Mwenyekiti wa Bodi ya TGNP, Vicensia Shule ( wa pili kushoto) akimpongeza Makamu wa Rais Tanzania, Bi. Samia Suluhu (kulia) kwenye Tamasha la Jinsia kwa mwaka 2017 katika viwanja vya TGNP Mabibo jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa TGNP, Bi. Lilian Liundi akipongeza.
Burudani kutoka kwa msanii Misoji Mkwabi (wa kwanza kushoto) kwenye Tamasha la Jinsia kwa mwaka 2017 katika viwanja vya TGNP Mabibo jijini Dar es Salaam.[/caption]
MTANDAO wa Jinsia Tanzania (TGNP) imetoa tuzo, kuzitambua na kuzipongeza halmashauri za wilaya ya Kishapu na Kisarawe baada ya kutenga sehemu ya bajeti zao kwa ajili ya kujali huduma za wanawake na watoto.
Halmashauri ya Kishapu tayari imetenga shilingi milioni 279.5 katika mwaka wa fedha 2017/18 kwa ajili ya ujenzi wa vyumba maalumu 33 vinavyotumiwa na wasichana shuleni kwa ajili ya kujistili wawapo katika siku zao.
Kwa upande wa Halmashauri ya Kisarawe imepewa tuzo kwa ajili ya kufanikiwa kuwawezesha wanawake katika wilaya hiyo, ambapo imetenga asilimia 5 ya mapato yao na kuzitumia katika kuwawezesha akinamama.
Tuzo za halmashauri hizo mbili zimekabidhiwa leo jijini Dar es Salaam na Makamu wa Rais wa Tanzania, Bi. Samia Suluhu alipokuwa akizinduwa rasmi Tamasha la Jinsia kwa mwaka 2017 katika viwanja vya TGNP Mabibo jijini Dar es Salaam.
Ofisi ya Ofisa Elimu Msingi wilayani Kishapu, inakiri kuwepo na changamoto ya watoto wa kike kukosa maeneo ya kujisitili wawapo shuleni na kuingia katika siku zao. Halmashauri ya Kishapu imeanza kuchukua hatua kwa kujenga vyumba maalumu shuleni kwa kushirikisha nguvu za wananchi ili kuweza kuwasaidia watoto wa kike.
Taarifa kutoka Kituo cha taarifa na maarifa Kata ya Songwa, zinaeleza kuwa wanafunzi wa kike katika shule za msingi na sekondari wilayani Kishapu hupoteza siku 40 za masomo kwa kila mwaka kutokana na shule nyingi wilayani humo kutokuwa na vyumba maalumu vya kujihifadhi pale wanapokuwa katika siku zao.
Makamu wa Rais Tanzania, Bi. Samia Suluhu akitembelea miradi ya akinamama.
Deo Temba (kushoto) akizungumza jambo na mmoja wa wanachama waanzilishi wa TGNP, Bi. Marjorie Mbilinyi (kulia) na mmoja wa waalikwa katika Tamasha la Jinsia Tanzania Mwaka 2017.
Makamu wa Rais Tanzania, Bi. Samia Suluhu (kulia) akiteta jambo na Mama Getrude Mongela.
Baadhi ya washiriki wa Tamasha la Jinsia Tanzania Mwaka 2017 wakifurahiya jambo na Makamu wa Rais Tanzania, Bi. Samia Suluhu mara baada ya kuzinduwa tamasha hilo.___________________________________________________________________________________
Joachim Mushi, Mwenyekiti wa Tanzania Bloggers Network (TBN) na Mhariri Mkuu wa Thehabari.com.
Mail address:- mushi@thehabari.com/ jomushi79@yahoo.com/ info@thehabari.com
Mobile:- 0717 030066 / 0756 469470
Web:- www.thehabari.com
http://joemushi.blogspot.com
EmoticonEmoticon