Waziri
wa Nchi Ofisi Waziri Mkuu Sera, Bunge,Kazi, Ajira,Vijana na wenye
Ulemavu, Mhe. Jenista Mhagama(kulia) akimkabidhi hundi ya shilingi
bilioni 1.5 zilizotolewa na NSSF kama mkopo kwa ajili ya upanuzi wa
kiwanda cha chaki Maswa, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya
Maswa, Dkt.Fredrick Sagamiko.
Na Stella Kalinga, Simiyu
Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) umekabidhi hundi ya shilingi bilioni 1.5 kwa
Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya ya Maswa Mkoani Simiyu, fedha ambazo ni mkopo
kwa ajili ya upanuzi wa kiwanda cha Chaki Wilayani humo na kuongeza uzalishaji.
Hundi hiyo imekabidhiwa kwa Waziri wa Nchi Ofisi Waziri Mkuu Sera, Bunge,Kazi, Ajira,Vijana na
wenye Ulemavu, Mhe. Jenista Mhagama kwa niaba ya Serikali na Mkurugenzi Mkuu wa NSSF
Prof.Godius Kahyarara wilayani Maswa mkoani Simiyu.
Akizungumza wakati wa makabidhiano ya hundi hiyo Mkurugenzi Mkuu wa NSSF Prof.Godius
Kahyarara amepongeza Mkoa wa Simiyu kwa kutekeleza Sera ya Ujenzi wa Uchumi wa Viwanda
kwa vitendo na kuwataka viongozi wa mkoa huo kutokatishwa tamaa.
Amesema NSSF kama Shirika la Umma linatekeleza sera na maelekezo ya Serikali na wametoa
mkopo huo kwa Halmashauri ya Wilaya ya Maswa ili wafanye upanuzi wa kiwanda cha chaki na
kuongeza uzalshaji kwa kuwa suala la Viwanda ni la kipaumbele.
Mkurugenzi
Mkuu wa NSSF Prof.Godius Kahyarara(kushoto) akimkabidhi Waziri wa Nchi
Ofisi Waziri Mkuu Sera, Bunge,Kazi, Ajira,Vijana na wenye Ulemavu, Mhe.
Jenista Mhagama hundi ya shilingi bilioni 1.5 zilizotolewa na NSSF kama
mkopo kwa ajili ya upanuzi wa kiwanda cha chaki Maswa, (kulia) Mkuu wa
Mkoa wa Simiyu, Mhe.Anthony Mtaka.
Waziri wa Nchi Ofisi Waziri Mkuu Sera, Bunge,Kazi, Ajira,Vijana na watu wenye Ulemavu, Mhe.
Jenista Mhagama amesema kiwanda cha Chaki Maswa kimebeba ujumbe na dhana ya Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe.Dkt. John Pombe Magufuli ya kushikamanisha Uchumi wa
Viwanda na Maendeleo ya watu kwa sababu kinatumia malighafi ya hapa nchini.
Aidha, amesema kiwanda hiki kitawanufaisha Watanzania hususani vijana wa Mkoa wa Simiyu
ambao watafanya kazi moja moja katika kiwanda na wale wataohusika katika uchimbaji wa
malighafi ambayo inapatikana maeneo mengine hapa nchini.
Waziri wa
Nchi Ofisi Waziri Mkuu Sera, Bunge,Kazi, Ajira,Vijana na wenye Ulemavu,
Mhe. Jenista Mhagama akipokea taarifa ya Upembuzi yakinifu wa panuzi wa
kiwanda cha chaki cha Maswa kutoka kwa mtalaam wa Taasisi ya Masuala ya
Kiuchumi na Kijamii(ESRF), Deodatus Sagamiko.
“Asilimia 56 ya nguvukazi hapa Tanzania ni vijana na vijana wengi bado hawana ajira lakini kiwanda
hiki kitasaidia, kwa kuwa sehemu ya hiyo asilimia 56 wataajiriwa katika kiwanda na wengine
watapata ajira huko mkoani Singida ambako malighafi ya kutengenezea chaki inapatikana” amesema.
