Timu ya Mpira wa Miguu ya Tanzania ‘Taifa Stars’, imeanza kujifua leo asubuhi kwenye Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam.
Wachezaji wote kutoka klabu za Tanzania wamefika kadhalika baadhi
kutoka nje ya mipaka ya Tanzania kama vile Nahodha Mbwana Samatta na
Elias Maguli. Mazoezi hayo yataendelea kila siku hadi Ijumaa wiki hii.
Kikosi hicho kinachofanya mazoezi chini ya Kocha Mkuu, Salum Shabani
Mayanga kinajindaa kucheza na Botswana katika mchezo wa kirafiki wa
kimataifa chini ya utaratibu wa kalenda ya Shirikisho la Kimataifa la
Mpira wa Miguu (FIFA).
Wiki ya FIFA kwa mechi za kimataifa inatarajiwa kuanza Jumatatu
Agosti 28 hadi Septemba 5, mwaka huu ambako Tanzania imekubaliana
kucheza Botswana kwenye Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam Jumamosi ya
Septemba 2, 2017.
Katika kikosi hicho cha wachezaji 21, Kocha Mayanga amemwita upya
Mlinzi wa Young Africans, Kelvin Yondani huku nyota kutoka nje ya mipaka
ya Tanzania wakiwa ni saba.
Kikosi hicho kinachopiga kambi hoteli ya Sea Scape iliyoko Kunduchi,
Dar es Salaam kina makipa Aishi Manula (Simba SC), Mwadini Ally (Azam
FC) na Ramadhani Kabwili (Young Africans).
Walinzi ni Gadiel Michael (Young Africans), Boniphas Maganga (Mbao
FC), Abdi Banda (Baroka FC/Afrika Kusini), Kelvin Yondani (Young
Africans), Salim Mbonde (Simba SC) na Erasto Nyoni (Simba SC).
Viungo ni Himid Mao - Nahodha Msaidizi (Azam FC), Hamis Abdallah
(Sony Sugar/Kenya), Mzamiru Yassin (Simba SC), Said Ndemla (Simba SC),
Saimon Msuva (Difaa El Jadidah/Morocco), Shiza Kichuya (Simba SC), Farid
Mussa (CD Tenerif/Hispania) na Orgenes Mollel (FC Famalicao/Ureno).
Washambuliaji ni Raphael Daud (Young Africans), Kelvin Sabato (Azam
FC), Mbwana Samatta (KRC Genk/Ubelgiji) na Elias Maguli (Dhofar
FC/Oman).
Benchi la Ufundi la Mayanga linaundwa na yeye mwenyewe ambaye ni
Kocha Mkuu, Fulgence Novatus (Kocha Msaidizi), Patrick Mwangata (Kocha
wa Makipa), Danny Msangi (Meneja), Dkt. Richard Yomba (Daktari wa timu),
Dkt. Gilbert Kigadye (Daktari wa Viungo) na Ally Ruvu (Mtunza Vifaa).
EmoticonEmoticon