Waziri
wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Dkt.
Augustine Mahiga(katikati) akiongea katika kikao cha uongozi wa Wizara
hiyo na Wabunge Wateule wa Tanzania kwenye Bunge la nne (4) la Jumuiya
ya Afrika Mashariki, kilichofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa
Kimataifa wa Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam, tarehe 12 Disemba
2017. Pembeni yake kushoto ni Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na
Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Susan Kolimba na kulia ni
Mwenyekiti wa Wabunge wateule wa Bunge la Afika Mashariki, Mhe. Abdullah
Makame.
Katibu
Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Prof.
Adolf Mkenda (kulia) akiongea katika kikao hicho ambapo aliwakaribisha
Waheshimiwa Wabunge wateule pamoja na kuwaeleza kuwa Wizara ya Mambo ya
Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki ipo tayari kuwapa ushirikiano
katika utekelezaji wa majukumu yao. Pembeni yake Naibu Katibu Mkuu wa
Wizara hiyo Balozi Ramadhan Muombwa Mwinyi.
Mwenyekiti
wa Wabunge Wateule wa Bunge la Jumuiya ya Afrika Mashariki, Mhe.Dkt.
Abdullah Makame akiushukuru uongozi wa Wizara ya Mambo ya Nje na
Ushirikiano wa Afrika Mashariki kwa kikao kizuri cha utangulizi kabla ya
kuanza kwa Bunge hilo na pia akaahidi kuwa wataenda kuliwakilisha Taifa
vizuri sambamba na kusimamia maslahi ya Jumuiya kwa maendeleo na ustawi
wa wananchi wake.
Sehemu
ya Waheshimiwa Wabunge Wateule wa Bunge la Afrika Mashariki
wakifuatilia maelekezo yaliyokuwa yakitolewa na Mhe. Waziri Mahiga
(hayupo pichani)
Sehemu nyingine ya Waheshimiwa Wabunge wakifuatilia kikao hicho.
Wakurugenzi
wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki
wakifuatilia kikao hicho. Kutoka kulia Bw. Eliabi Chodota, Bw. Bernard
Haule na Bw.Joachim Otaru
Mkurugenzi
wa Idara ya Siasa, Ulinzi na Usalama katika Wizara ya Mambo ya Nje na
Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Bw. Stephen Mbundi akitoa ufafanuzi
kuhusiana na taratibu na miongozo ya Jumuiya ya Afrika Mashariki kwa
Waheshima Wabunge Wateule.
Mhe.
Waziri na Naibu Waziri wakiwa katika picha ya pamoja na Wabunge Wateule
wa Tanzania kwenye Bunge la nne la Jumuiya ya Afrika Mashariki.
Picha ya pamoja uongozi wa Wizara na Wabunge Wateule wa Tanzania kwenye Bunge la nne la Jumuiya ya Afrika Mashariki.