Mkuu wa Utawala wa Jeshi la Polisi
(DCP) Leonard Paulo (katikati), akiwa ameongozana na Naibu Kamishna wa
Polisi mstaafu (DCP) Venance Tossi (Kushoto) na Mkuu wa chuo cha Polisi
Kidatu kilichopo mkoani Morogoro, kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP)
Zarau Mpangule, wakati alipowasili katika chuo hicho kwa ajili ya
kufunga mafunzo ya Utayari ya kuwajengea uwezo askari wakati
wanapotekeleza majukumu yao.
Naibu Kamishna wa Polisi mstaafu
(DCP) Venance Tossi (Kushoto), akizungumza jambo na Mkuu wa Utawala wa
Jeshi la Polisi (DCP) Leonard Paulo (katikati), muda mfupi kabla ya
kufunga mafunzo ya Utayari ya kuwajengea uwezo askari wakati
wanapotekeleza majukumu yao ya kazi za Polisi.
Mkuu wa Utawala wa Jeshi la Polisi
(DCP) Leonard Paulo, akifanya mazoezi ya viungo na baadhi ya askari
wanaoshiriki Mafunzo ya Utayari na kujengewa uwezo wakati wanapotekeleza
majukumu yao ya kazi za Polisi, mafunzo yanayofanyika katika Chuo cha
Polisi Kidatu Kilichopo mkoani Morogoro.
Picha na Jeshi la Polisi
EmoticonEmoticon