Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro amefungua mafunzo ya “Tathmini ya Uwezo” kanda ya Shinyanga ikiwa ni jitihada inayofanywa na shirika la Twaweza kwa lengo la kupima uwezo wa watoto juu ya umahiri wao wa kusoma,kuhesabu na kuandika.
Mafunzo hayo yanayofanyika kwa muda wa siku tatu katika ukumbi wa Karena Hotel Mjini Shinyanga,yameanza leo Alhamis Oktoba 5,2017.
Akizungumza wakati wa mafunzo hayo,Afisa Mawasiliano kutoka Jitihada ya Uwezo Twaweza,Greyson Mgoi akisema washiriki wa mafunzo hayo ni waratibu wa wilaya na waratibu wa vijiji kutoka wilaya nane za kanda ya Shinyanga inayojumuisha mikoa ya Dodoma,Singida,Simiyu na Shinyanga.
“Mafunzo ya tathmini ya Uwezo yanafanyika nchi nzima na kwa upande wa kanda ya Shinyanga,yanafanyika hapa ambapo tunafundisha mbinu na taratibu za kufanya wakati wa kutekeleza zoezi la Tathmini ya Uwezo kwenye wilaya mbalimbali nchini Tanzania na mwaka huu zoezi litafanyika katika wilaya 56”,alieleza Mgoi.
Alisema washiriki wa mafunzo hayo watafundishwa namna ya kufanya tathmini kuhusu uwezo wa watoto wenye kuanzia miaka 6 hadi 16 katika masomo matatu ya Kiingereza,Kiswahili na Hesabu.
Aliongeza kuwa Twaweza kupitia tathmini ya uwezo imekuwa ikishirikiana na serikali katika kuboresha elimu nchini.
Naye Mkurugenzi wa Shirika la OPE ambalo ni mdau wa Uwezo,William Shayo alisema lengo la msingi la Uwezo ni matokeo ya kujifunza kwa watoto na swali linaloulizwa kila siku ni “Je watoto wetu wanajifunza”.
“Tunatathmini uwezo ujuzi wa watoto katika kusoma na kuhesabu,lakini pia kusambaza matokeo ya utafiti sehemu kubwa kwa wananchi,wazazi,walimu na serikali hali hii inasababisha wananchi wachukue hatua za kuboresha ngazi za ujifunzaji za watoto kwenye jamii”,aliongeza.
Akifungua mafunzo hayo,Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro alisema serikali inatambua kazi nzuri zinazofanywa na taasisi katika kuboresha sekta ya elimu na kwamba serikali itaendelea kushirikiana nao.
Aidha Matiro aliwataka washiriki wa mafunzo hayo kutoa taarifa kwa serikali kuhusu mambo watakayoyabaini wakati wa tathmini yao ili kuisaidia serikali kuboresha elimu katika maeneo yenye changamoto.
“Mkimaliza kufanya tathmini mtuletee uhalisia,msituonee aibu kutuambia,tunahitaji kujua uhalisia wa mambo kwamba watoto kweli wanaelewa?wanajua kusoma? Hesabu wanazijua?,Mkileta tafiti zenu kwa uhalisia itakuwa rahisi kwa wadau mbalimbali ikiwemo serikali kupata ufumbuzi wa matatizo katika elimu kwa ajili ya kusaidia watoto”,aliongeza Matiro.
ANGALIA PICHA ZA MATUKIO HAPA CHINI
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro leo amefungua mafunzo ya “Tathmini ya Uwezo” kanda ya Shinyanga katika ukumbi wa Karena Hotel leo Alhamis Oktoba 5,2017-Picha na Kadama Malunde - Malunde1 blog
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro akizungumza wakati wa kufungua mafunzo hayo yatakayodumu kwa muda wa siku tatu.
Afisa Mawasiliano kutoka Jitihada ya Uwezo Twaweza,Greyson Mgoi akielezea kuhusu Tathmini ya Uwezo
Afisa Mawasiliano kutoka Jitihada ya Uwezo Twaweza,Greyson Mgoi akizungumza ukumbini.
Afisa Mawasiliano kutoka Jitihada ya Uwezo Twaweza,Greyson Mgoi akisisitiza jambo.
Mkurugenzi wa Shirika la OPE ambalo ni mdau wa Uwezo,William Shayo akizungumza wakati wa mafunzo hayo.
Washiriki wa mafunzo wakifuatilia kilichokuwa kinaendelea ukumbini.
Mkurugenzi wa Shirika la OPE,William Shayo akielezea namna shirika lake linavyoshirikiana na Twaweza kupitia zoezi la Tathmini ya Uwezo katika kuboresha elimu kwa watoto.
Washiriki wa mafunzo hayo wakifuatilia kilichokuwa kinaendelea ukumbini.
Mafunzo yanaendelea
Mafunzo yanaendelea.
Wadau wakiwa ukumbini.
Mwezeshaji katika mafunzo hayo Anandumi Ndosi akitoa mada wakati wa mafunzo hayo.
Mshiriki akinyoosha mkono ili aulize swali.
Washiriki wakifurahia jambo ukumbini.
Mwezeshaji katika mafunzo hayo Anandumi Ndosi akizungumza ukumbini.
Mafunzo yanaendelea.
Picha ya pamoja,washiriki wa mafunzo hayo na mkuu wa wilaya ya Shinyanga,Josephine Matiro.
Picha ya pamoja.
Picha zote na Kadama Malunde - Malunde1 blog
EmoticonEmoticon