MAMLAKA YA USIMAMIZI WA BANDARI TPA YAKAMATA BOTI ILIYOTUMIKA KUIBA MAFUTA BAHARINI

September 24, 2017
IMG_8616
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari-TPA, Mhandisi Deusdedit Kakoko (kulia) akitoa maelezo kwa Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb), kuhusu mafuta yanavyopakuliwa kutoka kwenye meli, alipotembelea bandarini hapo ili kupata maelezo kuhusu mchakato wa kupata mita mpya za kupimia mafuta (Flow Meters), Jijini Dar es salaam.
IMG_8658
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA), Mhandisi Deusdedit Kakoko (kushoto) akimuonesha Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) (kulia), namna maharamia wa mafuta walivyoharibu miundombinu ya bomba la mafuta baharini, baada ya kufanikiwa kukamata boti moja na vifaa vyake lililokuwa likitumiwa na wahalifu hao kuiba mafuta.
IMG_8685
Boti Jeupe lililonaswa na kikosi maalumu cha kuzuia uhalifu cha Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari (TPA) juzi wakati wahalifu wakijiandaa kutoboa bomba na kuiba mafuta kwenye kina kirefu cha Bahari ya Hindi. Wahalifu walifanikiwa kutokomea kusikojulikana baada ya kujitosa baharini, Dar es Salaam.
IMG_8689
Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango (Mb), akiwapongeza askari wa doria waliofanikisha kukamata boti moja pamoja na vifaa vyake muhimu ikiwemo injini baada ya kuwadhibiti maharamia waliotaka kutoboa bomba na kuiba mafuta katika Bandari ya Dar es Salaam.
IMG_8702
Mmoja wa maafisa wa TPA walioongoza zoezi la kupambana na wahalifu wanaoiba mafuta kwenye bomba la mafuta akionesha vilipuzi vilivyokamatwa vilivyokuwa vitumiwe na wahalifu waliokuwa wakijaribu kuiba mafuta kwenye bomba la mafuta katika Bandari ya Dar es Salaam.

IMG_8742
Kaimu Kamisha na Kodi za Ndani wa Mamlaka ya Mapato Tanzania Bw. Elijah Mwandumbya, akitoa maelezo kwa Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) (kulia), kuhusu hatua zilizochukuliwa kudhibiti upotevu wa mapato ya Serikali upande wa mafuta katika Bandari ya Dar es Salaam.
IMG_8778
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA), Mhandisi Deusdedit Kakoko, akitoa maelezo walipokuwa wakiagana na Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb)Katika ziara hiyo Waziri Mpango amepongeza juhudi mbalimbali zinazofanywa na Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania na Mamlaka ya Mpato katika kudhibiti ukwepaji kodi.
IMG_8693
Mmoja wa maafisa wa TPA walioongoza zoezi la kupambana na wahalifu wanaoiba mafuta kwenye bomba la mafuta akionesha vilipuzi vilivyokamatwa vilivyokuwa vitumiwe na wahalifu waliokuwa wakijaribu kuiba mafuta kwenye bomba la mafuta katika Bandari ya Dar es Salaam.
IMG_8771
Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) (mbele), akiwa ametoka kukagua mitambo ya kupitisha mafuta kutoka kwenye Meli ili kujihakikishia kama hakuna namna ya ubadhilifu au hujuma kwa mapato ambayo Serikali inatakiwa kuyapata.
IMG_8708
Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) (wa pili kulia)na Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA), Mhandisi Deusdedit Kakoko (kulia) na wengine, walipotembela Bandari ya Dar es Salaam, kitengo cha Mafuta, kukagua flow meters na tukio la kukamatwa kwa boti lililokuwa likitumika kuhujumu bomba la mafuta.
Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini-Wizara ya Fedha na Mipango

Share this

Related Posts

Previous
Next Post »