Leo Novemba 13, 2017 Mahakama
Kuu ya Tanzania kanda ya Dar es Salaam, imemuhukumu msanii maarufu wa
filamu nchini, Elizabeth Michael “Lulu” kutumikia kifungo cha miaka
miwili gerezani baada ya kupatikana na hatia ya mauaji ya bila kukusudia
ya msanii mwenzake marehemu Steven KanumbaHukumu hiyo imesomwa na Jaji
Sam Rumanyika ambaye amesema, ameridhika na ushahidi wa mashahidi wanne
wa upande wa mashtaka na wazee wa baraza waliotoa maoni yao kuwa kweli
mshtakiwa Lulu aliuwa bila ya kukusudia.Lulu ametiwa hatiani chini ya kifungu cha sheria Namba 195 cha cha mwenendo wa mashtaka ya jinai.
EmoticonEmoticon