Mbunge wa viti maalumu kupitia chama cha mapinduzi mkoa wa Arusha Catherine Magige akimkabidhi mkurugenzi na watoto wa kituo cha kulelea watoto yatima cha Faraja orphance kilichopo jijini hapa,kituo hichi cha watoto yatima kina jumla ya watoto 200 na kati ya watoto hao watoto 30 wanaishi na maambukizi ya virusi vya ukimwi.
wa pili kushoto mbunge wa viti maalumu akiwa anateta jambo na katibu wa UWT mkoa wa Arusha Fatuma Hassan ,wakwanza kulia ni katibu wa kanda ya kaskazini msikiti wa Twariqatul ndugu Abdi Ramathani
mbunge wa viti maalumu akiwa anamkabidhi zawadi za iddi mkurugenzi wa kituo cha watoto yatima cha Samaritan villege Jospephat Mmnyi
mbunge wa viti maalum akiwa pamoja na baadhi ya watoto wa kituo cha watoto yatima na wasiojiweza cha Faraja ,mkurugenzi wa kituo hicho pamoja na baadhi ya viongozi wa chama cha mapinduzi mkoa wa Arusha
mbunge wa viti maalumu akiwa amembeba moja ya mtoto aliotelekezwa na mama yake akiwa mdogo anaeishi katika kituo cha watoto yatima cha Faraja kilichopo jijini hapa wakati alipowapelekea zawadi ya iddi
mbunge wa viti maalumu akimkabidhi msaada wa chakula mmoja wa kijana wa kito cha Zawiani wakati alipotembelea kutoa zawadi za sikukuu ya iddi
mbunge wa viti maalumu Catherine Magige akiwa anapewa maelezo mafupi katika maabusu ya watoto Arusha ,Ambapo aliaambiwa mahabusu hiyo inauwezo wa kubeba watoto 50 wakike wakiwa 10 na wakiume wakiwa 40 lakini kwa sasa ina jumla ya mahabusu 12 tu na wote wakiwa ni wanaume (picha na Woinde Shizza,Arusha )
Mbunge wa viti maalumu Catherine Magige akiwa anamkabidhi mbuzi ,mchele na mafuta kiongozi wa kituo cha mahabusu Arusha Mussa Mapunda ikiwa ni zawadi ya idi kwa watoto hao
vijana wa kituo cha Zawiani wakisala kabla ya msaada kutolewa wakiwa na mbunge wa viti maalumu pamoja na baadhi ya viongozi wa chama cha mapinduzi
Habari picha na Woinde shizza,Arusha
Mbunge wa Viti maalumu kupitia chama cha Mapinduzi (CCM) Catherine Magige leo amekabidhi msaada wa mbuzi watano ,chakula na mafuta kwa vituo vinne vya kulelea watoto yatima na wanaoishi katika mazingira magumu pamoja watoto wanoishi katika mahabusu ya watoto mkoani hapa ili kusherekea sikukuu ya idi .
Akikabidhi msaada huo kwa katika vituo hivyo alisema kuwa watoto hao wanapaswa kusherehekea sikukuuu ya iddi kama wengine wanaoishi na wazazi wao majumbani kwao .
Alisema kuwa vitu vyote hivyo alivyovigawa katika vituo vyote alivyo vitoa ametoa kwa moyo wake wote ,ambapo alisema kuwa yeye kama mama ameguswa na akaamua kwenda kuwapa watoto hawa msaada huo ili nao wakisherekea sikukuu hii wajisikie nao wapo na wazazi wao.
"napenda kuwasihi wananchi wajijengee tabia ya kusaidia watoto hawa yatima pia wajifunze kutembelea hata hawa watoto mahabusu ata kama awana watoto katika mahabusu hizi lakini wanaweza wakatoka na misaada na kuamua kupelekea watoto hawa yatima au hawa watoto walioko mahabusu kwani ni watoto na wanahaki ya kupendwa kama watoto wengine"alisema Magige
Alivitaja vituo ambavyo vimepewa msaada kuwa ni pamoja na Faraja ophas,Samaritan villege,kituo cha watoto yatima na wasio jiweza cha Zawiani pamoja na Mahabusu ya watoto Arusha
Wakati huohuo, Ofisa Msimamizi wa kito hicho , Mussa Mapua aliiomba Serikali
kujenga uzio katika mahabusu hiyo ili kuzuia watu wenye nia mbaya
kuingiza dawa za kulevya au wale watoto ambao ni wakorofi kutoroka.
Aidha alisema kuwa pia wanahitaji wanasheria wa watoto hao ili kesi zao zilizoko
mahakamani ziishe kwa muda mfupi, tofauti na hali ilivyo sasa huku akisema kuwa mahabusu hiyo kwa sasa inawatoto wa kiume 12 wote wakiwa ni wanaume
"unajua kesi zinachelewa kutokana na kukosekana kwa wanasherisa wa kuwatetea watoto hivyo tunaomba serikali ijitaidi kutuletea mwanasheria wa kutetea watoto hawapia napenda kutumia nafasi hii kuliomba Jeshi la Polisi kuwa makini katika upelelezi wa kesi
mbalimbali ikiwamo kuzingatia umri wa watoto ili kuepuka kuwapeleka
wakubwa katika mahabusi hiyo "alisema Mapua
EmoticonEmoticon