mkutano wa tatu wa wadau kutoka Sekta
Binafsi na Sekta ya Umma uliojadili namna ya kuboresha mazingira ya
uwekezaji na ufanyaji biashara nchini, mjini Dodoma
…………………………………………………………………………..
Na Benny Mwaipaja, WFM, Dodoma
Sekta Binafsi nchini imekiri kuwa
uhusiano kati yake na Serikali umezidi kuimarika kutokana na kuboreshwa
kwa mazingira ya uwekezaji na ufanyajibiashara hapa nchini kuliko
ilivyokuwa hapo awali na kwamba hatua hiyo itachochea ukuaji wa uchumi
wa nchi.
Kauli hiyo imetolewa mjini Dodoma
na Makamu Mwenyekiti wa Taasisi ya Sekta Binafsi nchini (TPSF), Bw.
Salum Shamte, wakati wa mkutano wa tatu kati ya Sekta Binafsi na Sekta
ya Umma uliojadili namna ya kukuza ushiriki wa Sekta Binafsi katika
kukuza uchumi wa viwanda nchini.
“Sekta binafsi imenituma kuleta
pongezi kwa Serikali inayoongozwa na Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli kwa kutekeleza kwa vitendo
utambuzi wa kwamba Sekta Binafsi ni mbia muhimu wa maendeleo ya Taifa
letu” alisema Bw. Shamte.
Aliyataja baadhi ya mafanikio
yanayo onekana bayana kuwa ni pamoja na kuinusuru Bandari ya Dar es
Salaam kwa mabadiliko ya sheria ya fedha ya mwaka 2017 hasa kuondoa VAT
kwenye biashara ya mizigo ya kimataifa na kuondokana na umoja wa forodha
ambao ulipunguza kwa kiasi kikubwa kiwango cha biashara kati ya
Tanzania na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.
Bw. Shamte alisema kuwa
majadiliano hayo kati ya Serikali na Sekta Binafsi kumeikoa sekta ya
utalii hasa kwa kuondokana na kodi ya ongezeko la thamani (VAT) kwenye
leseni mbalimbali hatua ambayo imerejesha msisimko wa sekta hiyo.
“Serikali imepunguza pia
mlolongo wa kodi kwa wakulima, japokuwa – kazi haijakamilika lakini
mwanzo ni mzuri” aliongeza Bw. Shamte
Alieleza kuwa jitihada mpya na
nzuri za kutatua changamoto za kodi kwa kampuni zinazojihusisha na
biashara kati ya Tanzania Bara na Visiwani, na kuanza kufanya malipo kwa
wakandarasi na watoa huduma wa ndani hatua ambayo wanaamini itakuza
matumizi ya ndani na mzunguko wa fedha.
Makamu mwenyekiti huyo wa TPSF
alisema kuwa Serikali ya Awamu ya Tano ni sikivu na kwamba kwa mara ya
kwanza, wanatarajia kushuhudia Bajeti Kuu ya Serikali ya mwaka 2018/2019
ikiwa bora zaidi kwa kubeba mapendekezo yao mengi yatakayosaidia kukuza
sekta hiyo na pia kuboresha masuala ya kodi na mapato ya Serikali.
Wakizungumza kwenye mkutano huo,
Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Mpango, na Waziri wa Viwanda,
Biashara na Uwekezaji Bw. Charles Mwijage, wamesema kuwa Serikali
inathamini mchango wa Sekta Binafsi katika maendeleo ya uchumi wa
viwanda na kwamba itaendelea kutatua changamoto mbalimbali zinazoikabili
Sekta hiyo ikiwemo masuala ya kodi.
“Sekta Binafsi ndiyo mhimili wa
uchumi kwa hiyo ni muhimu tuhakikishe upande wa Serikali tunafanya
wajibu wetu kuiweesha Sekta hiyo iwe imara zaidi na iweze kukua kwa
sababu tutapata ajira, bidhaa bora na huduma mbalimbali hatimaye kukuza
uchumi wetu wa viwanda” alisisitiza Dkt. Mpango
Waziri wa Viwanda, Biashara na
Uwekezaji naye aliongeza kuwa Sekta Binafsi ndiyo itakayojenga viwanda
wakati Serikali itakuwa mwezeshaji ndio maana wameamua kukaa pamoja
kujadili changamoto zinazozikabili pande zote mbili na kwamba baadae
watajielekeza kujadili na kila Sekta ili kuharakisha maendeleo ya
kiuchumi.
Wametoa wito kwa Sekta binafsi
nchini kujenga uaminifu na kufuata sheria na kanuni za ufanyajibiashara
na uwekezaji nchini ikiwemo kulipa kodi stahiki.
Akizungumza katika mkutano huo wa
tatu uliojumuisha wadau mbalimbali kutoka ndani na nje ya nchi,
Mkurugenzi wa Shirika la Maendeleo la Marekani (USAID) hapa nchini, Bw.
Andy Karas, ameimwagia sifa Tanzania kwa kukuza uchumi wake kwa wastani
wa asilimia 7 na kushauri kuwa uchumi huo sasa uelekezwe kutatua
changamoto za wananchi hususan kukuza sekta ya kilimo inayoa ajiri idadi
kubwa ya watanzania.