Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), limetoa Ngao ya Jamii
mpya kwa ajili ya kuipa Simba ambayo ilifanikiwa kuishinda Young
Africans katika mchezo kuwania taji hilo uliofanyika Uwanja wa Taifa,
Dar es Salaam Agosti 23, mwka huu.
Siku hiyo mara baada ya mchezo ambao Simba ilishinda kwa mikwaju ya
penalti 5-4, TFF ilitoa Ngao ya Jamii ambayo ilikuwa na makosa ya
maandishi yaliyoonekana kwenye hivyo kuzua taharuki kwa wanafamilia wa
mpira wa miguu.
TFF iliomba radhi na kuahidi kutoa Ngao ya Jamii nyingine ambayo sasa
imetolewa leo Jumanne Agosti 29, mwaka huu na itakabidhiwa kwa Simba
kabla ya mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom dhidi ya Azam FC jijini Dar es
Salaam.
EmoticonEmoticon