MBUNGE AITAKA TBS KUWAFIKIA WAJASIRIAMALI WADOGO WADOGO

September 07, 2017
Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Tanga  kupitia (Chadema), Yosepher Komba akizungumza wakati akifungua semina kwa vikundi vya wajasiriamali wilayani Muheza inayofanyika kwa wiki nzima ambayo aliiandaa lengo kubwa likiwa kuwawezesha kuzitengenezea ubora bidhaa
zao wanazozalisha.



Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Tanga  kupitia (Chadema), Yosepher Komba katikati akifuatilia kwa umakioni mafunzo hayo
Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Tanga  kupitia (Chadema), Yosepher Komba wa kwanza kulia akifuatilia kwa umakini semina hiyo
Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Tanga  kupitia (Chadema), Yosepher Komba akifuatilia namna ya utengenezaji wa sabuni za maji kushoto ni Katibu wake
Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Tanga  kupitia (Chadema), Yosepher Komba kulia akiangalia namna sabuni ya maji inavyotengenezwa wakati wa semina hiyo
Baadhi wataalamu wakichanganya sabuni ya maji
Wajariamali wilayani Muheza wakifuatilia semina hiyo iliyoandaliwa na Mbunge huyo
SHIRIKA la Viwango Tanzania (TBS) limetakiwa kuweka utaratibu mzuri wa kuwafikia wajasiriamali wadogo wadogo nchini kwa kufungua ofisi zao kwenye ngazi za wilaya na mikoa ili kuwasaidia kuepukana na hasara wanazoipata kutokana na bidhaa zao kutokukidhi viwango.

Uwepo wao katika maeneo hayo utasaidia wajasiriamali hao kuweza
  kutengeneza bidhaa bora ambazo zitawawezesha kuweza kuingia kwenye soko la ushindani ili kupata mafanikio.

Ushauri huo ulitolewa  na Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Tanga
  kupitia (Chadema), Yosepher Komba  wakati akifungua semina kwa vikundi vya wajasiriamali wilayani Muheza inayofanyika kwa wiki nzima ambayo aliiandaa lengo kubwa likiwa kuwawezesha kuzitengenezea ubora bidhaa
zao wanazozalisha.

Alisema mara nyingi wajasiriamali wamekuwa wakikumbana na changamoto
  ya bidhaa zao kuambiwa hazijakidhi viwango hivyo iwapo TBS watashuka chini kwa wananchi hususani wajasiriamali itasaidia kuondokana na adha za namna hiyo.

“Ukiangalia wajasiriamali hasa wa maeneo ya vijijini wamekuwa

wakikumbana na changamoto nyingi hasa mara baada ya kuzalisha bidhaa zao au kuzitengeneza wanapokuwa wakizipelekea sokoni wanaambiwa hazina ubora hivyo TBS tumieni nafasi hiyo kuwafikia wananchi hao “Alisema

Aidha pia aliwataka wajasiriamali kuhakikisha wanapozitengeneza bidhaa
  zao ni lazima kuzipeleka kwenye shirika la viwango ili kuweza kupimwa ubora zilizonazo badala ya kuziingiza sokoni.

“Lakini kwa watengenezaji wa sabuni za maji msije mkatafuta soko kwa
  kuchukua maji mengi kuweka wakati wa uzalishaji wake hivyo ni kuharibu ubora wa bidhaa yako badala yake muweni wabunifu “Alisema.

Akiwa akizungumza mmoja wa washiriki wa semina hiyo, Gerald Nyaisa
  ambaye ni mkulima wa mbogamboga wilayani Muheza alisema wataumia mafunzo hayo ili kuweza kuongeza thamani ya bidhaa zao wanazozalisha .

Alisema umuhimu wa semina hiyo hasa kwa wajasiriamali ni muhimu
  kutokana na uwepo wa sera ya Tanzania ya Viwanda ambayo inawagusa wakulima kwa asilimia kubwa katika harakati za kukuza uchumi.

“Lakini pia nitoe wito kwa vijana waweze kujikita kwenye kilimo na
  ujasiriamali badala ya kuendelea kukaa vijiweni ambako wanapoteza muda mwingi ambao wangeweza kuutumia katika uzalishaji “Alisema.

Mafunzo hayo yalihusisha vikundi nane vya wajasiriamali kutokana
  maeneo mbalimbali wilayani humo ambavyo ni Muinuano Group,Wamama Wajasiriamali,New Muheza Investment, Bodaboda,Uvumilivu, Harakati Vicoba
Group Mshikamano Juu na Kikundi kipya cha genge Mzee.

Share this

Related Posts

Previous
Next Post »