Na Khadija Khamis –Maelezo
Jamii
inatakiwa kuweka utaratibu wa kupima afya ikiwemo afya ya kinywa na meno
ili kupatiwa uchunguzi wa awali pamoja na elimu sahihi ya afya angalau
mara mbili kwa mwaka .
Hayo
aliyaeleza na Mkurugenzi wa Kinga na Elimu ya Afya Dr Fadhil Mo’hd
Abdalla huko katika Kituo cha Afya Rahaleo, wakati akifungua zoezi la
uchunguzi wa afya ya kinywa na meno linaloendeshwa na Chama cha
Madaktari wa Kinywa na Meno kutoka Tanzania .
Alisema
afya hiyo ni muhimu kufanyika awali kabla ya madhara, kwa kupatiwa
ushauri wa mapema kabla ya athari kujitokeza na kusababishwa kupoteza
meno .Alifahamisha
kuwa katika miaka ya nyuma elimu ya afya ya kinywa na meno zilikuwa
zikitolewa katika maskuli ,wataalamu hutoa elimu kwa wanafunzi pamoja na
kung’oa meno kwa wale ambao meno yao yameadhirika .
Aidha
alisema mpango huo wa uimarishaji afya ya jamii iko haja kurejea
utaratibu wa kizamani , wataalamu wa afya ya kinywa na meno kutoa huduma
za matibabu katika maeneo mbali mbali ikiwemo maeneo ya maskuli na
vijijini .
“Huu
usiwe mwanzo wa kuonyesha njia kwa jamii na wala msisubiri kuumwa kila
muda mujiwekee utaratibu wa kujichunguza afya zenu ikiwemo afya ya
kinywa na meno pamoja na maradhi yasioambukiza ili muweze kupata ushauri
mapema kwa Madaktari ,”alisema Mkurugenzi Kinga.
Alieleza
kutoa elimu na uchunguzi wa afya kwa jamii itasaidia kupunguza gharama
za matibabu na kuimarisha kinga ya awali na kujiepusha na matumizi ya
vyakula ambavyo vinachangia kuleta madhara ikiwemo vyakula vya sukari
kuchangia uozeshaji wa meno hasa kwa watoto .
Nae
Mwenyekiti wa Chama cha Madaktari wa Afya ya Kinywa na Meno ( TBA) Dr
Lorna Carneiro alisema mara hii wamepata fursa ya kuja Zanzibar kwa
kufanya uchunguzi wa afya ya kinywa na meno ili kujua wale wagonjwa
ambao wanamatatizo na kuwapatia tiba pamoja na kuwapa elimu ya afya .
Alisema
Chama hicho kinahimiza umuhimu wa afya bora kwa jamii na kutoa ushauri
wa maradhi mbalimbali ikiwemo ukimwi ,saratani ,Kifua kikuu,afya ya
kinywa na meno pamoja na maradhi yasioambukiza kwa kuifanya jamii ipate
uelewa na kujikinga na maradhi ambayo yanauwezo wa kuepukika .
“Hali
ya idadi ya Wagonjwa ni kubwa wakati ya kuwa magonjwa haya yanakingika
kwa haraka na kupona lakini kikwazo ni kuwa na uchache wa madaktari
,“alisema Dr Lorna .
Alifahamisha
kila ifikapo tarehe 20 machi ya kila mwaka huadhimisha siku ya afya ya
kinywa na meno kwa mwaka ujao wanatarajia uzinduzi wa zoezi hilo
litafanyika Zanzibar .
Nae
Mgonjwa BI Nargisi Uzia ambae alifika kupatiwa huduma ya matibabu katika
kituo hicho alisema anaishukuru Serikali kwa kuwaletea wataalamu wa
kuchunguza afya zao lakini pia iko haja ya zoezi hilo liwe endelevu
kwani matatizo yako mengi yanahitaji uchunguzi.
Rais
wa Chama cha Madaktari wa Kinywa na Meno Tanzania Dokt,Lorna Carneiro
kulia akitoa hotuba ya makaribisho katikaUfunguzi wa Zoezi la Uchunguzi
wa Maradhi ya kinywa na Meno katika Kituo cha Afya Rahaleo Mjini Unguja.
Mkurugenzi
wa Kinga na Elimu ya Afya katika Hospitali ya Mnazi mmoja Dkt,Fadhil
Abdalla akitoa hotuba ya Ufunguzi wa Zoezi la Uchunguzi wa Maradhi ya
Kinywa na Meno katika Kituo cha Afya Rahaleo Mjini Unguja.Zoezi
linalofanywa na Chama cha madaktari wa Kinywa na Meno
Tanzania(TDA).wakishirikiana na madaktari wa Zanzibar.
Mkurugenzi
wa Kinga na Elimu ya Afya katika Hospitali ya Mnazi mmoja Dkt,Fadhil
Abdalla katikati akiwa katika picha ya pamoja na Madaktari kutoka Chama
cha madaktari wa Kinywa na Meno Tanzania(TDA).pamoja na madaktari wa
Zanzibar katika Zoezi la Uchunguzi wa Maradhi ya Kinywa na Meno katika
Kituo cha Afya Rahaleo Mjini Unguja.
Daktari
wa Kinywa na Meno kutoka Hospitali ya Taifa Muhimbili Dkt,Ismail Amour
akitoa Elimu ya kujikinga na maradhi hayo katika Ufunguzi wa Zoezi la
Uchunguzi wa Maradhi ya Kinywa na Meno katika Kituo cha Afya Rahaleo
Mjini Unguja.Zoezi linalofanywa na Chama cha madaktari wa Kinywa na Meno
Tanzania(TDA).wakishirikiana na madaktari wa Zanzibar.
Rais
wa Chama cha Madaktari wa Kinywa na Meno Tanzania Dokt,Lorna Carneiro
kushoto akifanya mahojiano na Muandishi wa Habari kutoka ITV Farouk
Kariym pamoja na muandishi wa Habari Maelezo Zanzibar Khadija Khamis
katika Ufunguzi wa Zoezi la Uchunguzi wa Maradhi ya Kinywa na Meno
katika Kituo cha Afya Rahaleo Mjini Unguja.Zoezi linalofanywa na Chama
cha madaktari wa Kinywa na Meno Tanzania(TDA).wakishirikiana na
madaktari wa Zanzibar.
Daktari
wa Kinywa na Meno kutoka Haspitali ya Arrahma Zanzibar akimfanyia
Uchunguzi wa mardhi ya Kinywa na Meno Kauthar Vuai mkaazi wa meli nne,
katika Zoezi la Uchunguzi wa Maradhi ya Kinywa na Meno katika Kituo cha
Afya Rahaleo Mjini Unguja.Zoezi linalofanywa na Chama cha madaktari wa
Kinywa na Meno Tanzania(TDA).wakishirikiana na madaktari wa Zanzibar.PICHA NA YUSSUF SIMAI/MAELEZO ZANZIBAR.
EmoticonEmoticon