Mkuu wa
Wilaya Kibaha, Assumpter Mshama akizungumza katika mkutano wa wadau wa
huduma za afya hususani ukimwi, uliofanyika mjini Bagamoyo ulioandaliwa
shirika lisilo la kiserikali la Tanzania Health Promotion Suppot (THPS).
Mkuu wa Wilaya Kibaha Assumpter Mshama alimwakilisha mkuu wa mkoa wa
Pwani, Evarist Ndikilo.
Mkuu wa
Wilaya ya Bagamoyo, Maggid Mwanga akizungumza jambo katika mkutano wa
wadau wa huduma za afya hususani ukimwi, uliofanyika mjini Bagamoyo
ulioandaliwa shirika lisilo la kiserikali la Tanzania Health Promotion
Suppot (THPS).
Mkurugenzi
wa THPS Dk. Mbatia akimkabidhi zawadi Mkuu wa Wilaya ya Kibaha
Assumpter Mshama aliyekuwa mgeni rasmi kwenye mkutano huo na
kumwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Everist Ndikilo
Mkuu wa
Wilaya ya Kibaha Assumpter Mshama akimkabidhi zawadi Dk. Beatrice (RMO
PWANI) iliyotolewa na wafanyakazi wa THPC kutokana na mchango wake
katika mkutano wa wadau wa huduma za afya hususani ukimwi, uliofanyika
mjini Bagamoyo ulioandaliwa shirika lisilo la kiserikali la Tanzania
Health Promotion Suppot (THPS).
Mgeni
rasmi wa hafla hiyo Mkuu wa Wilaya ya Kibaha, Assumpter Mshama
akimkabidhi zawadi pamoja na cheti Batuli Mituro ya Muuguzi bora kutoka
kituo cha Ikwiriri HC katika mkutano wa wadau wa huduma za afya hususani
ukimwi, uliofanyika mjini Bagamoyo ulioandaliwa shirika lisilo la
kiserikali la Tanzania Health Promotion Suppot (THPS).
Mgeni
rasmi Mkuu wa Wilaya ya Kibaha, Assumpter Mshama akipatiwa maelezo juu
ya upimaji wa saratani ya mlango wa kizazi kwa kina kutoka kwa mtaalamu
wa THPS.
Mgeni
rasmi Assumpter Mshama akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wakuu
wa wilaya wenzake wa mkoa wa Pwani pamoja na baadhi ya wafanyakazi wa
THPS
Baadhi ya wakuu wa wilaya wa Mkoa wa Pwani akibadilishana mawazo mara baada ya kumalizika kwa kutano huo
Wakurugenzi
wameagizwa kuhakikisha wanafuatilia watumishi wa afya waliojiriwa kwa
ufadhili wa mfuko wa dharura wa rais wa marekani ( PEPFAR) kupitia THPS
katika vituo mbalimbali mkoani Pwani wanalipwa mishahara yao kwa wakati.
Agizo
hilo limetolewa na Mkuu wa Wilaya ya Kibaha Assumpter Mshama alipokuwa
mgeni rasmi akimwakilisha mkuu wa mkoa wa Pwani Evarist Ndikilo, katika
mkutano wa wadau wa huduma za afya hususani ukimwi, uliofanyika mjini
Bagamoyo ulioandaliwa shirika lisilo la kiserikali la Tanzania Health
Promotion Suppot (THPS).
Mkuu wa
Wilaya ya Kibaha Assumpter Mshama alilipongeza shirika lisilo la
kiserikali la Tanzania Health Promotion Suppot (THPS) katika juhudi
wanazofanya katika sekta ya afya hususani mapambano dhidi ya ukimwi
mkoani humo na kuwataka watumishi wa afya kuhakikisha wana wanatoa
huduma ya vvu kila mahali katika vituo vya kutolea huduma za afya ,
mawodini, kliniki maalumu, kwenye mikusanyiko ya watu, na maeneo mengine
maalumu ili malengo ya serikali ya 90 ya tatu yatimie ifikapo mwaka
2020 .
Mshama
alisema serikali iliridhia maazimio ya shirika la umoja wa mataifa ya
kupambana na ukimwi ya tisini ya tatu ambapo alifafanua azimio hilo ni
ifikapo 2020 asilimia 90 ya watu wanaoishi na virusi vya ukimwi wawe
wanatambua hali zao za maambukizi, asilimia 90 ya hao wawe wanatumia
dawa na asilimia 90 ya walioko kwenye dawa wafubaze virusi kwa kiwango
kinachotakiwa cha kopi 1000 za virusi kwa milimita moja ya damu.
Mapema
akiongea katika mkutano huo Mkurugenzi Mtendaji wa THPS Dk. Redempta
Mbatia alisema shirika limekuwa likitoa huduma mbalimbali hususani
katika sekta ya afya katika mapambano dhidi ya vvu katika mradi wake kwa
kipindi cha miaka mitano Mkoani Pwani ikiwa ni pamoja nakuboresha
miundo mbinu ya vituo vya afya, kununua vifaa tiba, kutoa mafunzo
elekezi kwa watumishi pia kuhakikisha kila kituo kina dawa za kutosha.
“Tunatoza
ruzuku kwa mkoa wa Pwani zaidi ya shilingi million 700 kwa mwaka, fedha
hizi zinatakiwa zihudumie wananchi , zifanye mambo mbalimbali ikiwemo
kulipa mishahara baadhi ya watumishi wa afya walioajiriwa kwa ufadhili
wa PEPFA kupitia shirika letu, lakini pia tunatoa kiasi cha shilingi
10,000 kwa kila mtumishi atakayemgundua mteja wa VVU na kuhakikisha
anamshika mkono kwa mkono na kumwandikisha kwenye huduma na tiba”,
alisema Dk. Mbatia
Shirika
laTHPS linapata ufadhili wake kutoka mfuko wa Rais wa Marekani wa
kupambana na ukimwi (PEPFAR) na hapa nchini shirika hilo limekuwa
likiendesha miradi ya kutoa huduma za VVU katika mkoa wa Pwani, Mbeya,
Kigoma na Zanzibar.
EmoticonEmoticon