Mama Samia Azindua Jumuiya ya Watoa Huduma za Mafuta na Gesi Tanzania (ATOGS)

June 24, 2017
unnamed
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan akipokea kitabu cha picha kutoka kwa Kamishna wa Utalii Zanzibar Javed Jafferji wakati wa hafla ya futari iliyoambatana na uzinduzi wa Jumuiya ya Watoa Huduma za Mafuta na Gesi Tanzania (ATOGS) jana Jijini Dar es Salaam.
1
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan akionyesha kitabu cha picha alichokabidhiwa na Kamishna wa Utalii Zanzibar Javed Jafferji (kulia) wakati wa hafla ya futari iliyoambatana na uzinduzi wa Jumuiya ya Watoa Huduma za Mafuta na Gesi Tanzania (ATOGS) jana Jijini Dar es Salaam.Kushoto ni Mwenyekiti wa Jumuiya hiyo ambaye pia alikuwa Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue.
2
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan akishuhudia  Kamishna wa Utalii Zanzibar Javed Jafferji alipokuwa akisaini katika kitabu cha picha alichomkabidhi Makamu wa Rais wakati wa hafla ya futari iliyoambatana na uzinduzi wa Jumuiya ya Watoa Huduma za Mafuta na Gesi Tanzania (ATOGS) jana Jijini Dar es Salaam.
3
Mwanzilishi wa Jumuiya ya Watoa Huduma za Mafuta na Gesi Tanzania (ATOGS), Bw. Abdulsamad Abdulrahim akitoa maelezo kuhusu malengo ya jumuiya hiyo mbele ya mgeni rasmi Makamu Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan, wakati wa hafla ya futari iliyoambatana na uzinduzi rasmi wa Jumuiya hiyo jana Jijini Dar es Salaam. Mwanzilishi huyo alitoa mchango wa shilingi milioni 25 kama mtaji wa kuanzia wa ATOGS.
4
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan akiomba dua wakati wa hafla ya futari iliyoandaliwa na Jumuiya ya Watoa Huduma za Mafuta na Gesi Tanzania (ATOGS) jana Jijini Dar es Salaam, Mwanzilishi wa Jumuiya ya Watoa Huduma za Mafuta na Gesi Tanzania (ATOGS).Kutoka kulia ni Waziri wa Viwanda na Biashara Charles Mwijage na Mwanzilishi wa Jumuiya hiyo Bw. Abdulsamad Abdulrahim.
5
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan akimsikiliza Mwenyekiti wa Jumuiya ya Watoa Huduma za Mafuta na Gesi Tanzania (ATOGS) ambaye pia ni Katibu Mkuu Kiongozi mstaafu Balozi Ombeni Sefue(kushoto) wakati wa hafla ya futari iliyoandaliwa na Jumuiya hiyo jana Jijini Dar es Salaam,kulia ni Mwanzilishi wa Jumuiya hiyo Bw. Abdulsamad Abdulrahim. Hafla hiyo iliambatana na uzinduzi rasmi wa Jumuiya hiyo ambayo lengo lake ni kushirikiana na Serikali katika kuwahamasisha wazawa kujihusisha na masuala ya gesi na mafuta ili kuongeza mnyororo wa katika sekta hiyo.
6
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa katika picha ya pamoja na wajumbe wa Jumuiya ya Watoa Huduma ya Mafuta na Gesi Tanzania (ATOGS) mara baada ya kumalizika kwa hafla ya futari iliyoambatana na uzinduzi wa Jumuiya hiyo jana Jijini Dar es Salaam. Lengo la Jumuiya hiyo ni kushirikiana na Serikali katika kuwahamasisha wazawa kujihusisha na masuala ya gesi na mafuta ili kuongeza mnyororo wa katika sekta hiyo.
Picha na: Frank Shija – MAELEZO

Share this

Related Posts

Previous
Next Post »