TRA YAKUSANYA TRILIONI 11.78 NDANI YA MIEZI 9

April 10, 2018


Mkurungezi Mamlaka ya mapato Tanzania TRA Akiongea na Wandishi wa habari jijini Dar Es Salaam kitoa Ufaanuzi juu ya makusanyo ya kodi Kwa kipindi cha meizi Tisa Mwaka wa fedha 2017/2018
………………
Katika kipindi cha miezi tisa Mwaka wa fedha 2017/2018 Mamlaka ya Mapato Tanzania TRA imekusanya jumla ya shilingi Tirion 11.78 ikilinganishwa na shilingi Tirioni 10.86 amabazo zilikusanywa Mwaka wa fedha 2016/2017, Kiasi hiki sawa na ukuaji wa silimia 8.6.

Mkurugenzi wa Huduma na Elimu kwa Mlipa Kodi Mamlaka ya Mapato TRA Bw. Richard Kayombo amesema hayo Leo wakati akizungumza na wandishi wa Habari Jijini Dar es Salaam wakati akitoa taarifa ya makusanyo ya kodi kwa kipindi hicho.

Richard Kayombo amongeza kuwa katika mwezi Machi TRA imekusanya jumla ya shilingi Trrioni 1.54 akilinganishwa na makusanyo ya mwezi Machi 2017 Ambapo ilikusanya Shilingi tirioni 1.34 sawa na ukuaji wa asilimia 14.49
Ameongeza na kusema””Katika Kipindi hiki Mamlaka ya Mapato TRA inaendelea na usajili wa walipa kodi wapya ambapo Kwa wiki hii usajili unafanyika mkoani Geita”” alisema Kayombo.
Mkurungezi wa Huduma na Elimu Kwa Mlipa kodi Mamlaka ya Mapato TRA Amewakikishia wananchi kuwa TRA itandele kutoa elimu hii Kwa kila anae stahili kulipakodi Kwa hiyari na kwa wakati na kila Mwenye malalamiko juu ya makadirio amuone meneja wa eneo husika akiwa na vielelezo vyote vinavyotakiwa kwa mlipa kodi

Share this

Related Posts

Previous
Next Post »