Makamu
Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Sheria ndogo inayohusu
dhana, sheria na mfumo wa usimamizi wa maafa Mhe. William Ngeleja akitoa
maelezo ya awali kuhusu utendaji kazi wa kamati hiyo wakati wa Warsha
ya siku moja kwa wabunge wa Kamati hiyo iliyoandaliwa na Idara ya
Uratibu wa Maafa Ofisi ya Waziri Mkuu Novemba 12, 2017 bungeni Mjini
Dodoma.
Waziri
wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Ajira na Watu wenye Ulemavu)
Mhe. Jenista Mhagama akitoa maelezo kuhusu utekelezaji wa majukumu ya
Idara ya Uratibu wa Maafa na namna Serikali inavyojenga uwezo wa Idara
hiyo ili kuongeza tija wakati wa Warsha ya siku moja kwa wabunge Kamati
ya Kudumu ya Bunge ya Sheria ndogo inayohusu dhana, sheria na mfumo wa
usimamizi wa maafa .
Naibu
Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Ajira na Vijana), Mhe. Antony
Mavunde akisisitiza jambo wakati wa Warsha ya siku moja kwa wajumbe wa
Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Sheria ndogo inayohusu dhana, sheria na
mfumo wa usimamizi wa maafa iliyoandaliwa na Idara ya Uratibu Maafa
Novemba 12, 2017 bungeni Dodoma.
Katibu
Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera na Uratibu) Prof. Faustin Kamuzora
akiwashukuru wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Sheria ndogo
inayohusu dhana, sheria na mfumo wa usimamizi wa maafa wakati wa Warsha
ya siku moja kwa wabunge wa Kamati hiyo iliyoandaliwa na Idara ya Maafa
Ofisi ya Waziri Mkuu Novemba 12, 2017 Mjini Dodoma.
Mkurugenzi
wa Idara ya Uratibu wa Maafa Ofisi ya Waziri Mkuu Brig. Jen. Mbazi
Msuya akitoa maelezo kuhusu utendaji wa Idara yake kwa wajumbe wa Kamati
ya Kudumu ya Bunge ya Sheria ndogo inayohusu dhana, sheria na mfumo wa
usimamizi wa maafa wakati wa Warsha ya siku moja kwa wajumbe hao
iliyoandaliwa na Ofisi hiyo mjini Dodoma.
Mjumbe
wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Sheria ndogo inayohusu dhana, sheria na
mfumo wa usimamizi wa maafa Mhe. Aida Kenani akichangia hoja wakati wa
wakati wa Warsha ya siku moja kwa wajumbe wa Kamati hiyo iliyoandaliwa
na Ofisi ya Waziri Mkuu Idara ya Maafa bungeni mjini Dodoma.
Mmoja
wa wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Sheria ndogo inayohusu
dhana, sheria na mfumo wa usimamizi wa maafa mhe. Abdallah Mtolea (Mb)
akisisitiza jambo kwa wajumbe wa kamati na Watendaji wa Idara ya Uratibu
wa Maafa Ofisi ya Waziri Mkuu wakati wa Warsha ya siku moja kwa wajumbe
wa Kamati hiyo iliyoandaliwa na Ofisi hiyo kwa lengo la kutoa uelewa wa
masuala ya menejimenti ya maafa nchini.
Mmoja
wa wawezeshaji kutoka Idara ya Uratibu wa Maafa Ofisi ya Waziri Mkuu Bw.
Charles Msangi akiwasilisha mada wakati wa Warsha ya siku moja kwa
wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Sheria ndogo inayohusu dhana,
sheria na mfumo wa usimamizi wa maafa iliyoandaliwa na Ofisi hiyo ili
kutoa uelewa wa masuala ya Menejimenti ya maafa nchini Novemba 12,
2017. (PICHA ZOTE NA OFISI YA WAZIRI MKUU – DODOMA)
Na. MWANDISHI WETU
Ofisi
ya Waziri Mkuu imeendesha warsha ya siku moja kwa wajumbe wa Kamati ya
Kudumu ya Sheria Ndogo inayohusu Dhana, Sheria na Mfumo wa Usimamizi wa
maafa kwa lengo la kuwajengea uwezo wa masuala ya Menejimenti ya maafa
nchini.
Akizungumza
wakati wa warsha hiyo iliyofanyika Novemba 12, 2017 Makamu Mwenyekiti
wa Kamati hiyo Mhe.William Ngeleja alieleza kuwa warsha hiyo itawajengea
uwezo wajumbe wa Kamati hususani katika utekelezaji wa majukumu yao.
"Warsha
hii ni muhimu kwa wajumbe wa kamati kwani itaongeza uelewa kuhusu
sheria ya Usimamizi wa Maafa namba 7 ya mwaka 2015 pamoja na dhana nzima
ya Menejimenti ya Maafa"
Akifanua
mhe.Ngeleja amesema warsha hiyo itasaidia kuongeza tija katika utendaji
wa kamati hasa katika kuishauri Serikali kuhusiana na masuala ya maafa.
Kwa
upande wake Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Sera,
Bunge, Ajira na Watu wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama aliwaeleza
wajumbe kuwa Serikali inaendelea kuchukua hatua mbalimbali kuimarisha
uratibu wa usimamizi wa maafa nchini ili kujenga uwezo wa Kuzuia,
Kujiandaa, Kukabili na Kurejesha hali pindi maafa yanapotokea hivyo
warsha hii inatija kwa wajumbe wote.
"Warsha
hii itasaidia kuongeza uelewa kwa wajumbe kuhusu namna bora ya
kupambana na majanga yanapoytokea nchini na madhara yake, vyanzo na
sababu za kutokea, hatua zinazochukuliwa na Serikali katika kuzuia,
kupunguza madhara, kujiandaaa , kukabili na kurejesha hali katika ubora
zaidi" Alisisitiza Mhe. Mhagama.
Sambamba
na hilo Mhe. Mhagama alibainisha kuwa Serikali inaendelea kuchukua
hatua mbalimbali ikiwemo kuimarisha uratibu wa usimamizi wa maafa nchini
kwa kuanzisha Idara ya uratibu wa maafa inayotekeleza majukumu yake kwa
mujibu wa sheria, kanuni na taratibu zilizopo.
Pamoja
na hatua hizo Serikali ina sera ya Taifa ya Usimamizi wa maafa ya mwaka
2004 ambayo inaeleza hatua na majukumu ya wadau mbalimbali katika
shughuli za Manejimenti ya maafa na kutoa muongozo wa utekelezaji wake.
Aidha
mmoja wa wajumbe wa kamati hiyo Mhe.Elibariki Kingu alipongeza Ofisi ya
Waziri Mkuu kwa kuendesha warsha hiyo na kushauri serikali kuwekeza
zaidi katika kupambana na majanga yanayoweza kujitokeza hapo nchini.
AWALI
Mada
zilizowasilishwa katika warsha hiyo zilijikita katika Dhana, Sheria na
Mfumo wa Usimamizi wa Maafa hapa nchini ikiwa ni moja ya jukumu la Ofisi
ya Waziri Mkuu kupitia Idara ya Uratibu wa Maafa kwa kuwajengea uwezo
wadau na wananchi kwa ujumla ili kuweza kuyakabili maafa pindi
yanapotokea. Warsha ilikuwa ya siku moja iliyojumuisha wajumbe wote wa
Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Sheria Ndogo kuhusu masuala ya Menejimenti
ya Maafa iliyofanyika Bungeni Dodoma.
EmoticonEmoticon