Katibu Mkuu wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Wilfred Kidau akiongea na waandishi wa habari namna ambayo Timu ya stars ilivyoshiriki kampeni hiyo na pia akishukuru udhamini wa SBL kwa timu hiyo ,Katikati ni Ofisa Mnadhimu wa Kikosi cha Usalama Barabarani ACP Theopista Mallya na mwishoni ni Mkurugenzi Mtendaji wa SBL Helene Weesie ,mapema jana katika hoteli ya Hyatt Regency jijini Dar es salaam. |
Waandishi wa habari wakichukua matukio |
Moja ya Matangazo ambayo yatakuwa yakihamasisha unywaji wa kistaarabu
Dar es Salaam, Novemba 30 2017. Kampuni ya bia ya Serengeti (SBL) leo imezindua kampeni ya miezi miwili kuhamasisha wanywaji juu ya unywaji pombe wa kistaarbu kama jitihada za kampuni katika kupunguza changamoto za ajali nyingi barabarani hasa katika msimu huu wa sikukuu.
Katika kampeni hii, bia ya Serengeti Premium Lager imeungana na Timu ya Taifa, Taufa Stars kuhimiza umuhimu wa unywaji kistaarbu
Kampeni hiyo iliyopewa jina la “Mastaa wa kweli hunywa kistaarabu” Bia ya Serengeti imejikita kutoa elimu kwa watumiaji wa vyombo vya moto, abiria, waenda kwa miguu na jamii yote kwa ujumla juu ya umuhimu wa usalama barabarani msimu huu wa sikukuu. Kampeni hiyo itadumu kwa kipindi cha miezi miwili
Kampeni hii ya kitaifa inayohusisha wachezaji wa Timu ya Taifa, Taifa Stars itaonekana katika baa na vilabu mbalimbali na pia kwenye matangazo ya nje, runinga, redioni na mitandao mbalimbali ya kijamii. Bia ya Serengeti Premium ndiyo mdhamini mkuu wa Timu ya Taifa, Taifa Stars.
“SBL imejikita sio tu katika usalama wa wafanyakazi wetu na mali zetu pia katika jamii kubwa ya Watanzania kwa ujumla ambapo biashara yetu ni kati ya sehemu hiyo. Ni kwa misingi hiyo basi kampeni hii ya “Mastaa wa kweli hunywa kistaarabu” inalenga kutoa elimu kwa vijana, waendesha magari na bodaboda, waenda kwa miguu na jamii nzima kwa ujumla juu ya unywaji kistaarabu katika kipindi hiki cha kuelekea msimu wa sikukuu na kuonya matumizi ya uendeshaji chombo cha moto ukiwa katika hali ya ulevi” alisema Mkurugenzi Mkuu wa SBL Bi Helene Weesie wakati wa sherehe za uzinduzi
Mkurugenzi huyo wa SBL amesema kuwa kampuni yake imekuwa ikiendesha kampeni ya Unywaji wa Kistaarbu kwa takribani miaka mitano sasa kwa ushirikiano kutoka kwa Jeshi la Polisi nchini na wadau mbalimbali waliojitolea katika kuhakikisha usalama barabarani. Uelimishaji wa unywaji pombe kistaarabu unafanywa kwenye vyuo, sehemu za kazi na kwenye baa ambapo wahusika huelimishwa ni kwa kiasi gani kinywaji akipendacho kina kilevi ndani yake
“Katika kuwatakia Watanzania msimu wa fanaka na Baraka za sikukuu, tuna jukumu la kuwakumbusha kuendelea kufurahia bidhaa za SBL kistaarabu na kubaki salama wakati wakisherehekea na marafiki na familia” aliongezea
Akihudhuria hafla hiyo, Ofisa Mnadhimu wa Kikosi cha Usalama Barabarani ACP Theopista Mallya aliwashukuru SBL kwa mpango wao akisema kuwa ni mchango chanya katika kukuza usalama wa barabarani katika msimu huu wa sikukuu.
Malya alilaumu juu ya uharibifu wa mali na vifo vitokanavyo na ajali akisisitiza kuwa ajali za barabarani pia zinawapa mzigo mkubwa sana sekta ya afya nchini katika kuwahudumia manusura wa ajali.
EmoticonEmoticon