Katibu
Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. Doto James (kulia) akiwa na
Mwakilishi Mkazi wa Benki ya Dunia katika nchi za Tanzania, Malawi,
Burundi na Msumbiji Bi. Bella Bird, wakielekea kusaini Mkataba wa mkopo
nafuu wa Dola za Marekani milioni 150 (Sh. bilioni 340) kwa ajili ya
kufungua utalii katika Ukanda wa Kusini mwa Tanzania, Jijini Dar es
Salaam
Baadhi
ya Maafisa waandamizi wa Wizara ya Fedha na Mipango, na Katibu Mkuu
Wizara ya maliaasili na Utalii( wa kwanza kushoto) wakifuatilia kwa
makini tukio la kusainiwa kwa Mkataba wa mkopo nafuu wa Dola za Marekani
milioni 150 (Sh. bilioni 340) kwa ajili ya kufungua utalii katika
Ukanda wa Kusini mwa Tanzania, Jijini Dar es Salaam.
Sehemu
ya Ujumbe wa Benki ya Dunia walioshiriki tukio la Tanzania na Benki
hiyo kutiliana saini mkataba wa mkopo nafuu wa Dola za Marekani milioni
150 (Sh. bilioni 340) kwa ajili ya kufungua utalii katika Ukanda wa
Kusini mwa Tanzania, Jijini Dar es Salaam
Katibu
Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii Meja Jenerali Gaudence Milanzi,
akitoa neon la shukurani wakati wa kusainiwa kwa Mkataba wa Mkopo Nafuu
kati ya Serikali ya Tanzania na Benki ya Dunia wenye thamani ya Dola za
Marekani milioni 150 (Sh. bilioni 340) kwa ajili ya kufungua utalii
katika Ukanda wa Kusini mwa Tanzania, Jijini Dar es Salaam. Kulia kwake
ni Mwakilishi Mkazi wa Benki ya Dunia katika nchi za Tanzania, Malawi,
Burundi na Msumbiji Bi. Bella Bird.
Katibu
Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. Doto James (wa pili kulia) na
Mwakilishi Mkazi wa Benki ya Dunia katika nchi za Tanzania, Malawi,
Burundi na Msumbuji, Bi. Bella Bird, wakisaini Mkataba wa Mkopo wenye
masharti nafuu wa Sh. Dola za Marekani milioni 150 sawa na Shilingi
bilioni 340 kwa ajili ya Mradi wa kuibua fursa za Utalii Ukanda wa
Kusini mwa Tanzania, huku Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii Meja
Jenerali Gaudence Milanzi (wa pili kulia waliosimama-tai nyekundu)
akishuhudia, katika Ukumbi wa Wizara ya Fedha na Mipango Jijini Dar es
Salaam.
Katibu
Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. Doto James (wa pili kulia) na
Mwakilishi Mkazi wa Benki ya Dunia katika nchi za Tanzania, Malawi,
Burundi na Msumbuji, Bi Bella Bird, wakisaini Mkataba wa Mkopo wenye
masharti nafuu wa Sh. Dola za Marekani milioni 150 sawa na Shilingi
bilioni 340 kwa ajili ya Mradi wa kuibua fursa za Utalii Ukanda wa
Kusini mwa Tanzania, katika Ukumbi wa Wizara ya Fedha na Mipango Jijini
Dar es Salaam.
Mkurugenzi
Mkuu wa Shirika la Hifadhi za Taifa-TANAPA, Bw. Allan Kijazi na
Mwakilishi Mkazi wa Benki ya Dunia katika nchi za Tanzania, Malawi,
Burundi na Msumbuji, Bi Bella Bird, wakisaini Makubaliano ya utekelezaji
wa Mkataba wa Mradi wa kuibua fursa za Utalii Ukanda wa Kusini mwa
Tanzania utakao gharimu Shilingi bilioni 340 zilizotolewa kama mkopo
wenye masharti nafuu na Benki hiyo kwa Tanzania, Ofisi za Wizara ya
Fedha na Mipango, Jijini Dar es Salaam.

Fedha na Mipango, Jijini Dar es Salaam. Wanaoshuhudia nyuma ni Katibu
Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango Bw. Doto James, (wa pili kulia
waliosimama akifuatiwa na Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii Meja
Jenerali Gaudence Milanzi, Jijini Dar es Salaam.
Katibu
Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. Doto James (kulia) na Mwakilishi
Mkazi wa Benki ya Dunia katika nchi za Tanzania, Malawi, Msumbiji na
Burundi Bi. Bella Bird (kushoto) wakibadilishana Mkataba wa Mkopo wenye
masharti nafuu wa Sh. bilioni 340 kwa ajili ya Mradi wa kuibua fursa za
Utalii katika Ukanda wa Kusini mwa Tanzania, katika Ukumbi wa Wizara ya
Fedha na Mipango Jijini Dar es Salaam.

Burundi Bi. Bella Bird (kushoto) wakionesha Mkataba wa Mkopo wenye
masharti nafuu wa Sh. bilioni 340 kwa ajili ya Mradi wa kuibua fursa za
Utalii katika Ukanda wa Kusini mwa Tanzania, baada ya kusainiwa katika
Ukumbi wa Wizara ya Fedha na Mipango Jijini Dar es Salaam.
(Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini-Wizara ya Fedha na Mipango)
Benny Mwaipaja, Dar es Salaam
BENKI
ya Dunia imeipatia Tanzania Mkopo wenye masharti nafuu wa Dola za
Marekani milioni 150, sawa na takriban Shilingi bilioni 340 kwa ajili ya
kutekeleza mradi mkubwa wa kufungua fursa za utalii katika Ukanda wa
Kusini mwa Tanzania.