Mhe.Mhagama ameongeza kuwa kiwanda kitatatua tatizo la upatikanaji wa chaki hapa
nchini,kitaokoa fedha kwa kuwa chaki zitauzwa kwa bei nafuu na kitaongeza mapato ya fedha za
kigeni kwa kuwa chaki zitakazozalishwa zitauzwa katika soko la nje ya nchi.
Naye Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Mhe.Anthony Mtaka amesema Halmashauri ya Wilaya ya Maswa
imeonesha mfano katika kutekeleza agizo la Rais wa Tanzania Mhe.Dkt.John Pombe Magufuli la
kubuni vyanzo vipya vya mapato kwa kujenga kiwanda hicho kikubwa, ambapo amesema kufikia
mwaka 2020 Halmashauri za Mkoa wa Simiyu zitakuwa mfano kwa kuwa na miradi yake zenyewe .
Mkuu wa
Mkoa wa Simiyu(wa tatu kushoto), viongozi wa Wilaya ya Maswa
wakimkabidhi Meneja wa Benki ya Azania( wa pili kulia)Hundizilizotolewa
na NSSF kwa ajili ya upanuzi wa kiwanda cha chaki wilayani humo ili
aendelee na taratibu za kibenki.
“Kama Halmashauri zinakopa mabilioni kujenga stendi, masoko kwa nini zisikope kujenga viwanda,
zikatumia malighafi ya hapa nchini zikaajiri Watanzania wakapata kipato na nchi yetu ikanufaika;
Halmashauri za Mkoa wa Simiyu zitaajiri na kwenye miaka mitano ya Mhe.Rais tutatoa mfano wa
kuwa Halmashauri zenye miradi yake” amesema.
Kwa upande wake Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ,
Mhe.Riziki Pembe Juma amesema Zanzibar ni wadau wakubwa wa Chaki zinazotengenezwa
Maswa(Maswa Chalks), hivyo ameomba ushirikiano ulioanzishwa kati ya Zanzibar na Simiyu
udumu ili kufikia malengo katika kukuza kiwango cha elimu na utekelezaji wa Sera ya Viwanda.
Kiwanda cha kutengeneza chaki Wilayani Maswa kwa sasa kinazalisha katoni zaidi ya 180 kwa siku
na chaki hizo zinatumika katika shule zilizopo katika maeneo tofauti hapa nchini, ikiwa ni pamoja na
mikoa yote za Zanzibar na baadhi ya mikoa ya Tanzania bara ikiwemo Simiyu, Mwanza, Shinyanga,
Geita na Tabora.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu,Mhe.Anthony Mtaka (kushoto) na Mkurugenzi Mkuu wa NSSF Prof. Godius
Kahyarara(kulia) wakiteta jambo wakati wa hafya ya makabidhiano ya hundi ya shilingi bilioni 1.5 zilizotolewa na
NSSF kama mkopo kwa ajili ya upanuzi wa kiwanda cha chaki Wilayani Maswa.
Waziri wa Nchi Ofisi Waziri Mkuu, Mhe.Jenista Mhagama(wa tatu kulia), Waziri wa Elimu na Mafunzo ya
Amali wa Serikali ya Mapinduzi (wa pili kulia) katika picha ya pamoja na viongozi wa Mkoa, wilaya ya Maswa na
Vijana wa Maswa Family wanaofanya kazi katika kiwanda cha chaki.
Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar , Mhe.Riziki Pembe Juma
akizungumza na viongozi wa Mkoa wa Simiyu wakati wa hafla ya makabidhiano ya Hundi ya shilingi bilioni 1.5
zilizotolewa na NSSF kama mkopo kwa ajili ya upanuzi wa kiwanda cha chaki Maswa.
