Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.
John Pombe Magufuli akifungua rasmi Tawi la Benki ya CRDB lililopo katikati ya
mjini wa Dodoma. Wengine katika picha ni Mke wake Mama Janeth Magufuli watatu
kutoka (kushoto), Waziri Mkuu mstaafu Mzee John Samwel Malecela wanne kutoka
kushoto pamoja na viongozi wengine wa kitaifa na wa mkoa wa Dodoma.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipiga makofi na
Waziri Mkuu mstaafu Mzee John Samwel Malecela, Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli
pamoja na viongozi wengine mara baada ya kufungua rasmi Tawi hilo la Benki ya
Biashara ya CRDB lililopo mjini Dodoma.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa amekaa na
Waziri Mkuu mstaafu Mzee John Samwel Malecela, katika eneo la wateja maalum wa
Benki ya CRDB ndani ya Tawi hilo jipya alilolifungua.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimpongeza Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB Dkt. Charles Kimei mara baada ya kufungua Tawi jipya la CRDB lililopo mjini Dodoma. |
Mke
wa Rais Mama Janeth Magufuli akiagana na baadhi ya wafanyakazi wa Benki ya CRDB
mara baada ya sherehe za ufunguzi wa Tawi jipya la CRDB lililopo mjini Dodoma.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Waziri Mkuu mstaafu Mzee John
Samwel Malecela mara baada ya ufunguzi wa Tawi la Benki ya CRDB lililopo mjini Dodoma.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na msanii Peter Msechu aliyekuwa
akitumbuiza na Bendi yake katika sherehe za ufunguzi wa Tawi jipya la CRDB
lililopo mjini Dodoma.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Spika wa Bunge Job Ndugai
wakati alipokuwa akitoka ndani ya Tawi jipya la Benki ya CRDB lililopo mjini
Dodoma.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimkabidhi mkuu wa mkoa wa Dodoma Dkt. Bilinith Mahenge hundi hiyo ya kiashi cha
Tsh. Milioni mia moja (100,000,000/=) itakayotumika katika ujenzi wa Wodi ya
wagonjwa itakayojengwa katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Dodoma. PICHA NA IKULU