Naibu Waziri Kazi, Vijana na Ajira (kushoto) Mh. Antony Mavunde (Mbunge), akimkabidhi mshindi wa 14 wa mchezo wa tatu Mzuka Bw. Robert A. Changadiko(45), hundi ya shilingi milioni sitini , Mjini Dodoma.
Mshindi wa droo ya 14 ya Tatu Mzuka Bw.Robert A. Changadiko (kulia)aliyejishindia donge nono la shilingi milioni sitini wiki hii, akiwa na rafiki yake bwana Bw. Daudi Mwangoto (katikati), ambaye alizawadiwa shilingi milioni moja kutoka katika promosheni ya cheza na washkaji shinda na washkaji ya Tatu Mzuka, kushoto ni Bw.Edwin Kawito ni mshindi wa Tatu Mzuka droo ya kumi (10) aliyejishindia shilingi milioni sitini.
Mshindi wa shilingi milioni sitini kutoka kijiji cha Msembata (Dodoma)Bw.Robert A. Changadiko mwenye umri wa maika 45, ambaye ni fundi minara,akifurahia ushindi wake.
Naibu Waziri wa Kazi, Vijana na Ajira Mheshimiwa Anthony Mavunde leo amemkabidhi kitita cha shilingi Milioni 60 mshindi wa droo ya Tatumzuka Bwana Robert Changadiko ambaye alijishindia kiasi hicho katika ‘Jackpot’ ya wiki hii katika droo ya kusisimua iliyoonyeshwa siku ya jumapili kupitia vituo vya runinga kote nchini.
Bwana Changadiko ambaye anafanya kazi kama fundi minara mjini Dodoma alielezea furaha yake juu ya ushindi huo ambao hakuutegemea na akaishukuru Tatumzuka kwa kutimiza hitaji lake la pesa wakati alipokuwa akizihitaji zaidi.
"Niliamua kucheza Tatu Mzuka kutokana na matatizo niliyokuwa nayo ya kifedha ambapo nilihitaji fedha za haraka ili kukidhi mahitaji hayo. Kwakweli nina furaha kubwa sana na nashukuru kwamba nilijaribu bahati na ikatimia” alisema.Mavunde alimpongeza mshindi kwa kushinda kiasi hicho na Tatu Mzuka kwa ajili ya kuendelea kutengeneza mamilionea na kubadilisha maisha ya watu.
"Ninakushauri kwamba kabla ya kuanza kutumia pesa yako,tenga muda kufikiri namna utakavyotumia fedha yako ili utimize malengo yako na ili pesa uliyojishindia ilete mabadiliko ya kweli katika maisha yako." Mheshimiwa Mavunde alishauri.Mheshimiwa. Mavunde alihitimisha kwa kusisitiza kwamba hizi pesa ambazo watu wanajishindia kupitia Tatumzuka ni fursa hasa kwa vijana kujitengenezea ajira na kubadilisha maisha ya wale walio karibu yao.
Afisa wa Mawasiliano wa Tatu Mzuka, Bi Patty Mtatiro alielezea kwamba Tatu Mzuka hadi sasa imetengeneza mamilionea 120 na kutoa zaidi ya shilingi bilioni 5.3. Akasema kwamba sio hivyo tu, tarehe 19 Novemba ambapo ni wiki mbili kutoka sasa Tatumzuka kupitia SUPA Mzuka Jackpot itatoa milioni 150 za uhakika kwa mshindi atakayejishindia.
" Kwa sasa unaweza kushinda kwa njia 3 kwa kucheza mara moja tu kwa shilingi 500. Tatu Mzuka inakupa nafasi ya kushinda hadi Tz 6, 000,000 masaa 24 kwa siku. Kila Tzs500 unayoitumia inakupa nafasi ya moja kwa moja kuingia kwenye Mzuka Jackpot ya kila wiki ambapo unaweza kushinda zaidi ya shilingi Milioni 60. Namna ya tatu ni kupitia droo ya Supa Mzuka Jackpot ambapo dau la uhakika la Milioni 150 litatolewa kwa mshindi. Hakuna dili kali zaidi ya hili "alisema Bibi Mtatiro.
EmoticonEmoticon