Mkurugenzi
Mkuu wa WCF, Bw. Masha Mshomba, akimkabidhi Dkt.Kezia, cheti cha
ushiriki wa mafunzo ya tathmini ya ajali na majeraha kwa mfanyakazi
aliyeumia wakati akitekeleza majukumu yake mahala pa kazi, wakati wa
kilele cha mafunzo ya siku tano kwa madaktari kutoka hospitali za umma
na binafsi za jijini Dar es Salaam. Jumla ya madaktari 70 kutoka
hospitali 35 walishiriki.
NA K-VIS BLOG/Khalfan Said
MAFUNZO
ya siku tano kwa madaktari yaliyoandaliwa na Mfuko wa Fidia kwa
Wafanyakazi, (WCF), ili kuwajengea uelewa wa namna ya kufanya tathmini
ya ugonjwa na ajali kwa mfanyakazi aliyepata madhara mahala pa kazi
yamemalizika kwa washiriki kutunukiwwa vyeti.
Mafunzo
hayo yaliyofunhga na Mkurugenzi Mkuu wa WCF, Bw. Masha Mshomba makao
makuu ya Mfuko huo, jingo la GEPF barabara ya Bagamoyo jijini Dar es
Salaam, Juni 23, 2017, yaliwaleta pamoja madaktari 70 kutoka hospitali
mbalimbali za umma na binafsi jijini Dar es Salaam.
Mafunzo
hayo yaliyogusa maeneo mbalimbali pia yaliwawezesha madaktari hao
kujifunza Muongozo mpya unaohusu namna ya kufanya tahmini kabla ya
kumlipa fidia stahiki Mfanyakazi aliepata madhara mahala pa kazi.
Akizungumza
kwenye ufungaji wa mafunzo hayo, Mkurugenzi Mkuu wa WCF, Bw Masha
Mshomba, alisema kuwa ni iani ya Mfuko kuwa Madaktari hao wamefaifika
na mafunzo hayo na yatawezesha ufanisi katika kjutoa huduma hizo kwa
wafanyakazi waliopata magonjwa au kuumia wakati wakiwa kazini.
Dkt.Benjamin
Najimu Mohammed, akizungumz kwa niaba ya madaktari wenzake. "Nia ya
mafunzo haya ni kwenda kuwasaidia watanzania wenzetu kwa niaba ya
wenzangu napenda kuushukuru Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi, kwa kutambua
umuhimu wa ushiriki wetu katika mafunzo haya ili hatimaye kuwasaidia
walengwa ambao ni watanzania wenetu." Alisema Dkt. Mohammed kutoka
hospitali ya Kairuki ya Mikocheni jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti
wa jopo la wataalamu walioendesha mafunzo hayo, Dkt.Robert Mhina kutoka
Taasisi ya Mifupa MOI, akizungumza wakati wa ufungaji wa mafunzo hayo
Mkurugenzi Mkuu wa WCF, Bw. Masha Mshomba, akimkabidhi cheti cha ushiriki Dkt.Arnold Mtenga
Mkurugenzi Mkuu wa WCF, Bw. Masha Mshomba, akimkabidhi cheti cha ushiriki Dkt.Aida O. Salim.
Mkurugenzi Mkuu wa WCF, Bw. Masha Mshomba, akimkabidhi cheti cha ushiriki Dkt.Alex Shuli
Dkt. Machumani Kiwanga akisikilzia kwa makini hotuba ya ufungaji
Mkuu
wa Kitengo cha Uhusiano WCF, Bi. Laura Kunenge, (kulia), akifuatilia
kwa makini hafla hiyo ya ufungaji wa mafunzo kwa wataalamu hao wa afya.
Washiriki wakisikiliza hotuba
Bw.
Masha Mshomba, (kushoto), Mkurugenzi Mkuu, WCF akiwa na Daktari bingwa
wa upasuaji na majeruhi kutoka tasisi ya Mifupa MOI, Dkt. Robert Mhina,
ambaye ndiye alijkuwa mwenyekiti wa jopo la wataalamu waliotoa mafunzo
hayo
EmoticonEmoticon