MASHAURI 18 YA MADAI YA KODI YA ARDHI YENYE THAMANI YA BILIONI 1.1 YAWASILISHWA BARAZA LA ARDHI NA NYUMBA WILAYA YA TANGA

June 24, 2017
Mwakilishi wa Kamishna wa Ardhi Msaidizi Kanda ya
Kaskazini, Ardhi Mwandamizi Thadeus Riziki akizungumza na
waandishi wa habari kuhusu Baraza la Ardhi Mkoani Tanga kupokea mashauri 18 yenye thamani ya Bilon 1.1 ambayo yamefikishwa kutokana wamiliki wa nyumba ,makazi na viwanda  kushindwa kulipa kodi ya ardhi kwa wakati

 Afisa Ardhi Mteule Halmashauri ya jiji  la Tanga Straton Thobias akielezra mkakati wa  mwaka wa fedha wa 2016/7 halmashauri imeweka lengo la  kukusanya kodi ya ardhi kiasi cha shilingi bilioni 2.5 ambapo hadi sasaimefanikiwa kukusanya shilingi bilioni 2.3
Mwanasheria wa  Ofisi ya Kamishina wa Ardhi Kanda ya Kaskazini  Rosemery Mshana akiwataka wamiliki wa ardhi wanatakiwa kilipa kodi bila shuruti na kwamba kinyume chake watafikishwa mahakamani  mujibu wa kifungu cha  50  cha sheria ardhi namba nne(4
 Mashauri 18 ya madai ya kodi ya ardhi yenye thamani ya shilingi bilioni 1.1 yamewasilishwa katika Baraza  la ardhi na nyumba  wilaya ya Tanga ikiwa ni mkakati wa Serikali wa kuwabana wamiliki wa viwanja wanao kwepa kulipa kodi.

Akizungumza mara baada ya kuwasilishwa kwa mashuari hayo mwakilishi wa afisa ardhi msaidizi kanda ya kazikazini Thadeus Riziki amesema hatua ya kuwafikisha mahakamani wamiliki wa viwanja  hivyo ni kupata kibali kitakacho wezesha wizara kulipwa makusanyo ya madeni

Amesema baada ya halmashauri kuwapelekea wamiliki hati ya madai na kushindwa kulipa hatua inayofuata ni kuwafikisha mahakamani ili kupata ridhaa ya kisheria ya kukamata mali za wadaiwa.

Kwa upande wake afisa ardhi mteule Halmashauri ya jiji  la Tanga Straton Thobias amesema katika mwaka wa fedha wa 2016/7 halmashauri imeweka lengo la  kukusanya kodi ya ardhi kiasi cha shilingi bilioni 2.5 ambapo hadi sasaimefanikiwa kukusanya shilingi bilioni 2.3

Akizungumzia zoezi hilo mwanasheria ofisi ya kamishina wa ardhi  Rosemery Mshana amesema wamiliki wa ardhi wanatakiwa kilipa kodi bila shuruti na kwamba kinyume chake watafikishwa mahakamani  mujibu wa kifungu cha  50  cha sheria ardhi namba nne(4)

Share this

Related Posts

Previous
Next Post »