RC MASENZA: MARUFUKU WENYEVITI WA MITAA NA VIJIJI KUJIHUSISHA NA UUZAJI WA ARDHI

September 10, 2017
Mkuu wa mkoa wa Iringa Amina Masenza akizungumza na wadau mbalimbali wa wilaya ya mufindi wakati wa kutambulisha mpango kabambe wa halmashauri ya mji wa Mafinga uliokuwa na lengo la kuonyesha dira ya miaka ya hamsini (50) ya maendeleo ya mji wa Mafinga ambapo inasemeka ni moja kati ya miji inayokuwa kwa kasi .
 hawa ni baadhi ya wadau waliojitokeza katika ukumbu wa chama cha mapinduzi (CCM) wilaya ya mufindi kushuhudia utambulisho wa mpango kabambe wa halmashauri ya mji wa mafinga.

Na Fredy Mgunda, Iringa

Mkuu wa mkoa wa Iringa Amina Masenza ametaka wenyeviti wa vijiji  au wa mitaa kutojihusisha na uuzaji wa ardhi ili kuondoa migogoro ambayo imekuwa ikisababishwa na viongozi hao.

Akizungumza wakati wa utambulisho wa mpango kabambe wa halmashauri ya mji wa Mafinga, Masenza alisema kuwa kumekuwa na migogoro ambayo inasababishwa na wenyeviti wa serkali za vijiji au mtaa hivyo ni marufuku viongozi hao kujihusisha na swala hilo.

“Sipendi kusikia mwenyekiti wa mtaa au mwenyekiti wa kijiji akihusisha kuwa shahidi wa uuzwaji wa ardhi kwa kuwa hilo sio jukumu lao waichie mamlaka ya ardhi kufanya kazi kwa utaalamu wao”alisema Masenza

Aidha Masenza alimtaka wakurugenzi wote wa mkoa wa iringa kuwaambia ukweli viongozi juu ya sheria ya uuzaji wa ardhi ili kuondoa migogoro inayosababisha maumivu kwa upande unaonewa na kudhurumiwa haki yao ya msingi na kusababisha kumrudisha nyuma kimaendeleo.

“Wakurugenzi waambieni vijana wetu waache ujanja ujanja wa kupokea,kuchora,kuonyesha na kuelekeza swala lolote linalohusu uuzwaji wa ardhi ili hii mipango kabambe ya halmashuri ziende vizuri kama serikali inavyopanga”alisema Masenza

Masenza alisema kuwa acheni kufanya kazi kwa ujanja ujanja maana serikali ya uwamu ya tano chini ya uongozi wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr John Pombe maguli haitaki wananchi na viongozi kuishi kwa mazoea.

Sixbet Kayombo ni mwenyekiti wa serikali ya mtaa wa Balali katika halmashauri ya mji wa Mafinga alisema kuwa tamko la mkuu wa mkoa lianukweli ndani yake kwa kuwa kuna wenyeviti wengi wamekuwa wakisababisha migogoro isiyokuwa na maana kwa uroho wa kupokea pesa.

“Lakini ukiangalia kwa undani utagundua kuwa haiwezekani wananchi kuuza ardhi bila kuwepo ushaidi wa serikali ya mtaa hivyo tunamuomba mkuu wa mkoa kutafuta njia mbadala ili mwananchi asiwe na ukakasi wowte wakati wa uuzaji wa ardhi yake” alisema Kayombo

Naye mwenyekiti wa mtaa wa Amani kata ya Upendo Merikioni Ndelwa  alisema kuwa tatizo hilo limekuwa kubwa hasa vijijini kwa kuwa viongozi wengi bado hawana elimu ya mwisho wa madaraka yaho hivyo tunamuomba mkuu wa mkao kutoka elimu wa wenyeviti ili kuepusha migogoro ya ardhi.

Share this

Related Posts

Previous
Next Post »