USAJILI TIMU ZA WANAWAKE WATANGAZWA
Want create site? Find Free WordPress Themes and plugins.
Wakati
Ligi Kuu ya Wanawake Tanzania Bara, ikitarajiwa kuanza Novemba 26, 2017
katika vituo viwili vya Dar es Salaam na Arusha, tayari usajili wa
msimu kwa timu zote 12, umekamilika.
Kwa mujibu wa kalenda ya mashindano, usajili ulipangwa ufanyike kati
ya Oktoba 25 na Novemba 12, mwaka huu na kwamba kuanzia leo Novemba 13
hadi 17, mwaka huu ni kipindi cha pingamizi.
Novemba 18, mwaka huu kutakuwa na kikao cha Kamati ya Sheria kabla ya Novemba 20, mwaka huu kutoa leseni za wachezaji.
Novemba 24, mwaka huu kutakuwa na Semina ya Viongozi wa klabu, Waamuzi na Makamishna jijini Dar es Salaam.
Ligi hatua ya makundi ikianza Novemba 26, mwaka huu ukomo utakuwa
Desemba 9, mwaka huu Ligi Kuu na kupata jumla ya timu nane ambazo
zitacheza ligi hatua ya Nane Bora ‘Super 8’ itaanza Desemba 20, mwaka
huu. Ligi inatarajiwa kumalizika Machi 28, mwakani.
Timu zilizosajili kutoka Kundi A ambazo ziko Dar es Salaam ni Simba
Queens ya jijini Dar es Salaam iliyopanda daraja msimu huu. Timu
nyingine kwenye kundi hilo ni Mburahati Queens, JKT Queens, Evergreen
zote za Dar es Salaam pamoja na timu za Fair Play ya Tanga na mabingwa
watetezi – Mlandizi Queens.
Kundi B litakuwa na timu za Alliance ya Mwanza ambayo imepanda kutoka
kituo cha Dodoma. Timu nyingine ni Marsh Academy pia ya Mwanza; Panama
ya Iringa; Kigoma Sisterz ya Kigoma, Baobab ya Dodoma na Majengo Queens
ya Singida.
EmoticonEmoticon