Waziri
wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. January Makamba
akiwa katika kikao wa watumishi wa Ofisi ya Uratibu - Serikali ya Mapinduzi
Zanzibar. Waziri Makamba amepata wasaa wa kuzungumza na Menejimenti na
watumishi wa Ofisi hiyo leo jijini Dar es Salaam, Mtaa wa Luthuli.
Waziri
wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. January Makamba
hii leo amefanya ziara ya kikazi kutembelea Ofisi za Uratibu wa shughuli za
Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ) zilizopo Mtaa wa Luthuli Jijini Dar es
Salaam.
Katika
Ziara hiyo Mhe. Makamba amepata fursa ya kuongea na Menejimenti ya Ofisi hiyo
na kupata wasaa wa kubadilishana uzoefu na kuweka mikakati ya kuimarisha
ushirikiano zaidi baina yao.
Awali,
akimkaribisha Waziri Makamba, Mratibu Mkuu Bw. Issa Mlingoti amemshukuru Waziri
Makamba kwa kufika na kuahidi kuimarisha ushirikiano katika nyanja za Elimu,
ajira na fursa kwa pande zote za Muungano.
"Sisi
tumefarijika sana kwa ujio wako na tunategemea kuwa huu ni mwanzo na mwelekeo
mzuri wa kuzidi kuimarisha mashirikiano baina yetu ikiwa sisi ni waratibu wa
shughuli za Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar" Alisisitiza Bw.Mlingoti
Katika
ziara hiyo Waziri Makamba alipata fursa ya kuongea na wafanyakazi, kusikiliza
changamoto zinazowakabili na kuahidi kuzipatia ufumbuzi.
EmoticonEmoticon