Kamati ya Uchaguzi ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF),
imetangaza majina manane ya wagombea ambao yamepita katika mchujo wa
awali kuwania nafasi mbalimbali katika Kamati ya Uongozi (Management
Committee) ya Bodi ya Ligi Kuu Tanzania Bara.
Waliopitishwa ni kuwania uenyekiti wa Management Committee ni Clement
Sanga na Ahmed Yahya wakati Shan Crysostoms ameiptishwa kuwania nafasi
ya makamu mwenyekiti.
Kwa mujibu wa kamati hiyo, Ramadhan Mahano na Hamisi Madaki
wamepitishwa kuwania nafasi ya Ujumbe wakitokea klabu za Ligi Kuu ya
Vodacom Tanzania Bara.
James Bwire na Almas Kasongo wamepitishwa kuwania Ujumbe wakitokea
klabu za Ligi Daraja la Kwanza. Brown Ernest hakupitishwa kwa sababu
hakuthibitishwa na klabu yake.
Edga Chubura amepitishwa kuwania ujumbe akitokea klabu za Ligi Ligi Daraja la Pili.
Wagombea kwa mujibu wa kanuni za uendeshaji wa Bodi ya Ligi Kuu ni
marais au wenyeviti wa klabu husika. Wagombea wanatakiwa kuwa wenyeviti
au Marais wa klabu husika.
Nafasi ya Mwenyekiti na Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya Ligi Kuu Tanzania inagombewa na klabu za Ligi Kuu pekee.
Uchaguzi huo wa kamati hiyo utafanyika Jumapili Oktoba 15, 2017
jijini Dar es Salaam na unaendeshwa kwa mujibu wa kanuni za Uchaguzi za
TFF toleo la 2013.
EmoticonEmoticon