Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akishikana mkono na kupongezana
na Mwenyeji wake Rais wa Uganda Yoweri Kaguta Museveni mara baada ya
kuweka jiwe la msingi la ujenzi wa Bomba la Mafuta ghafi litakalo toka
Hoima nchini Uganda hadi eneo la Chongoleani mkoani Tanga. Sherehe za
uwekaji wa jiwe hilo zimefanyika katika eneo la Mutukula Wilayani
Kyotera nchini Uganda
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli na Mwenyeji wake Rais wa Uganda
Yoweri Kaguta Museveni wakisikiliza maelezo ya namna ya bomba hilo la
mafuta ghafi litakavyojengwa na kuanza kufanyakazi.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli na Mwenyeji wake Rais wa Uganda
Yoweri Kaguta wakijadiliana jambo mara baada ya kupewa maelezo ya mradi
huo mkubwa wa bomba la mafuta ghafi.
hilo la Ufunguzi la Ujenzi wa Bomba hilo la Mafuta ghafi
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli na Mwenyeji wake Rais wa Uganda
Yoweri Kaguta Museveni wakiondoka katika eneo la Mutukula mara baada ya
uwekaji wa jiwe la msingi la bomba la mafuta.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Mke wake Mama Janeth
Magufuli wakifurahia ngoma za asili za watoto wa Uganda mara baada ya
kuwasili nchini humo huku Rais wa Uganda Yoweri Musevini akitazama
watoto hao.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli pamoja na Rais wa Uganda Yoweri
Museveni wakizungumza na mamia ya wananchi hawaonekani pichani katika
eneo la Kyatera nchini Uganda mara baada ya ufunguzi wa Bomba la Mafuta.
PICHA NA IKULU
EmoticonEmoticon