Mkataba
wa mkopo huo umetiwa saini Jijini Dar es Salaam kati ya Katibu Mkuu
Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. Doto James na Mwakilishi Mkazi wa Benki
ya Dunia anayehudumia nchi za Tanzania, Malawi, Msumbiji na Burundi, Bi.
Bella Bird.
Bw.
James alisema kuwa mkopo huo umelenga kuimarisha miundombinu ya utalii
katika ukanda huo wa kusini ikiwemo ujenzi wa barabara, viwanja vya
ndege, madaraja pamoja na kuibua fursa nyingi za utalii ili kuvutia
watalii wengi zaidi.
Alisema
pia kwamba mradi huo umelenga kuwajengea uwezo wananchi wanaozunguka
maeneo ya utalii kwa kuanzisha miradi itakayo chochea maendeleo yao ya
kijamii na kiuchumi pamoja na kuendeleza uhifadhi katika maeneo yao.
Aidha,
mkopo huo utatumika katika kampeni ya kutangaza vivutio vya utalii
vilivyoko katika ukanda huo ndani na nje ya mipaka ya Tanzania ili
kuvutia watalii wengi zaidi kutembelea maeneo hayo badala ya hali ilivyo
sasa ambapo watalii wengi wanatembelea vivutio vilivyoko ukanda wa
Kaskazini.
Mradi
huo utakaotekelezwa kwa kiasi kikubwa na Mamlaka ya Hifadhi za Taifa
Tanzania-TANAPA, utainufaisha zaidi Hifadhi ya Taifa ya Ruaha, Mikumi,
Udzungwa na Pori la Akiba na Selous.
Alisema
kuwa manufaa hayo yatalenga kujengwa viwanja vya ndege, barabara
hifadhini, utunzaji wa mazingira utakao uwezesha mto Ruaha Mkuu
kutiririsha maji muda wote katika Hifadhi ya Taifa ya Ruaha kupitia
uwanda wa Usangu.
“Mpango
wa kuibua fursa za utalii katika ukanda wa Kusini mwa Tanzania,
umelenga kuimarisha usafiri wa anga na nchi kavu ambapo uwanja mkubwa na
wa kisasa utajengwa mkoani Iringa pamoja na kuboresha barabara
inayotoka Iringa hadi Msembe yenye urefu wa kilometa 105” alisema Bw.
James
Aisema
kuwa hatua hiyo inatarajia kuongeza idadi ya watalii wa ndani na nje ya
nchi na kupunguza gharama za usafiri kutoka katika maeneo ya Zanzibar,
Dar es Salaam na Kilimanjaro hivyo kuongeza mapato ya Serikali.
Bw.
Doto James aliishukuru Benki ya Dunia kwa mkopo huo utakao changia kwa
kiasi kikubwa kukuza uchumi wa nchi na maendeleo ya wananchi wake
kupitia sekta ya utalii.
Kwa
upande wake Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii Meja Jenerali,
Gaudence Milanzi alisema kuwa mradi huo, utahusisha ujenzi wa viwanja
15 vya ndege, ujenzi wa kilometa 982 za barabara kwenye hifadhi, kununua
mitambo ya kukarabati barabara, kuimarisha reli ya TAZARA ili
kuwawezesha watalii kufika kwenye Pori la Akiba la Selous.
Aidha,
alisema kuwa wananchi wanaozunguka eneo la mradi watapatiwa mafunzo ya
namna ya kuongoza watalii, kutoa huduma kwenye hoteli na kuwajengea
uwezo wa kutengeneza bidhaa zinazohusiana na utalii ili wajiongezee
kipato.
Meja
Jenerali Milanzi alisema kuwa wanategemea mradi huo utaongeza idadi ya
watalii kutoka milioni moja hivi sasa hadi kufikia zaidi ya watalii
milioni 2 ifikapo mwaka 2020.
Akizunguza
wakati wa tukio hilo, Mwakilishi Mkazi wa Benki ya Dunia, hapa nchini
Bi. Bella Bird alisema kuwa mkopo huo ulioridhiwa na Bodi ya Wakurugenzi
wa Benki hiyo Jijini Washington DC Septemba 28, 2017, umelenga kukuza
uchumi wa Tanzania kupitia sekta hiyo ya utalii na kupunguzia umasikini
wananchi wake.
“Utalii
na uhifadhi vinakwenda pamoja na kwamba vitu hivyo viwili vitaisaidia
nchi kukua kiuchumi na kukuza ajira ya watu wake kwa kiwango kikubwa
hivyo kuondokana na umasikini ikichagizwa pia na kilimo” alisisitiza Bi.
Bella Bird.
Alisema
sekta ya utalii inakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo migogoro
ya watu na wanyama, ujangili, na ndiyo maana Benki ya Dunia imeamua
kuisaidia Serikali na taasisi zinazojihusha na kudhibiti changamoto hiyo
kwa kuzijengea uwezo wa kukabiliana nazo.
Bi.
Bird alisema kuwa mradi huo utakuja na suluhisho la changamoto ya
wananchi kuwa sehemu ya uhifadhi kwa kuwapa miradi ya maendeleo
itakayokuwa mbadala wa shughuli walizokuwa wakifanya kwenye maeneo ya
hifadhi ikiwemo kuanzisha utalii wa kiutamaduni, kilimo ili waendeleze
maisha yao.
EmoticonEmoticon