Na Woinde Shizza wa libeneke la kaskazini blog
WAKAGUZI
wa
ndani Nchini wamewataka wakurugenzi wa taasisi za umma na sekta binafsi
kuzifanyia kazi taarifa zao za kiukaguzi na kuacha kuzikalia pindi
wanapokabidhiwa jambo ambalo linasababisha kupotea kwa ufanisi
wa utendaji kazi kwa sekta hizo.
Kauli hiyo
imetolewa jijini Arusha na mkaguzi mkuu wa ndani wa serikali,Mohamedi
Ntonga katika mkutano mkuu wa mwaka wa wakaguzi wa ndani unaowajumuisha
wakaguzi kutoka sekta ya umma na binafsi
wakiwemo kutoka nje ya nchi.
Ntonga alisema
kuwa wakaguzi wa ndani wana umuhimu mkubwa katika maendeleo ya Taifa lolote
Duniani hivyo taarifa za kiukaguzi wanapozikabidhi zinapaswa kufanyiwa kazi
kwani zinakuwa zimefanyika kitaalamu,hivyo kitendo cha kuzikalia taarifa hizo
kinachofanywa na baadhi ya wakurugenzi wa Taasisi husika kinapelekea kupunguza
weledi katika utendaji kazi wao.
Alisema kuwa
Mkutano huo ni muhimu sana kwa wakaguzi wa ndani katika kubadilishana uzoefu wa
taaluma na kukumbushana yale yaliyo muhimu kwa mujibu wa taaluma yao hivyo
akiwasihi watanzanzia kuta mbua umuhimu wa kuwatumia wakaguzi wa ndani katika
masuala ya uwazi na uwajibikaji.
Aidha
akizungumzia faida za wakaguzi wa ndani kuwa wameweza kuibua wafanyakazi hewa,Mishahara
hewa ,watumishi wasio kuwa na taaluma,na upotevu wa fedha unaofanyika kwenye
taasisi mbalimbali zikiwemo Wizara, na Halmashauri za Serikali .
Kwa upande
wake Rais wa Wakaguzi wa Ndani Tanzania Richard Magongo amesema wakaguzi wa
ndani wamekuwa wakitumika kuchochea mabadiliko ya utendaji kazi ili kukabiliana
na wizi wa kimtandao ambao umekuwa ukitumika kutokana na kuongezeka kwa
Technolojia Duniani.
Magongo
aliongeza kuwa mkutano huo utajikita
kuangalia jinsi gani ya kuzitumia taaluma za wakaguzi ili kuenenda sambamba na
mabadiliko ya Technolojia yanayosababisha kuongezeka kwa wizi wa kimtandao .
Akizungumzia changamoto zinazo wakabili wakaguzi wa ndani ni
pamoja na kufukuzwa kazi pindi wanapokuwa wamekamilisha taarifa za kiukaguzi
zinazoonyesha kugusa maslahi ya baadhi ya watendaji jambo linalowapelekea
baadhi yao kuingiwa na uwoga na kushindwa kutekeleza majukumu yao ipasavyo.
EmoticonEmoticon