Waziri wa Nchi Ofisi Waziri Mkuu Sera, Bunge,Kazi, Ajira,Vijana na wenye Ulemavu, Mhe. Jenista
Mhagama( wa pili kushoto) akiangalia kikundi cha ngoma mara mara baada ya kuwasilisi wilayani Maswa, kwa ajili ya
makabidhiano ya Hundi ya shilingi bilioni 1.5 zilizotolewa na NSSF kama mkopo kwa ajili ya upanuzi wa kiwanda cha
chaki Maswa.
Msanii Elizabeth Maliganya (kulia) na baadhi ya waimbaji wa Kwaya ya Kanisa la AICT Bariadi (wenye sare
za vitenge) wakicheza na viongozi mbalimbali mara baada ya makabidhiano ya hundi ya shilingi bilioni 1.5
zilizotolewa na NSSF kama mkopo kwa ajili ya upanuzi wa kiwanda cha chaki Maswa.
Waziri wa nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Jenista Mhagama(wa tano kulia), Waziri wa Elimu Zanzibar (mwenye
ushungi mwekundu), mkuu wa mkoa wa Simiyu, Mhe.Anthony Mtaka (wa sita kulia) wakiwa katika picha ya pamoja na
viongozi wa wilaya yaMaswa na wadau wengine wa maendeleo baada ya makabidhiaono ya Hundi ya shilingi bilioni 1.5
zilizotolewa na NSSF kama mkopo kwa ajili ya upanuzi wa kiwanda cha chaki Maswa.
Waziri wa nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Jenista Mhagama katika picha ya pamoja na viongozi wa mkoa na
wakuu wa idara wa Halmashauri ya Wilaya ya Maswa baada ya makabidhiaono ya Hundi ya shilingi bilioni 1.5
zilizotolewa na NSSF kama mkopo kwa ajili ya upanuzi wa kiwanda cha chaki Maswa.
Waziri wa Nchi Ofisi Waziri Mkuu Sera, Bunge,Kazi, Ajira,Vijana na wenye Ulemavu, Mhe. Jenista
Mhagama akisalimiana na Mbunge wa Maswa Mashariki, mhe.Stanslaus Nyongo mara baada ya kuwasili wilayani
Maswa, kwa ajili ya makabidhiano ya Hundi ya shilingi bilioni 1.5 zilizotolewa na NSSF kama mkopo kwa ajili ya
upanuzi wa kiwanda cha chaki Maswa.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe.Anthony Mtaka akitoa salamau za mkoa wakati wa hafla ya makabidhiano
ya Hundi ya shilingi bilioni 1.5 iliyotolewa na NSSF kama mkopo kwa ajili ya upanuzi wa kiwanda cha chaki Maswa.
Baadhi ya viongozi katika Mkoa wa Simiyu wakifuatilia masuala mbalimbali katika hafla ya makabidhiano
ya Hundi ya shilingi bilioni 1.5 zilizotolewa na NSSF kama mkopo kwa ajili ya upanuzi wa kiwanda cha chaki Maswa.
Baadhi ya viongozi katika Mkoa wa Simiyu wakifuatilia masuala mbalimbali katika hafla ya makabidhiano ya
Hundi ya shilingi bilioni 1.5 zilizotolewa na NSSF kama mkopo kwa ajili ya upanuzi wa kiwanda cha chaki Maswa.
Waziri wa Nchi Ofisi Waziri Mkuu Sera, Bunge,Kazi, Ajira,Vijana na wenye Ulemavu, Mhe. Jenista
Mhagama akisalimiana na Mkurugenzi Mkuu wa NSSF Prof. Godius Kahyarara(mara baada ya kuwasili wilayani
Maswa, kwa ajili ya makabidhiano ya Hundi ya shilingi bilioni 1.5 zilizotolewa na NSSF kama mkopo kwa ajili ya
upanuzi wa kiwanda cha chaki Maswa.
EmoticonEmoticon